Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe, akizindua Zahanati ya ya kijiji cha Vikula halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
Mwenyakiti wa Halmashauri Mh. Festo Mgina, akizindua Zahanati ya Kijiji cha Nundwe Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
Mwenyekiti
wa halmashauri akiwahamasisha wakazi wa Kijiji cha Ihalimba kuchangia
Mfuko wa CHF kabla ya kuweka jiwe la Msingi kwenye jengo la zahanati ya
Kijiji hicho.
Na
Afisa Habari Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya
Maufindi imeendelea kutekeleza sera ya serikali ya kuhakikisha kila Kijiji
kinakuwa na Zahanati kwa kuzindua na
kuweka mawe ya msingi kwenye zahanati za
Vijiji vinne kati ya vitano zilizopo kata ya Ihalimba Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi.
Uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi
umetekelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Festo Mgina, Diwani wa kata
Ihalimba Mh. Award Mahanga sanjari na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri Prof.
Riziki Shemdoe.
Taarifa hiyo imevitaja
vijiji vilivyo nufaika na huduma hiyo muhimu kwa usatawi wa afya ya jamii kuwa,
ni pamoja na Kijiji cha Wamimbalwe uwekaji wa Jiwe la msingi, uzinduzi wa
Zahanti ya Kijiji cha Vikula, uzinduzi wa zahanati ya Kijiji cha Nundwe pamoja
na uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye azahanati tarajiwa ya Kijiji cha Ihalimba.
Awali akiwahutubia wakazi wa
Vijiji hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Festo Mgina, alitoa rai kwa wananchi
kujiepusha na tabia hatarishi zinazochochea maambukizi ya Virusi vya ukimwi
huku akiutaja Mkoa wa Iringa kuwa na asilimia kubwa ya maabukizi ya 09.1 wakati asilimia ya kitaifa ni 05.6
Pekee.
Aidha, Kiongozi huyo mwenye
dhamana ya juu ya uongozi katika halmashauri hiyo, amekemea vitendo vya ubakaji
kwa Watoto ambavyo vinashamili kwa kasi Wilayani Mufindi.
Mnamo mwaka 2015 wakati wa
ufunguzi wa Bunge la Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Mh. Dk.
John Pombe Magufuli, aliahidi kuwa serikali ya awamu ya Tano itahakikisha sera
ya kuwa na zahanati kwenye kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata
inatekelezwa kwa vitendo.
0 comments:
Post a Comment