Friday, May 12, 2017

IRFA CHAWEKA HISTORIA KWA BINGWA WA MKOA

Mkuu wa wlaya ya Iringa Richard Kasesela akimkabidhi Zawadi za ubingwa wa mkoa wa Iringa kwa kapteni wa timu ya Real moja moja katika Uwanja wa kreluu
mkuu wa wlaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi wa mpira wa miguu Mkoani Iringa wakati wa kukabidhi Zawadi kwa washindi wa mkoa timu ya Real moja moja

Na Fredy Mgunda, Iringa

Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa kwa Mara ya kwanza baada ya miaka mingi kimetoa zawadi kwa bingwa wa mkoa ambayo timu ya Real moja moja wamepewa kombe na mpira miwili ili kuendelea kuboresha na kuongeza morali kwa timu shiriki zote za mkoa wa Iringa.

Zawadi hizo zimetolewa leo mbele ya mgeni rasmi Richard Kasesela katika uwanja wa chuo cha kreluu kilichopo manispaa ya Iringa huku lengo lake likiwa ni kutoa hamasa kwa virabu husika vitakavyokuwa vinashiriki michuano ya ngazi ya mkoa.

Akizungumza wakati utoaji wa zawadi hizo mkuu wa wlaya ya Iringa Richard Kasesela aliupongeza uongozi wa chama cha mpira (IRIFA) kwa kuamua kuanza kutoa zawadi kwa washidi ili kuwaongezea morali wachezaji na timu kujituma kufanya vizuri na kuchukua kombe hilo msimu ujao.

"Kuinua kwapa sio kazi ndogo ni lazima use umefanya kazi ya ziada kwenye michuano mbalimbali hasa hii ya ngazi ya mkoa ambayo huwa inakuwa migumu huku sheria zikifuatwa kwa asilimia kubwa hivyo zawadi mlizoanza kutoa leo zitaongeza nguvu kwa timu nyingine zitakazoshiliki msimu ujao wa mwaka 2017/2018" alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wachezaji wa timu ya Real moja moja kufanya mazoezi ya nguvu ili kwenda kukabiliana na timu pinzani kwenye kituo husika walichopangiwa na kurudi na ushindi ili msimu ujao mkoa wa Iringa upeleke timu nyingine ngazi ya mkoa huku Real Moja moja watakuwa daraja la pili.

Aidha Kasesela alisema kuwa anakasilishwa na mgogoro unaondelea ndani ya club ya lipuli na kuwataka viongozi kuondoa tofauti zao ili kufanikisha usajili na kuanza kambi ya timu mara moja bila kupata suluhu timu ya lipuli haitafanya vizuri katika michezo yake ya ligi juu.

"Nawaomba viongozi wa lipuli fanikisheni uchaguzi wa timu kama Tff walivyosema ili Iringa itulie na kuendelea na mambo mengine ya kuboresha timu nyingine zinazoshiriki ligi mbalimbali nazo zifanye vizuri ili baadae tuwe na timu nyingi ligi kuu na tuachane na utegemezi wa timu moja"alisema Kasesela

Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha soka Mkoani Iringa (IRFA) Dr Ally Ngalla alisema kuwa uongozi wa IRFA umepania kuendelea kuboresha timu zote zinazoshiriki ligi mbalimbali hapa Mkoani Iringa ili kuwa na timu nyingi na bora ambazo kitakuwa na tija kwa wakazi wa mpira wa miguu Mkoani Iringa.

"Ukiangalia leo ndio tumeanza kutoa zawadi kwa bingwa wa mkoa tofauti na ilivyokuwa hapo awali mabingwa walikuwa hawapewi kitu chochote kitu kilichosababisha timu nyingi kutokuwa na morali wa kujenga timu bora" alisema Ngalla

Ngalla alisema kuwa hapeni kuona timu za mkoa wa Iringa zikiwa zinafungiwa kwa chuki binafsi ambazo ndio chanzo cha migogoro mingi katika soka la Mkoani Iringa.

"Saizi nazitalata timu zote za mkoa wa Iringa kuwa uongozi na Katiba zao ili kuepukana na migogoro ya hapo baadae kama ambayo ipo saizi katika club ya lipuli "alisema Ngalla

Lakini Ngalla alisema kuwa ataendelea kuboresha zawadi za mabingwa wa mkoa ili kizifanya timu kuwa na morali na hii itaifanya Iringa kuwa mfano kwa mikoa mingine.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More