Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe kutoka makitaba ya Kitengo cha habari.
Mkaguzi
Mkuu wa hesabu za Serilkali nchini CAG ameitunuku hati safi ya hesabu na matumizi
sahihi ya Fedha za Umma Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya
ukaguzi na kujiridhisha na matumizi yaliyozingatia taratibu, Sheria na kanuni
za fedha za Umma kwa mwaka wa Fedha wa 2015 – 2016.
Taarifa
ya Afisa habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo
vya habari Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imefafanua kuwa CAG ametunuku hati hiyo kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi wa kawaida wa kila mwaka
kwa mujibu wa sheria za fedha zinazompa mamlaka ya kukagua hesabu za mamlaka za
serikali za Mitaa.
Mwakapiso,
ametanabaisha baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwenye ukaguzi huo, kuwa ni
pamoja na ujenzi wa miradi inayoendana na thamani ya fedha zilizotumika, uzingatiaji
wa sharia na taratibu za Manunuzi ya tenda, matumizi mazuri
ya fedha za miradi ya maendeleo na zile za zatumizi ya kawaida sanjari na
uandaaji wa taarifa za fedha unaozingatia viwango vya kimataifa( IPSAS)
Huu
ni mwaka wa 05 mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inapata hati safi ya
CAG. Aidha kwa mujibu wa kanuni za
ukaguzi, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mara baada ya kukamilisha ukaguzi
wake kwa mwaka wa fedha husika, anaweza kutoa moja kati ya hati zifuatazo Hati
safi, Hati yenye mashaka au Hati chafu.
0 comments:
Post a Comment