Na Mwandishi Wetu, IRINGA
WAHITIMU wa
kidato cha sita wa Sekondari ya Lugalo mkoani hapa wameiomba Serikali kuisadia kuboresha
miundombinu kwa ajili ya wanafunzi walemavu.
Katika Risala
yao kwa mgeni Rasmi wamesema pamoja na mafanikio mengi waliyoyapata kupitia shule
hiyo bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana kwa uzio, mfumo mbovu wa
maji taka kukosekana kwa karatasi maalum za walemavu wasioona pamoja na kutokuwa
na miundombinu rafiki kuwezesha kuwa salama katika mazingira ya shule kwa wanafunzi
wenye uhitaji maalum pamoja na uhaba wa waalimu wa Sayansi.
Akijibu Risala
ya wanafunzi hao, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma shuleni hapo,
Nayman Chavalla, kupitia kampuni inayoitwa Lugalo Associate Company Limited
wameanza kukarabati nyumba ya Mkuu wa shule pamoja na ya Makamu wa shule na kuahidi
kuwa umoja huo utaendelea kusaidia shule hiyo endapo matokeo ya taaluma yataboreshwa.
Chavalla ameongeza
kuwa Umoja huo unayo nia ya dhati katika kusaidia kutatua changamoto za elimu shuleni
hapo na kuwataka walimu kufuta daraja sifuri na daraja la nne katika matokeo ya
kitaifa ili kuleta motisha kwa wadau wanaochangia maendeleo ya shule.
Pia amesema
pamoja na kuwa Serikali inahamasisha Elimu Bure lakini bado jukumu la kujibidiisha
katika masomo na kuinua viwango vya ufaulu ni la Mwanafunzi na waalimu wenyewe katika
kukuza taaluma yenye viwango.
Mmoja wa wahitimu
mwenye ulemavu wa macho, Elizabeth Mwaisoba mwenye umri wa miaka 18 amesema kuna
haja kwa Serikali kuendelea kusaidia wazazi wenye watoto wenye uhitaji maalum katika
kupata elimu kwani inahitaji kipato kikubwa katika kuwahudia wanafunzi wenye uhitaji
wa ziada na kuiomba Wizara husika kutillia mkazo suala la komputa zenye sauti ili
nao waweze kwenda sambamba na teknolojia ya sasa.
Felista Mkesela,
mwenye ualbino, amesema ipo haja ya waalimu kuona umuhimu wa kuweka vifaa vya kukuza
maandishi ya ubaoni na kuongeza muda wa ziada kwa wanafunzi walio na ulemavu wawapo
darasani, kwani kuwapa muda sawa na wanafunzi wa kawaida kunaathiri kufanya vizuri
katika masomo yao.
Mkuu wa Shule
hiyo, Benjamin Kabungo, amesema kwa sasa
shule hiyo ina wanafunzi 63 wenye ulemavu wakiwemo wasioona, albino, wenye uoni
hafifu, na walemavu wa viungo na kwamba walimu 4 wa Elimu Dumishi, awali Shule hiyo
ambayo ilianzishwa mwaka 1945 na kujulikana kama The H.H Aga Khani, pia imeanzisha
ufugaji wa viumbe wakiwemo panya weupe kwa ajili ya kufanya utafiti wa Kisayansi.
0 comments:
Post a Comment