Mkurugenzi wa kituo cha
kuendeleza soka cha Iringa (IFA) Ally
Msigwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akielezea mipango yake ya kuinua soka la vijana mkoani Iringa na Nje ya mkoa wa Iringa.
Mkurugenzi wa kituo cha
kuendeleza soka cha Iringa (IFA) Ally
Msigwa akionyesha jinsi ambavyo nembo ya puma iatapoa kwenye jezi za kituo hicho
Mkurugenzi wa kituo cha
kuendeleza soka cha Iringa (IFA) Ally
Msigwa akiwa na kocha mkuu wa kituo hicho mwalimu Saleh molelikatika ofisi za IFA mkoani Iringa
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
KITUO cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)
kimefanikiwa kuingia mkataba wa udhamini wa wa jezi na vifaa vya michezo kwa
muda wa miaka miwili na kampuni ya mafuta ya Puma Energy.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa kituo cha
kuendeleza soka cha Iringa (IFA) Ally
Msigwa, alisema kuwa kituo hicho kimepata udhamini wa vifaa vya michezo kutoka kampuni
hiyo na udhamini huo utakijita kwenye safari zote za timu inapoelekea katika
michezo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.
Msigwa alisema kuwa kituo hicho kimekuwa kimbilio la
vijana wengi wenye vipaji na kimefanikiwa kupata ufadhili wa kudumu kutoka kwa kampuni
ya Alishati Investment ambayo itafadhili mahitaji mbalimbali katika kituo
hicho.
Alisema kuwa kituo hicho ambacho kimekuwa
kikubwa kwa sasa kina mahitaji mengi ambayo yanahitajika katika kujikimu na kwa
sasa kinatarajia kuwa na uwanja wake maeneo ya Ifunda kata ya Lumuli wilaya ya
Iringa ambapo ujenzi wake uko katika mchakato kuanza baada ya kila kitu
kukamilika.
Msigwa ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Yanga
alisema kuwa katika ujenzi wa uwanja wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa
utakaochukua watu zidi 5000 hivyo kuwa moja ya viwanja bora kabisa kwa upande
wa Nyanda za Juu Kusini.
Msigwa Aliongeza kuwa uongozi wa kituo hicho umeeamua
kuunda bodi ya wakurugenzi ambao watasaidiana katika kufanikisha ndoto
mbalimbali za kukuza soka la vijana nchini Tanzania ambapo Dk. Mshindo Msola
ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wa kituo hicho na kocha Salehe Molel kuwa
kocha wa vijana chini ya miaka 15 hadi 17.
Aidha Msigwa alisema kuwa IFA imefanikiwa kuteua
wajumbe wa bodi ambapo itaongozwa na Augustino Mahiga Waziri wa Mambo Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu ofisi
ya Msajili Hazina Wizara ya Fedha Gerald Mwanilwa.
Wengine watakaounda wajumbe wa bodi ni Ezra Chomete
mtanzania mwenye makazi Marekani, Abdul Mapembe ambaye ni Meneja TRA Ilala,
Mhindisi Patrick Mbendule na Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa,
Cyprian Kuyava.
Naye kocha mkuu wa kituo hicho mwalimu Saleh moleli
alisema kuwa amepata sehemu sahihi ya kuujenga upya mpira wa mkoa wa Iringa kwa
kuwa hapo awali alikuwa kocha anayefundisha timu za wakubwa tu.
“Kupata nafasi hii kwangu kama kocha mzoefu nimefarijika
sana,nitakikisha naitumia vilivyo kwa kuahikisha mpira wa vijana unakuwa na
kuzailisha kizazi cha soka hapa mkoani Iringa na duniani kwa ujumla” alisema
Moleli
Moleli alisema kuwa watahakikisha vijana wote
watakokuwa kwenye kituo hicho watapata elimu bila wasisi wowote ule.
“Wazazi wengi wamekuwa wakiwazuia watoto wao kukuza
vipaji vyao kwa kuhofia kutoendelea na masomo yao lakini kwenye mpingo yetu
kutakuwa na shule ambayo itawasaidia wanafunzi kusoma wakiwa hapo kituoni”
alisema Moleli
0 comments:
Post a Comment