Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Albert Chalamila akitema cheche kwa uongozi wa UWT mkoa wa Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa
CHAMA cha mapinduzi (CCM)
mkoa wa Iringa kimeagiza jumuiya umoja wa wanawake wa chama hicho (UWT)
kusimamia vyema fedha walizopewa na Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas kwa ajili ya kuimarisha miradi yao ya
maendeleo yaliyokusudiwa na sio kuzitafuna kama njugu na kwa malengo yao binafsi.
Agizo hilo
limetolewa na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa Albart chalamila wakati
akizungumza na umoja wa wanawake wa chama hicho na kuongeza kuwa wanataka jumuiya hiyo iwe imara hivyo inatakiwa kuwa na
uchumi imara ambayo itawawezesha kutimiza majukumu yanayotakiwa kama ambavyo
wamepanga kufanya shughuli za kukuza uchumi.
Pia Chalamila
alitoa angalizo kwa kiongozi yoyote wa umoja huo ambaye atatafuna fedha za miradi
ya maendeleo au kukwamisha maendeleo atawajibishwa kwa mujibu wa sheria za
chama ikiwa ni kufukuzwa uwanachama pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya
dola.
Alisema kuwa CCM ya sasa sio ya kuishi
kimazoea kama iliyokuwa miaka iliyopita hivyo kila fedha itakayotolewa kwa
ajili ya maendeleo ya chama itafuatiliwa hadi senti ya mwisho.
Niwaeleze
ukweli CCM ya sasa sio kama ya miaka iliyopita miaka ya nyuma fedha nyingi
zilikuwa zikitumiwa ndivyo sivyo sasa nikiwa kama mwenyekiti wa CCM mkoa
nitahakikisha kufuatiliya hadi senti ya mwisho kwa lengo la kuhakikisha fedha
zilizotolewa zinatumiwa kwa amalengo yaliyokusudiwa.”
Aidha Chalamila alisema
ili jumuiya hii iwe imara inatakiwa kuwa na uchumi imara ambayo itawawezesha
kutimiza majukumu yanayotakiwa kama ambavyo wamepanga kufanya shughuli za
kukuza uchumi.
Lakini Chalamila alisema
MNEC Salim Asas amekuwa mdau mkubwa kwa kuchangia maendeleo ya chama cha
mapinduzi na serikali kwa ujumla kwa lengo la kuboresha maendeleo na kuokoa
maisha ya watanzania wengi wenye kipato cha chini.
“Amesaidia sana kuboresha
sekta ya afya ,sekta ya elimu,sekta ya utalii na sekta ya miundumbinu hapa mkoani
Iringa na kusaidia kuokoa maisha ya wananchi na kuongeza ukuaji wa uchumi wa
mkoa wa Iringa kwa ujumla” alisema Chalamila
MNEC salimu Asas
anafanya kazi kubwa sana na hapaswi kubezwa hata kidogo kwa kazi zake za
kuchangia maendeleo kwa wananchi wa kawaida hata wanachama wa chama cha
mapinduzi ,hivyo ni muhimu kuhakikisha tunampa ushirikiano wa kutosha ili
aendelee kuchapa kazi
Awali akizungumza mjumbe wa
halmashauri kuu ya taifa ya Chama hicho MNEC Salim Asas alikabidhi kiasi cha
zaidi ya Millioni 40 kwa umoja huo kwa lengo la kuimarisha miradi ya chama.
Mnec alisema kuwa amekabidhi fedha hizo ambazo
zitatumika kwa ajili ya kuanzisha miradi mipya na kukuza uchumi na kuacha kuwa
omba omba.
“Zimetolewa fedha
nyingisana hapa kwa ajili ya kukuza uchumi wa jumuiya hii kwa mkoa mzima hivyo
mnatakiwa kuzitumia kwa malengo na sio kuzitafuta kama njugu.” alisema Asas
Katika hatua nyingine
mwenyekiti huyo alitoa angalizo kwa umoja huo wasitumie fedha hizo kuanzisha
migogoro kwenye jumuiya yao.
“Lengo letu ni kuhakikisha
kuwa tunaijenga CCM mpya ambayo itawaletea maendeleo wananchi wa mkoa wetu kwa
sababu leo hii mnec ametusaidia na amekuwa mdau mkubwa sana,amechangia sekta
mbalimbali ikiwamo afya,maji,elimu kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania
wanaoishi ndani ya mkoa wetu.”alisema Chalamila
Akizungumza mwenyekiti
wa (UWT) mkoa huo Nikolina Lulandala licha ya kushukuru kupokea fedha hizo
alisema atasimamia kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na hakuna
hata senti itakayoptea kwa sababu wanataka kuwaletea wananchi maendeleo.
Lulandala alisema kuwa wanataka
kuleta maendeleo kwa wananchi waliwaamini na kuwapa kura hivyo hawana budi
kutorudisha fadhili lakini kubwa kuliko yote ni kuhakikisha 2020 wanakomboa
jimbo la Iringa mjini ambalo linamilikiwa na mbunge wa jimbo hilo Mch.Peter
Msigwa.
0 comments:
Post a Comment