Kamanda wa taasisi ya
kuzuaia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa
wa Iringa Aidan Ndomba akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea juu ya
kilichotokea katika kipindi cha Julai hadi
Desemba 2017.
Baadhi ya viongozi wa takukuru na waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa taasisi ya kuzuaia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa Aidan Ndomba
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa taasisi ya kuzuaia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa Aidan Ndomba
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Taasisi ya kuzuia
na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Iringa imepokea jumla ya malalamiko 91
ya rushwa kutoka kwa wananchi katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2017.
Hayo
yamezungumzwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa Aidan Ndomba alipokuwa akitoa
taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU Mkoani hapa katika kipindi cha mwezi Julai
hadi disemba 2017 na kuongeza kuwa katika sekta ya TAMISEMI kumekuwa na
malalamiko 18.
Ndomba alisema kuwa taasisi imechunguza
miradi nane ya sekta ya elimu ,maji na barabara yenye
thamani ya takribani bilioni 2.5 katika wilaya ya
Iringa , Mufindi na Kilolo baada ya kuwepo kwa dalili ya
matumizi mabaya ya fedha za za miradi hiyo .
alisema ndani
ya kipindi hicho ofisi yake ilifuatilia na
kufanya ukagzi wa fedha za miradi nane ya
maendeleo katika sekta za elimu ,maji na barabara yenye
thamani ya takribani shilingi bilioni 2,588,000,000 na kubaini
mapungufu katika miradi yenye thamani ya shilingi milioni 818
ambapo uchunguzi wa matumizi ya fedha za miradoi
umeanzishwa.
Alisema kuwa
miradi miwili ilifuatiliwa na kukaguliwa katika
Halmashauri ya Iringa na ina thamani ya
shilingi 1,164,614,899 iliyopo katika kijiji cha
Mfyome kata ya Kiwere na Malizanga
kata ya Mlowa huku miradi mitatu iliyofuatiliwa
na kukaguliwa ipo katika Halmashauri ya Kilolo
ina thamani ya shilingi 908,138,034 kuwa miradi hii ipo
kijiji cha Ng'uruhe , Irindi, na Ipalamwa .
Ndomba alisema kwa
upande wa barabara miradi miwili ilifuatiliwa na kukaguliwa
katika wilaya ya Mufindi na ina thamani ya shilingi
407,343,774 na kuwa miradi hiyo ni pamoja na barabara za Maduma
-Tambalang'ombe na Maguhani - Udumka .
wakati kwa wilaya
ya Kilolo kuna mradi mmoja wa barabara
wenye thamani ya shilingi 107,343,774 umefuatiliwa
na kukaguliwa mradi huu ni ule wa Ilula ujulikanao kama
KItelewasi - Ilambo .
Ndomba alisema kuwa baadhi
ya sekta zilizolalamikiwa ni pamoja na TAMISEMI (
Halmashauri na serikali za mitaa,vijiji )
kwa kuwa na malalamiko 18 , jeshi la polisi
malalamiko 12 na mabaraza ya ardhi malalamiko 8.
Aidha Ndomba alisema
mashauri mawili yalikamilika kwa kutolewa
hukumu katika shauri namba CC 03/2017 kati ya Jamhuri
na Upendo Mponzi (VEO- Ilula) na mwenzake
Tulinutwa Alphonce Mlangwa ambae ni diwani
wa kata ya Kipaduka wote wakiwa ni watumishi
wa umma hakimu wa mkoa wa Iringa John
Mpitanjia aliwatia hatiani wote na kuhukumiwa
jela miezi 6 ama kulipa faini ya shilingi 300,000 kila mmoja .
Pia alisema
katika shauri la pili namba CC.39/2016 mshtakiwa
Selemani Futani ambae ni mfamasia msaidizi wa Halmashauri
ya Mufindi aliachiwa huru na mahakama ya
wilaya ya Mufindi hata hivyo upande wa Jamhuri
(Takukuru) wamekata rufaa mahakama kuu .
Kamanda
Ndomba alisema kwa kipindi hicho Takukuru
mkoa wa Iringa imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 100,000
baada ya kubaini kuwa kiasi hicho cha fedha zilikuwa
zilipwe mahakamani kama faini zilitumiwa na mtumishi
binafsi wa mahakama badala ya kuziingiza kwenye
mfuko wa serikali .
Hivyo
amewataka wananchi kuendelea kufika ofisini kwake
ama ofisi za wilaya kutoa taarifa mbali
mbali za rushwa ama kutumia simu 0784606519/0754606519
ama kupiga simu ya bure 113 au *113# kupitia
huduma ya longa nasi kwa ujumbe mfupi SMS 113
0 comments:
Post a Comment