Monday, April 16, 2018

UONGOZI WA TIMU YA SINGIDA UNITED WAMEWATAKA WAKULIMA WA MKOANI IRINGA KUTUMIA MBOLEA YA YARA

 Meneja wa timu ya Singida United ya mkoani Singida Ibrahim Ahamed akiwa kwenye shamba darasa ambalo lipo katika kata ya Ruaha mkoani Iringa
 Wachezaji na viongozi wa timu ya Singinda United wakiwa kwenye shamba darasa ambalo mahindi yake yamepandwa kwa kutumia mbolea ya Yara ambayo pia kampuni hiyo ya Yara Tanzania inawadhamini pia timu hiyo ya Singida United
 Wachezaji na viongozi wa timu ya Singinda United wakiwa kwenye shamba darasa ambalo mahindi yake yamepandwa kwa kutumia mbolea ya Yara ambayo pia kampuni hiyo ya Yara Tanzania inawadhamini pia timu hiyo ya Singida United
Moja ya shamba shamba darasa lilopo katika kata ya Ruaha mkoani Iringa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Uongozi wa timu ya Singida United ya mkoani Singida umewataka wakulima wa mkoani Iringa kulima kilimo bora kwa kutumia mbolea ambazo zinazalishwa na kampuni ya Yara iliyopo kulasini jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ruaha manispaa ya Iringa wakati kikosi cha wakulima alizeti kilipo watembelea wakulima wanaotumia mbolea za kampuni ya Yara kwenye shamba darasa lilipo katika kata hiyo, meneja wa timu hiyo Ibrahim ahamed alisema kuwa wataendelea kutoa elimu ya kilimo bora kwa kushirikiana na wananachi ili kuhakikisha wanalima kilimo chenye faida kubwa kuliko wanavyofanya sasa wakulima wengi.
“Wananchi wengi wanapenda kulima lakini bado hawafuati taratibu na kanuni za kilimo bora hivyo atahakikisha kupitia kampuni ya Yara wanatoa elimu kwa wakulima ili kuwakomboa katika kilimo wanacholima kwa sasa hadi kufikia kulima kilimo cha kisasa na chenye faida” alisema  
Ahamed aliwataka wakulima kutumia mbolea za kampuni ya Yara ambazo kwa sasa ndio imekuwa mkombozi wa wakulima kwa kuzalisha mazao mengi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
“Mbolea za kampuni ya Yara zinavirubisho ambavyo vinasaidia mazoa kukuwa na kuzalisha mazao mengi ambayo yanakuwa faida kwa wakulima”
Timu ya Singida United inadhaminiwa na kampuni ya Yara ambayo inazalisha mbolea bora kwa sasa hapa nchini na imekuwa kipenzi cha wakulima wengi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More