Baadhi ya viongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda loa katika viwanja vya kichangani manispaa ya Iringa na kuwataka wanachama kununua hisa kwa wingiili nao wawe wamiliki wa taasisi na kufanikiwa kuwa na maamuzi ya chama hicho kwa maendeleo ya mwanachama
Baadhi ya wananchi na viongozi walipokuwa wakibadilishana mawazo kwenye banda la TALGWU
Baadhi ya viongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda loa katika viwanja vya kichangani manispaa ya Iringa.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wanachama wa chama cha
wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU) wametakiwa kujiandaa kununua hisa hapo baadae za TALGWU microfinance PLC ili nao wawe wamiliki wa taasisi na kufanikiwa kuwa na maamuzi ya chama
hicho kwa maendeleo ya mwanachama.
Akizungumza hii leo kwenye
banda TALGWU katika maonyesho ya kuelekea mei mosi,mkurugenzi mtendaji wa
microfinance PLC Jackson Ngalama alisema kuwa mwananchama wa TALGWUakinunua
hisa atakuwa atapata gawio la kila mwaka kutoka na faida ambayo itakuwa
imetengenezwa kwa kipindi hicho kutoka katika kampuni ya TALGWU microfinance PLC.
Ngalama alisema kuwa wananchama
aliye na hisi katika kampuni ya TALGWU microfinance PLC ataruhusiwa kukopa kwa
riba nafuu ambayo itamuongezea kufanya maendeleo binafsi tofauti naakienda
kukopa sehemu nyingine.
“Sisi tunamlinda na kumheshimu
mwanachama wetu hivyo hata akikopa atapewa elimu ya jinsi ya kutumia mkopo wake
kwa faida maana tumeona watu wengi wakikopa huwa inakuwa vigumu kujua amekopa
kwa ajili ya nini hivyo tumeamua kuta elimu kwanza ili kumfanya awe mwanachama
mwenye mafanikio makubwa” alisema Ngalama
Ngalama alisema kwa sasa hisa
zinatarajiwa kuuzwa kwa shilingi elfumoja na mwananchama anatakiwa kuanza kununua hisa za
shilingi elfu hamsini na kuendelea ili kuongeza thamani ya kampuni hiyo na
mteja wake anayetumtumia na kupata huduma hiyo.
“hisa zetu zinatarajiwa kuanza kuuzwa hivyo naomba nitoe rai kwa wanachama wetu wote waanze kujiandaa kununua hisa ambazo
zitauzwa kwa gharama nafuu ya shilingi elfu moja tu.
Wakati huo huo afisa habari wa
TALGWU Shani Kibwasali alisema kuwa TALGWU imekuwa ikiboresha na kuendeleza
hali nzuri za wanachama wakiwa kazini,kuondoa tofauti zinazojitokezakati ya
mwajiri na mwajiriwa wakiwa kazini na
kuwarudisha kuwa wamoja na kuendelea kufanya kazi na kuleta maendeleo.
“Sisi kazi yetu kuhakikisha
mwanachama wetu anapata haki zakezote za msingi hivyo tunaposikia kunamgogoro
mahali inatupaswa kwenda kuutatua na kuhakikisha kila mtu anapata haki yake”
alisema Kibwasali
Kibwasali alisema kuwa TALGWU
imefanikiwa kuishawishi serikali kuwarudisha wafanyakazi waliokuwa wamefukuzwa
kazi mwaka 2017 kwa kuwa walikuwa wanaelimu ya kidato cha nne,mwaka 2016 hadi
2017 walishinda jumla ya kesi 37 zilizokuwa zinawakabili wanachama wakena pia
walisimamia kutolewa kwa muundo mpya wa mwaka 2013/2014 wa watendaji wa
kata,mitaa na vijiji.
Aidha Kibwasali alisema kuwa
TALGWU imeweka mikakati ya mwaka 2016 hadi 2021 kwa kuhakikisha inawaunganisha
wanachama wote kuwa kitu kimoja,kujenga na kuhimiza wanachama kuwa wawajibikaji
wakiwa makazini,kuimalisha chama kiuchumi ili kutoa huduma inastahili kwa
wanachama,kufanya ziara ya mara kwa mara ili kujua kero na changamoto mbalimbali
zinawazowakabili wanachama wake
0 comments:
Post a Comment