Friday, April 20, 2018

RC MASENZA: MAANDALIZI YA MEI MOSI YANAENDELEA VIZURI NA MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA RAIS DR JOHN POMBE MAGUFULI


 Mkuu wa Iringa Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maandalizi ya siku ya Mei mosi yatakayofanyika mkoani Iringa kitaifa huku Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mkoani hapa.




 Baadhi ya waaandishi wa habari wakiwa makini kuandika alichokuwa anakisema mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza

NA FREDY MGUNDA,IRINGA

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mkoani Iringa.


Katika mkutano wake na waandishi wa habari mkuu wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa kuelekea siku hiyo ya wafanyakazi Mei Mosi Iringa kutaambatana na matukio mbalimbali ikiwemo semina,michezo na makongamano yatakayofanyika katika wilaya zote za Iringa.


“Kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ya mei mosi mwaka 2018 kutakuwa na michezo mbalimbali itakayokuwa inachezwa katika viwanja mbalimbali hapa mkoani Iringa na michezo hiyo ni kama ifuatayo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba,bonanza la michezo mbalimbali na michezo hii ilianza tarehe 17 /04 /2018  na itahitimishwa 30 /04 / 2018” alisema masenza


Akielezea  juu ya maandalizi ya  sherehe  za mei  mosi  mkoani  Iringa  alisema  kwa  sehemu  kubwa   maandalizi yanakwenda  vizuri na  wamepata  ratibu ya  kuzunguka  wilaya  zote za  mkoa  wa Iringa kutoa elimu  pamoja na kututana na  wafanyakazi ili  kujua  changamoto  zao.

“Tumejiridhisha kuwa kila kitu kinaenda kama tulivyopanga ndio maana leo tunahuru wa kusema kuwa mei mosi itafanyika kwa mafanikio makubwa mno” alisema

 Hata hivyo  Masenza aliwataka  wafanyakazi   kujitokeza  kwa  wingi  kushiriki sherehe  hizo  na  kuwa  kupitia sherehe  hizo  watapata fursa ya  kujua  mikakati ya  serikali  dhidi ya wafanyakazi  hapa nchini.


Kila mwaka sherehe hizi hufanyika na kuambatana na kauli mbi yake,mwaka huu kauli mbiu inasema “KUUNGANISHWA KWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI KULENGE KUBORESHA MAFAO YA WAFANYAKAZI”


Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli kutua Iringa tangu kuchaguliwa kwake kuwa Rais mwaka 2015

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More