Friday, December 29, 2017

MBUNGE MGIMWA AMEKABIDHI MIFUKO 400 YA SARUJI NA BATI 150 KWA AJILI YA UJENZI NA UKARABATI WA MAJENGO YA SHULE NA ZAHATI ZA KATA YA MAPANDA

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Mapanda Obed Kalenga na mwenyekiti wa kijijicha Ihimbo wakati wa kueleza vitu gani ambavyo amevifanya kwenye kata hii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata ya Mapanda
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya darasa ambalo litakarabatiwa kutumia mfuko wake wa jimbo ili liwe kwenye kiwango kinachotakiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa  akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua majengo ya shule na kuangalia majengo yapi yanastahili kukarabatiwa
 Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya zahati ambayo inatakiwa kufanyiwa ukarabati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Mapanda

 Na Fredy Mgunda,Mufindi.

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa   amekabidhi  jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi pamoja na zahati za Kata ya Mapanda kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kule kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Nimetoa jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule na zahati za kata hii ikiwa ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine na bati hata vitu vingine ili kulifanya jimbo la Mufindi Kaskazini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa halmashauri ya Mufindi imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata maji ya kutosha na kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hiyo kwa kufanya maendeleo.

“mimi lengo langu inapofika kipindi cha uchaguzi ninakuwa nimetatua kero zote za wananchi na kujihakikishia napewa ridha ya kuongoza kipindi kingine kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini na kuongeza kuwa hatakusikia kuwa kuna kitu kinasababisha migogoro ya kugombea ardhi katika jimbo hili la Mufindi Kaskazini” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa shule na zahanati zilizopata saruji na mabati ni shule za kijiji cha Mapanda,shule ya kijiji cha Uhafiwa,Ukama,Ihimbo na Chogo lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mgimwa amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata na ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la Mufindi Kaskazini na kutatua kero nyingine za wananchi wa jimbo hilo.

Obedi Madembo, Peter Kaguo, Kristopher Ngunda,Thobias Luvinga na Fransisco Mfaume ni wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatafutia wananchi mandeleo kwa kutumia nguvu zake zote.

“Hata ukiangalia mwandishi utagundua gharama alizozitumia mbunge zimewaondolea wananchi kuchangia kabisa hivyo bila mbunge huyu mzigo wote huu ulikuwa unawaangukia wananchi wa vijiji vyote vya kata ya Mapanda” walisema wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda

Kwa upande wake diwani kata ya Mapanda Obed Kalenga alimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo ili andelee kufanya kazi ya kuwatafutia maendeleo wananchi wa kata ya Mapanda na jimbo la Mufindi Kaskazini kwa ujumla.

“Wananchi kweli wananjitoa sana kufanya kazi za kuleta mandeleo hiyo wanapoona kuwa mbunge naye anatumia nguvu kubwa kufanya maendeleo kutaongeza chachu ya kufanya kazi kwa kujitolea kwenye shughuli za kimaendeleo hata mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi na ukarabati wa shule na zahati ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo na kupatikana kwa huduma za afya bora kwa wananchi wote” alisema Kalenga

Tuesday, December 26, 2017

MBUNGE RITTA KABATI ASHEREKEA SIKU YA KUZALIWA KWAKE NA WATOTO WA KANISA LA KKT KIHESA IRINGA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akitoa neno kwa watoto waliojitokeza kwenye sherehe yake ya kuzaliwa na kuamua kusherehekea nao katika kanisa la KKT Kihesa manispaa ya Iringa.
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikata keki tayari kwa kuwalisha watoto waliokuwa wamejitokeza kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwalisha keki waliokuwa wamehudhuria sherehe hiyo
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akilishwa keki na mmoja wa mtoto waliokuwa wamejitokeza kushiriki naye  kwenye sherehe ya kuzaliwa kwake
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akilishwa keki na mmoja wa mtoto waliokuwa wamejitokeza kushiriki naye  kwenye sherehe ya kuzaliwa kwake
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliohudhuria sherehe ya kuzaliwa kwake

WANANCHI JIJINI DAR ES SALAAM WAIPONGEZA KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu (kulia), Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga  na Dk. Mohamed Mohamed wa ugonjwa wa Kisukari katika hospitali hiyo wakikata keki maalumu iliyotengenezwa kwa bidhaa za Sugar Free zisizo na sukari wakati wa uzinduzi  wa bidhaa hizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

 Muonekano wa keki hiyo iliyotengenezwa kwa bidhaa hizo zisizo na sukari.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza bidhaa hizo. (Kwa maelezo zaidi kuhusu bidhaa hizo piga simu namba 0784834010)
Hii ndiyo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale



WANANCHI jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake wameipongeza  Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kwa kuwaletea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari kwenye vyakula.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam walisema kampuni hiyo haina budi kupongezwa kwa kuzileta bidhaa hizo katika soko la Tanzania ili kukabiliana na changamoto ya matumizi kupitia vyakula.

"Hivi sasa kila pembe ya nchi yetu kumekuwa na changamoto ya ugonjwa wa kisukari ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na mfumo wa ulaji na unywaji wa vyakula vyenye sukari kupita kiasi kwa bidhaa hizi mpya zinazosambazwa na Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD hakika itasaidia sana" alisema Frank Erasto mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam.

Erasto alisema yeye ni mihongoni mwa waathirika wa ugonjwa wa kisukari lakini tangu bidhaa hizo ziingie katika soko la Tanzania amekuwa akitumia bidhaa hizo ili asiongeze sukari mwilini mwake baada ya kupata matibabu.

Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina moaja la Reuben alisema familia yake imeanza kutumia bidhaa hizo ambazo hazina gharama kubwa.

"Familia yangu na marafiki zangu tumeanza kutumia bidhaa hizi za Sugar Free kusema kweli ni nzuri na zina radha kama ile zilizopo kwenye chakula halisi" alisema Reuben.


Mkazi wa Kariakoo Happyness Kimaro alisema kwake anaona bidhaa hizo ni mkombozi kwani ameanza kuzitumia baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari na hapendi kuongeza sukari mwilini mwake.

"Sisi wagonjwa wa kisukari tumekuwa na changamoto kubwa ya ulaji wa vyakula mara tunaambiwa tusile hiki na kile tule vyakula ambavyo havina sukari ambavyo havina ladha sasa kwa kuletewa bidhaa hizi tunasema ni nafuu kwetu" alisema Kimaro.

Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 


Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.

"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.

Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).


Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.


Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 


Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.


Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.

TANESCO YAFURAHISHWA NA HATUA ZA SERIKALI KULINDA VYANZO VYA MAJI YA KUFUA UMEME

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
INAELEZWA kuwa umeme wa maji, (Hydro power) ndio umeme wenye bei nafuu zaidi ukilinganisha na umeme unaotokana na vyanzo vingine.
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa TANESCO anayeshughulikia uzalishaji (Power Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, matumizi ya juu ya umeme nchini kwa sasa ni Megawati 1,060, kati ya hizo, TANESCO kwa kutumia mitambo yake, huzalisha Megawati zaidi ya 1,000, na kati ya hizo, Megawati 381 zinatokana na umeme unaozalishwa kutokana na maji, (Hydro powere) kutoka vituo vinne vya umeme wa maji vya Kidatu, Mtera, New Pangani Falls, Hale na Nyumba ya Mungu.
Hata hivyo katika siku za karibuni shughuli za kibinadamu zimekuwa zikiongezeka kwenye vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye vituo vya kufua umeme, na hivyo kutishia shuhghuli za uzalishaji umeme kwenye vituo hivyo.
Mhandisi Ikwasa alitoa mfano Mto Pangani ambapo yapo maeno ambayo shughuli za kilimo zinaendelea karibu na mto, na madhara yatokanayo na shughuli hizo hupelekea kingo za mto kuwa dhaifu na wakati wa mvua maji yanachukua udongo na kuingiza kwenye mto na hivyo kina cha mto kinakuwa kifupi.
“Sasa kipindi ambacho mvua zinanyesha unatarajia maji mengi yatiririke kwenye mto lakini kwa sababu kina kimepungua mto hauwezi kubeba yale maji na badala yake maji yanasambaa na kusababisha mafuriko na mbaya zaidi hayafiki kwenye mabwawa kwa kiwango kinachohitajika.” Alisema Mhandisi Ikwasa.
Alisema TANESCO kama wadau wakubwa wa maji wamekuwa wakishirikiana na mamlaka zinazosimamia mabonde, ili kuelimisha watumiaji wengine wa  maji.
“Tunataka kuhakikisha kwamba, kunakuwepo na matumizi endelevu ya maji, tunatambua wananchi wanahitaji maji kwa kilimo na sisi tunayahitaji kwa uzalishaji umeme kwa hivyo yakitumika vizuri yanaweza kufanya kazi zote.” Alisema.
Mhandisi Ikwasa aliipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazochukua kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.
“Makamu wa Rais aliunda kikosi kazi cha kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa na juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda.” Alisema.
Ili kuhakikisha wananchi wanajenga dhana ya umiliki wa miundombinu ya TANESCO, Shirika limekuwa likishirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia kutoa huduma za afya, elimu ya awali na usafiri katika maeneo yanayozunguka vituo vya kuzalisha umeme.

“Tunataka wananchi wafahamu kuwa pamoja na kwamba kazi yetu ni kuzalisha umeme, lakini tunataka tuwe sehemu ya maisha yao, kwa kusaidia mambo ya kijamii kama vile kutoa elimu bure ya awali, zahanati, na usafiri wa basi unaosaidia wananchi kusafiri kuelekea kwenye shughuli zao, tunadhani kwa ushirikiano huu, wananchi watakuwa wakwanza kulinda miundombinu yetu na pia kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwenye vyanzo vya maji.” Alisema Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.
Ili kuhakikisha ujumbe huo pia unawafikia wananchi wote kupitia vyombo vya habari, wahariri wa vyombo vya habari walipata fursa ya kutembelea vituo vya kufua umeme wa maji vya Hale, New Pangani na Nyumba ya Mungu, vilivyoko mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, kituo cha Mtera kilichoko mkoani Iringa na Kidatu mkoani Morogoro ili hatimaye watoe elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya vyanzo vya mito ambayo maji yake ndio huelekea kwenye vituo vya kufua umeme.
 Meneja wa kituo cha kufua umeme wa maji cha Kidatu, Mhandisi Anthony Mbushi, (kushoto), akizungumza kuhusu jinsi mageti ya kuruhusu maji kwenye mabwawa kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yanavyofanya kazi. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme. Mhandsisi Abdallah Ikwasa.
 Wananchi wa Kidatu, wakisub iri usafiri wa basi la Shirika la Umeme TANESCO, kuwapeleka kwenye mnada ili kuuza mazao yao. Usafiri huo hutolewa bure na Shirika katika mpango wake wa Corporate Social Responsibility (CSR) ili kujenga uhusiano mwema.
 Moja ya mashine za kufua umeme wa maji, (turbine), kituo cha Hale.
 Wasimamizi wa kituo cha kudhibiti mfumo wa umeme cha Mtera.
 Bwawa la New Pangani Water Falls.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza jambo.
Mhandisi Mahenda S.Mahenda, Meneja vituo vya kufua umeme vya Pangani Hydro Systems, akifafanua jambo.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA SIKUKUU YA KRISIMASI

Na Jumia Travel Tanzania



Ule msimu wa watu kufurahi na kujumuika umewadia tena!




Haina ubishi kwamba sikukuu na mapumziko ya mwisho wa mwaka ambayo huambatana na sikukuu za Krismasi (Desemba 25) na mwaka mpya ndiyo huwa na shamrashamra nyingi zaidi duniani.




Ni kipindi hiko ndicho familia, ndugu, jamaa na marafiki hukutana kwa pamoja na kufurahia kuumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mpya unaofuatia. Mbali na hilo, kutokana na shughuli za mwaka mzima katika kutafuta kipato na kujenga maisha, hiki ni kipindi ambacho watu hupumzisha mwili na akili kwa kufurahia matunda waliyoyachuma kwenye kipindi cha mwaka mzima lakini hata kutafakari namna watakavyoukabili mwaka mpya ambao huja na majukumu na matarajio mapya.



Katika kipindi hiki cha sikukuu mambo mengi hutokea ambayo kwa namna moja ama nyingine endapo hautokuwa makini yatakuacha kwenye hali mbaya. Jumia Travel ingependa kukumbusha wakati ukiwa kwenye ari ya shamrashamra za msimu huu wa sikukuu kuepuka kuyafanya mambo yafuatayo.




Tumia muda wa kutosha na familia. Itapendeza endapo sikukuu ya Krisimasi na mapumziko ya mwisho wa mwaka ukazitumia kufurahia na familia yako. Ni kipindi ambacho miongoni mwenu mpo likizo, watoto wamefunga shule na ndugu hupata fursa ya kutembeleana. Ni jambo la kawaida kuona watanzania mbalimbali kilo kona ya nchi wakifurika kurudi makwao au wengine wakialikana ili kufurahia kipindi hiki. Kamwe usiipoteze fursa hii ya kujumuika na wale uwapendao kwani hutokea mara moja tu kwa mwaka na ni vema ukaitumia ipasavyo.



Zingatia kiwango na aina ya vyakula unavyokula. Kwa sababu katika kipindi hiki kunakuwa na vyakula vya kila aina, ndiyo ukawa unakula tu bila ya kuwa makini. Ulaji wa vyakula tofauti bila ya mpangilio na kiwango maalumu unaweza kukusababishia madhara kwenye mwili wako na kukusesha raha ya kufurahia sikukuu. Hivyo basi, kama inawezekana basi jaribu kuendana na utaratibu wako uliojiwekea wa kula. Usizidishe kwa sababu siku hii vyakula ni vingi.




Kuwa makini na kiasi cha pombe. Ndiyo ni sikukuu, hauna wajibu siku inayofuatia au mtondogoo. Lakini hii isiwe sababu ya kutokuwa makini na kiwango cha pombe unachokunywa. Unywaji wa pombe kuzidi kiwango unaweza kukusababishia mbali tu na uchovu kwenye mwili wako na kushindwa kufurahia matukio ya muhimu na familia yako bali pia hata madhara kwako na watu wanaokuzunguka. Jaribu kuwa mvumilivu kwa kipindi hiki kifupi, furahia kwa kunywa kiasi na familia pamoja na wapendwa wako. Kwa kuongezea, unywaji wa pombe kupitiliza unaweza kukusababishia ukaingia matatani na vyombo vya sheria, kwa sababu ni kipindi cha mapumziko haimaanishi kwamba sheria na taratibu za nchi zimelala.




Tumia pesa kwa makini. Kipindi hiki pia watu wengi hushuhudia wakitumia kiwango cha pesa bila ya kutarajia. Ni vema ukawa umetenga kiwango fulani cha fedha kwa ajili kutumika kwenye msimu huu wa sikukuu. Kama haukufanikiwa kutenga mapema bajeti ya kutumika kipindi hiki basi hakikisha fedha utakayoitumia haitaathiri matumizi yako ya baadaye. Unaweza kufanya hivyo kwa kubana matumizi kwani sio lazima kuwa na shamrashamra kubwa. Kwa sababu ni kipindi cha mwisho wa mwaka na tunafahamu namna maisha yetu watanzania yalivyo, mwaka mpya huja na majukumu kama vile kodi za nyumba, karo za shule, pango za sehemu za biashara, leseni au vibali vya vyombo vya moto nakadhalika.



Usijibane sana, furahia! Inawezekana mipango haijakaa sawa kwenye msimu huu wa sikukuu hivyo kukunyima fursa ya kufurahia vilivyo. Kumbuka, kipindi hiki hutokea mara moja tu kwa mwaka na hautakiwi kujuta sana kwamba kwa nini haukufanikiwa. Ni mafanikio kuwa mzima mpaka kufanikiwa kuuona msimu huu wa sikukuu kwani wengine hawajafanikiwa. Jumia Travel inaamini kwamba kwa kuumaliza mwaka ukiwa na matumaini kutakupa fursa ya kujipanga vema zaidi na mwaka ujao.

JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAMPOKEA KWA KISHINDO MWENYEKITI WA TAIFA WA JUMUIYA HIYO DK. EDMUND MNDOLWA

 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi wa wana CCM waliofurika katika ukumbi wa Tawi la CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambao walifika kumlaki katika mapokezi yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam, jana.
 Gari la Dk. Mndolwa likiwasili lango Kuu la Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mapokezi hayo
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar  Abdallah Haj Haidar akimpokea Dk Mndolwa kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisilindikizwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba kwenda kusaini vitabu wa wageni na kuzungumza na uongozi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Dk. Mndolwa akisaini kitabu wa wageni katika Ofisi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alipowasili. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa huo, Frank Kalokola Kamngisha
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Abdallah Haj Haidar akisaini kitabu cha wageni, huku Dk. Mndolwa akiendelea kufanya hivyo pia.
 Abdallah Haj Haidar akisalimia
 Mama Patricia Rukia Mndolwa akisalimia
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Bara Burhan Rutta akisalimia
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Kusilawe akisalimia
 Kalokola akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, amkaribishe Dk. Mndolwa kuzungumza na Uongozi
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alizungumza kabla ya kumkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza
 Kate Kamba akimkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza na uongozi
 Dk. Mndolwa akizungumza na Uongozi
 Mwafongo na Katibu wa CCM Kata ya Ilala Habib Nasser ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, wakitoka nje kumsubiri Dk Mndolwa kutoka nje tayari kwa safari ya kwenye kwenye eneo kuu la mapokezi ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala
 Gari lilobeba Dk Mndolwa likiwasili kwenye Viwanja vya Ofisi ya Tawi la CCM Mwinjuma 
 Kijana wa CCM akimvisha Skafu Dk. Mndolwa baada ya kuwasili CCM Mwinjuma
 Dk. Mndolwa akipokea kwa ukakamavu saluti ya kijana wa CCM baada ya kuvishwa skafu
 Dk Mndolwa akiongozana na baadhi ya viongozi kwenda eneo la tukio
 Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya wana CCM wakati akienda ukumbini
 Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya viongozi wakati akienda ukumbini  
 TOT wakitumbuiza kumlaki ukumbini Dk. Mndolwa
 Dk. Mndolwa akienda meza kuu
 Dk. Mndolwa na Makamu wake- zanzibar wakiwa tayari meza kuu
 Viongozi wa meza kuu wakiungana na Dk Mndolwa kushangilia baada ya kuwasili eneo hilo
 Mmoja wa viongozi katika Baraza la Wazee wa jumuiya ya Wazazi Mzee Mkali akisalimia
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mwafongo akifanya utambulisho wa viongozi ndazi ya mkoa
 Viongozi ndazi ya mkoa wakisalimia baada ya kutambulishwa 
 Baadhi ya viongozi waliohudhuria mapokezi hayo wakiwa ukumbini
 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya wazazi Tanzania Ndugu Rutta akitambulisha viongozi ngazi ya taifa  
 Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi tanzania Seif Shaban Mohammed akifafanua maana na umuhimu wa neno 'Mapinduzi'  baada ya kutambulishwa  
 Ndugu Mwafongo akiendeleza ratiba
 Mwenyekiti wa CCM Temeke ndugu Almish akizungumza baada ya kutambulishwa 
 Ndugu Kalokola akizungumza kumtambulisha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Haj
 Kakamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Hajj akizungumza
 Shabiki wa CCM akimuombea maisha marefu na uongozi bora Dk. Mndolwa tukio ambalo lilikuwa la ghafla
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba akizungumza kabla ya kumkaribisha Dk. Mndolwa kuzungumza na hadhara 
 Omar Kimbau aliyewahi kuhamia CUF akitangaza kurudi CCM mbele ya Dk. Mndolwa
 Dk. Mndolwa akimpongeza Kimbau kwa kuzinduka na kurejea CCM
 Dk. Mndolwa akihutubia kweye mapokezi hayo

CHAKULA CHA JIONI SERENA HOTEL
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mwafongo akiwakaribisha Dk. Mndolwa na Mkewe walipowasili hoteli ya Serena kwa ajili ya chakula cha jioni
 Mwafongo akiwaongoza kwenda eneo la kuketi 
 Dk. Mndolwa akimsalimia Mwenyekiti  wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Kalokola
 Dk Mndolwa akimsalimia  Ndugu Kizigha
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania- Zanzibar Ndugu Hajj akimsalimia Mama Mndolwa
 Dk Mndolwa akizungumza jambo wakati wakisubiri muda wa chakula
 Ndugu Mwafongo akiwa amesimama kuwakaribisha rasmi waalikwa wote 
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Kalokola akizungumza maneno ya ukaribisho kwenye chakula hicho cha jioni
 Dk Mndolwa akiongozana na Ndugu Hajj kuchukua chakula
 Angela Kizigha akimsaidia Dk. Mndolwa kubeba chakula
 Mweneyekiti wa CCM Kinondoni akichukua chakula
 Viongozi mbalimbali wakichukua chakula
 Ndugu Mwafongo akiongoka na chakula chake kwenda sehemu ya kuketi
 Ndugu Hajj akichukua chakula 
 Baadhi ya waandaaji wa nyama choma hotei ya Serena
 Waalikwa wakila chakula 
 Dk Mndolwa na mkewe wakipata chakula na waalikwa wengine  

 Dk Mndolwa akitoa nasaha zake baada ya chakula   
Kisha Dk. Mndolwa akapozi kwa picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali aliopata nao chakula hicho cha jioni. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More