Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza utekelezaji wa zoezi la kubomoa kuta za nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya Mto Msuka katika eneo la Kilimahewa, kwa ajili ya kupanua mto huo ili kuondoa athari za mafuriko zinazojitokeza wakati wa mvua za masika. Wananchi wametakiwa kutojenga maeneo yasiyo rasmi.
Na BMG
Zoezi ka ubomoaji likiendelewa ambapo limesimamiwa na mgambo wa halmashauri hiyo ya Manispaa ya Ilemela
Mto huu unapaswa kupanuliwa zaidi na kujengewa kuta maana wakati wa mafuriko huwa unapitisha maji mengi yanayosababisha mafuriko kwa wakazi wa eneo hili la Kilimahewa.
Miongoni mwa kuta zilizoingia eneo la hifadhi ya mto Msuka baada ya kubobolewa
Miongoni mwa kuta zilizoingia eneo la hifadhi ya mto Msuka baada ya kubobolewa
Na George Binagi-GB Pazzo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza utekelezaji wa zoezi la kubomoa kuta za nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya Mto Msuka katika eneo la Kilimahewa, kwa ajili ya kupanua mto huo ili kuondoa athari za mafuriko zinazojitokeza wakati wa mvua za masika.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza utekelezaji wa zoezi la kubomoa kuta za nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya Mto Msuka katika eneo la Kilimahewa, kwa ajili ya kupanua mto huo ili kuondoa athari za mafuriko zinazojitokeza wakati wa mvua za masika.
Mhandisi wa
Manispaa hiyo, Jacob Mwakyambiki, amesema zoezi hilo limefanyika baada ya tahadhari
kutolewa kwa wakazi wa eneo hilo kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita na kwamba
mpango uliopo ni kujenga mtaro mkubwa katika mto huo ili kusaidia maji yake
kutosababisha mafuriko wakati wa mvua za masika.
Amesema
tayari mkandarasi ameanza kazi hiyo na kwamba ujenzi wa mto huo
utakapokamilika, utasaidia maji yake kutiririka moja kwa moja hadi ziwa
Victoria badala ya kumwaga maji kwenye makazi ya watu kama ilivyokuwa hapo awali
na kusababisha athari za kimafuriko.
Hata hivyo baadhi
ya wakazi wanaoishi katika eneo linalopitiwa na mto Msuka wamesema zoezi hilo
limefanyika wakati ambao bado hawajui hatima yao kwani wakati wanajenga makazi
yao katika eneo hilo walipata vibali vyote ikiwemo hati miliki za viwanja vyao
ambapo wamependekeza kulipwa fidia licha ya Manispaa ya Ilemela
kuwatahadharisha kwamba hakuna fidia itakayotolewa kwa waliojenga katika
hifadhi ya mto.
Licha ya
malalamiko hayo, baadhi ya wakazi wa Kata ya Ibungilo wanaoishi katika maeneo
jirani na mto Msuka wamepongeza zoezi la upanuzi wa mto huo kwani wamekuwa
wakipata athari kubwa ikiwemo mali zao kusombwa na maji wakati wa mvua za
masika kutokana na makazi ya wananchi yaliyojengwa kwenye karibu na mto huo.
Katika misimu
kadhaa ya mvua za masika, athari mbalimbali ikiwemo vifo vya watu na mifugo kutokana
na mafuriko ya mto Msuka, zimekuwa zikitokea katika eneo la Kilimahewa kutokana
na wananchi kujenga makazi yao hadi kwenye hifadhi ya mto huo hivyo upanuzi na
ujenzi wake unaelezwa kuwa mwarobaini wa kadhia hiyo.
0 comments:
Post a Comment