Tuesday, October 11, 2016

VIDEO: STAA WA NIGERIA, YCEE AUNGANA NA DJ MAPHORISA WA AFRIKA KUSINI KWENYE REMIX YA OMO ALHAJI

Msanii wa Hip-hop wa Nigeria, Ycee ameungana na mtayarishaji wa muziki na muimbaji wa Afrika Kusini, DJ Maphorisa kwenye remix ya wimbo wake unaofanya vizuri barani, ‘Omo Alhaji’.

Ikifanyika jijini Johannesburg, na kuongozwa na La Dupont Productions, remix ya wimbo huo inahusisha rap iliyoshiba na inayohitaji usikivu.

DJ Maphorisa amechanganya ladha ya kipekee ya Kusini kwenye mrindimo unaoungana vyema na mtindo wa Ycee na kuzalisha wimbo utakaofanya vizuri kwenye klabu, mtaani na hata kwenye redio. Remix hii ya Omo Alhaji, haina shaka itateka tena mawimbi ya redio na TV barani Afrika.

Ycee anasema, “Limekuwa jambo kubwa kufanya remix hii, kama msanii ninafurahi kujaribu muziki tofauti. Ulikuwa uzoefu mkubwa na wa kufurahia kufanya kazi na DJ Maphorisa. Ninaamini mashabiki watafurahia remix hii.”

KUHUSU YCEE

Akizaliwa kwa jina la Alejo Martin Oludemilade, tarehe 29, January 1993, Ycee ni msanii wa hip hop wa Nigeria na mshindi wa tuzo.  Amesainishwa kwenye lebo ya muziki ya TINNY ENTERTAINMENT. Alianza rasmi muziki Disemba 2012 kwa kuachia wimbo 'Smile on Me' uliotayarishwa na Jay Sleek, na zingine kama 'Pass Me' na 'Amen' akimshirikisha Mbryo.

Alikuja kujipatia umaarufu zaidi July 2015 baada ya kuachia wimbo 'Jagaban.' Jagaban ukaja kuwa miongoni mwa nyimbo kubwa zaidi kwa mwaka 2015/16 na kuja kuwa na remix nzito aliyomshirikisha staa wa YBNL, Olamide na video yake ikiongozwa na Director Q.

Wimbo huo ulimweka sehemu nzuri Ycee kama kinara wa hip hop ya kizazi kipya nchini Nigeria na hatimaye kumpa tuzo ya “Rookie Of The Year” kwenye tuzo za Headies, mwaka 2015.

Kutoka kwa wimbo ‘Omo Alhaji’, Disemba 2015, kulimpandisha zaidi Ycee kama mmoja wa wasanii wakali kabisa wa hip hop nchini Nigeria. Alikuja kuachia video ya wimbo huo iliyoongozwa na Director Q iliyofanyika Uingereza. Wimbo huo pamoja na video yake viligeuka wimbo wa taifa kwenye chati za redio za TV za Nigeria, kwenye klabu na hata mtaani huku ukiipa umaarufu sentesi: 'Who's your Daddy?

EP yake ya kwanza iliyopewa jina The First Wave itatoka Oktoba, 2016.

KUTAZAMA VIDEO HIYO FUATA LINK HIYO CHINI:

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More