Wednesday, October 5, 2016

LUKUVI AWAPA MADIWANI WA CCM PAWATILA 15 KWA AJILI YA MAENDELEO YAO ZENYE THAMANI YA TSH MILIONI 105.



 Diwani wa kata ya Kising'a Ritta Mlagara akiwa akijiandaa kuendesha moja kati ya pawatila 15 zenye  thamani ya  Tsh milioni 105   zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa  Wiliam Lukuvi kwa  ajili ya madiwani wa tatu  kushoto ni katibu wa mbunge Lukuvi.

Diwani wa kata ya Malenga makali  Flanzisca Kalinga akiwa akijiandaa kuendesha moja kati ya pawatila 15 zenye  thamani ya  Tsh milioni 105   zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa  Wiliam Lukuvi kwa  ajili ya madiwani wa tatu  kushoto ni katibu wa mbunge Lukuvi , Thom Malenga ambae  alikabidhi kwa niaba ya mbunge  Lukuvi akiwa na baadhi ya madiwani  hao.
 
na fredy mgunda,Iringa
 
MBUNGE wa jimbo la Isman ambaye pia ni waziri wa ardhi mh Williamu Lukuvi ametoa pawatila kumi na tano (15) kwa madiwani kumi na tano (15) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye jimbo la ismani lengo likiwa ni kuwasaidia madiwani wakati wa utekelezaji wa shughuri za kimaendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa mbunge Thom Malenga alisema kuwa mbunge wa jimbo la Ismani Williamu Lukuvi amewapa madiwani pawatila ili kuchochea maendeleo katika kata zao na kuboresha maendeleo ya kata 
 
“Hizi pawati nimeambiwa niwape kwa lengo la kupunguza adha ya kipato kwa madiwani husika na kuwapunzia mzingo wananchi wa kukodi pawatila kwa gharama kubwa kwa kuwa anauhakika nie madiwani ni wapenda maendeleo na mnawatumikia wananchi hivyo anajua pawatila hizi zitatumika kuleta maendeleo”alisema Malenga

Aidha Malenga amewataka madiwani kuwatumika wananchi ipasavyo ili kumuunga mkono mbunge kwa kukuza uchumi wa kila kata na kulifanya jimbo la ismani kuwa na maendeleo ya haraka kwa kuwa madiwani ndio wapo karibu na wananchi kuriko mbunge.

“Pawatila hizi ni mali ya madiwani mali ya madiwani na madiwani ndio watajua jinsi gani ya kuzitumia mbunge amwapa wao ili watafute njia za kujikwamua kiuchumi kwa kuwa kipato cha diwani ni kidogo hakikidhi mahitaji ya wananchi hivyo kupitia pawatila hizo nafikiri zitawapunguzia mzigo kiasi” alisema Malenga

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Iringa vijijini Khalfani Hassani alisema madiwani ndio wa kwanza kukutana na changamoto kabla ya mbuge hivyo kupewa kwa pawatila hizo zitawasaidia kujenga uchumi wa madiwani na kuwasaidia kutatua changamoto za wananchi.

“Mwananchi akiwa na kesi,matatizo au huduma yoyote ile wa kwanza kumuona ni diwani hivyo sisi ni vinara wa kupewa kero na changamoto za wananchi na wanaona madiwani ndio kimbilio lao”alisema Hassan

Lakini Hassani alimshukuru  mbunge wa jimbo la Ismani Mh William Lukuvi  kwa kuwajali madiwani kwa kuwa anajua kipato chao na kumuomba aendelee kuwa na moyo wa kuwasaidia wananchi na madiwani wa jimbo la Ismani

Nao madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Ismani wameshukuru mbuge kwa kuwakumbuka kwa kuwa wao ndio walezi wa Chama cha Mapinduzi katika kata hivyo kupewa kwao pawatila zitawasiaidia kuwakomboa wananchi kimaendeleo hasa ukizingatia mbunge wetu ni mpenda maendeleo

Mh Lukuvi ni mtu mpenda maendeleo huwa achagui nani ni nani yeye anachojali ni kulifanya jimbo la Ismani kuwa na maendeleo hivyo pawatila hizi zitatoa ajira kwa wananchi wengine.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More