Wednesday, October 5, 2016

DC MTATURU AWAAGIZA VIONGOZI WA VIJIJI VYOTE KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI NDANI YA WIKI MOJA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kata ya Ntuntu wakati kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake Wilayani Ikungi
Wananchi wa Kata ya Ntuntu wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwahutubia wananchi wa kata ya Ntuntu

Kaimu katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Dandala Mzunguor akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turukaili naye amkaribishe Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwahutubia wananchi wa kata ya Ntuntu
Wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya akitoa maagizo ya mpango wa maendeleo ya Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza maelekezo yaliyopelekea kukwama kwa ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Ntuntu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ntuntu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Taru kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza sababu zilizochangia kukwama kwa ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Lighwa
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ulipoishia ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Lighwa
Wakazi wa Kijiji cha Mwisi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizitaja siasa taka kuwa ndizo zilizokwamisha kupatikana kwa maendeleo katika Wilaya ya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake wa kazi katika kata ya Lihgwa

Na Mathias Canal, Singida

Viongozi wa Vijiji vyote Wilayani Ikungi Mkoani Singida wameagizwa kusoma mapato na matumizi ili kuwarahisishia wananchi kufahu jinsi fedha zao zinavyotumika katika ukweli na uwazi na kutoa fursa kwa wananchi kupata nafasi ya kuhoji ili kujiridhisha pale wanapokuwa na mashaka.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa mikutano yake ya kazi katika Wilaya hiyo iliyoanza jana kwa kutembelea kila kata kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo la kujua maeneo ya utendaji na kuwakumbusha wenyeviti na watendaji wa Vijiji na Kata kutambua majukumu yao na kuyapatia majibu sawia na kubadili changamoto kuwa fursa.

Dc Mtaturu ameagiza kufanyanyika uchunguzi ili kubaini kama kuna watendaji wamehamishwa kazi na wanatuhumiwa kuhujumu mapato ya serikali na michango ya wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo kurudishwa haraka iwezekanavyo ili kutoa majibu ya tuhuma hizo na kuchukuliwa hatua endapo watabainika kujihusisha na kadhia hiyo.

Katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Ntuntu na Kata ya Lighwa Dc Mtaturu amesema kuwa wazazi wote ambao watoto wao wanajihusisha na utoro watachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kubaini chanzo cha utoro huo kama unasababishwa na wazazi wenyewe ama wanafunzi kujihusisha na makundi ovu ikiwemo kufanywa vijakazi katika maeneo ya mijini.

Dc Mtaturu amewakemea wanasiasa ambao wamezuia wananchi kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu, Ujenzi wa Shule na maabara huku wakiwaahidi kuwa serikali itajenga kila kitu na kuongeza kuwa serikali kuu haiwezi kufanya kila jambo badala yake wananchi kwa umoja wao wanapaswa kushiriki katika uchangiaji wa huduma za kijamii.

Mkuu huyo wa Wilaya amewaagiza watumishi wote wa serikali ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata kufanya kazi kwa haki, Usawa na uwazi na kiwashirikisha wananchi katika kila jambo linalohusu vipaombele vya maeneo yao.

Pia amevitaka vijiji 39 ambavyo havijapimwa kupimwa na kurahisisha upangaji wa matumizi bora ya ardhi ili kuepuka migogoro mbalimbali ya ardhi ambayo imekuwa ni changamoto kubwa katika maeneo mengi nchini.

Akizungumzia kadhia ya maji safi na salama kati kata hizo mbili Dc Mtaturu alisema kuwa serikali inatambua kuwa hakuna maji safi na salama hivyo imejipanga kuzikabili changamoto hizo katika kipindi cha muda mfupi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wamempongeza mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kufanya ziara katika Kata hizo kwani wana miaka zaidi ya 10 hawajawahi kutembelewa na Mkuu wa Wilaya wala Mkurugenzi.

Wananchi hao wametoa mifano ya Wakuu wa Wilaya waliowahi kufika wakati huo Wilaya ikiwa haijagawanywa kitoka Wilaya ya Singida kuwa ni pamoja na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Hawa Ngurume (Marehemu) sawia na Mhe Abas Kandoro ambaye hivi karibuni alistaafu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ameivunja kamati ya maji katika Kijiji cha Ntewa B iliyopewa mamlaka ya kuendeleza upatikanaji wa huduma ya maji na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka kufatilia ili kujua chanzo cha kukosekana kwa maji katika kijiji hicho ilihali miundombinu ya kupatikana maji kijijini hapo imekamilika vyema.

Dc Mtaturu alisema kuwa Demokrasia inayohubiriwa na baadhi ya wanasiasa nchini inapaswa kuwa Demokrasia ya kweli kwa kuwa na nidhamu na mamlaka pia kutoitukana serikali na kupinga kila jambo linalofanywa na serikali.

Sambamba na hayo pia Dc Mtaturu amemuagiza Mkuu wa Polisi Wiliya ya Ikungi kuwakamata haraka iwezekanavyo wazazi wa watoto watatu ambao ni wanafunzi wa katika Shule ya Sekondari Lighwa waliopatiwa mimba ili kutoa taarifa ya watu waliowapa ujauzito huo na kuchukuliwa hatua.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More