Monday, April 30, 2018

UDHAMINI WA PUMA NDANI YA IFA UTASAIDIA KUINUA VIPAJI VYA SOKA MKOANI IRINGA

Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake akielezea mipango yake ya kuinua soka la vijana mkoani Iringa na Nje ya mkoa wa Iringa.
 Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa akionyesha jinsi ambavyo nembo ya puma iatapoa kwenye jezi za kituo hicho
Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa akiwa na kocha mkuu wa kituo hicho mwalimu Saleh molelikatika ofisi za IFA mkoani Iringa

 NA FREDY MGUNDA, IRINGA

KITUO cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA) kimefanikiwa kuingia mkataba wa udhamini wa wa jezi na vifaa vya michezo kwa muda wa miaka miwili na kampuni ya mafuta ya Puma Energy.

Akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake, Mkurugenzi wa kituo cha kuendeleza soka cha Iringa (IFA)  Ally Msigwa, alisema kuwa kituo hicho kimepata udhamini wa vifaa vya michezo kutoka kampuni hiyo na udhamini huo utakijita kwenye safari zote za timu inapoelekea katika michezo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Iringa.

Msigwa alisema kuwa kituo hicho kimekuwa kimbilio la vijana wengi wenye vipaji na kimefanikiwa  kupata ufadhili wa kudumu kutoka kwa kampuni ya Alishati Investment ambayo itafadhili mahitaji mbalimbali katika kituo hicho.

 Alisema kuwa kituo hicho ambacho kimekuwa kikubwa kwa sasa kina mahitaji mengi ambayo yanahitajika katika kujikimu na kwa sasa kinatarajia kuwa na uwanja wake maeneo ya Ifunda kata ya Lumuli wilaya ya Iringa ambapo ujenzi wake uko katika mchakato kuanza baada ya kila kitu kukamilika.

Msigwa ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Yanga alisema kuwa katika ujenzi wa uwanja wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa utakaochukua watu zidi 5000 hivyo kuwa moja ya viwanja bora kabisa kwa upande wa Nyanda za Juu Kusini.

Msigwa Aliongeza kuwa uongozi wa kituo hicho umeeamua kuunda bodi ya wakurugenzi ambao watasaidiana katika kufanikisha ndoto mbalimbali za kukuza soka la vijana nchini Tanzania ambapo Dk. Mshindo Msola ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wa kituo hicho na kocha Salehe Molel kuwa kocha wa vijana chini ya miaka 15 hadi 17.

Aidha Msigwa alisema kuwa IFA imefanikiwa kuteua wajumbe wa bodi ambapo itaongozwa na Augustino Mahiga Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu ofisi ya Msajili Hazina Wizara ya Fedha Gerald Mwanilwa.

Wengine watakaounda wajumbe wa bodi ni Ezra Chomete mtanzania mwenye makazi Marekani, Abdul Mapembe ambaye ni Meneja TRA Ilala, Mhindisi Patrick Mbendule na Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa, Cyprian Kuyava.

Naye kocha mkuu wa kituo hicho mwalimu Saleh moleli alisema kuwa amepata sehemu sahihi ya kuujenga upya mpira wa mkoa wa Iringa kwa kuwa hapo awali alikuwa kocha anayefundisha timu za wakubwa tu.

“Kupata nafasi hii kwangu kama kocha mzoefu nimefarijika sana,nitakikisha naitumia vilivyo kwa kuahikisha mpira wa vijana unakuwa na kuzailisha kizazi cha soka hapa mkoani Iringa na duniani kwa ujumla” alisema Moleli

Moleli alisema kuwa watahakikisha vijana wote watakokuwa kwenye kituo hicho watapata elimu bila wasisi wowote ule.

“Wazazi wengi wamekuwa wakiwazuia watoto wao kukuza vipaji vyao kwa kuhofia kutoendelea na masomo yao lakini kwenye mpingo yetu kutakuwa na shule ambayo itawasaidia wanafunzi kusoma wakiwa hapo kituoni” alisema Moleli

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric Shitindi katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya MFuko kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani tarehe 28 Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala ya usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka.

Maadhimisho haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29.

Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa ushindi walioupata na kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja ya malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na kuendeleza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi. Mshomba ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa baada ya kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala ya afya ya usalama mahala pa kazi. 

Aidha, akikabidhi tunzo hiyo kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi ameupongeza Mfuko kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika nyanja tofauti tofauti pamoja na kwamba hauna miaka mingi sana toka uanzishwe. “Tunajivunia sana kuona ya kwamba Mfuko umeweza kulipa fidia stahiki kwa wakati, kitu ambacho kilikuwa changamoto hapo awali” Aidha, pongezi zangu ziwafikie kwa kuanzisha mifumo inayoboresha huduma kwa waajili na waajiliwa wote ikiwemo mifumo ya ki- electroniki inayowazezesha waajili kujisajili, kulipia michango na kufuatilia michango yao. 


Mfuko umehitimisha maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi katika Mkoa wa Iringa na unajiandaaa na semina ya wadau itakayofanyika tarehe 30 Aprili na hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Tarehe 01 May 2018. 
Katikati Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya kupokea tunzo na cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe pamoja na Bw. Shitindi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
Bw. Ibrahim Mussa Afisa Madai Mwandamizi – WCF akimhudumia mteja aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya Kichangani Iringa.
Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati), akiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Fulgence Sebera, akizungumza 

IRINGA IJIPANGE SAWASAWA KUWA KITOVU CHA UTALII

 Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi akisalimiana na Rais wa jamhuri ya muungano Dr John pombe Magufuli alipofika Iringa kwa ajili ya ziara yake
Baada ya uzinduzi wa barabara ya Migori-Iringa ambayo ni sehemu ya Barabara ya Dodoma hadi Iringa, Mhe Rais alizungumzia nia yake ya kuhakikisha Utalii unanyanyuka Southern Circuit ambapo Mkoa wa Iringa ndio kitovu.

Kati ya mambo ambayo Serikali imedhamiria kuyafanya ni pamoja na kuufanya uwanja wa ndege wa Nduli kuwa mkubwa na wa kisasa, na kujenga barabara ya Iringa hadi geti la Ruaha National Park.

Hatua hizi ni wazi kuwa zitaifungua Iringa kifursa mbalimbali. Ni muhimu kuanza kujiweka sawa kuanzia mafunzo katika masuala ya Utalii.

Ni wajibu wetu kuwa-encourage vijana wetu kujihusisha na masuala ya Utalii ikiwa ni pamoja na kujifunza lugha za nje kama Kispaniola, kifaransa, kijerumani nk

Ukienda Zanzibar kwa mfano, kuna vijana wengi sana wamejikita katika shughuli za utalii kama kuongoza watalii nk. Vijana hao wamefanikiwa kwa sababu waliona hiyo fursa na kuichangamkia japo kwa kupata basic courses za masuala ya Utalii.

Kwa mujibu wa taarifa za Serikali, mpaka kufikia 2017, sekta ya utalii ndio ilikuwa inaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni, kiasi cha zaidi ya 17%. Kwa hiyo kuna fursa katika Utalii. Iringa na maeneo/mikoa ya jirani tujiandae katika kuchangamkia fursa hii inayokuja mbele yetu.

*Cosato Chumi*
*Mafinga Mjini*
*30 April, 2018*

Saturday, April 28, 2018

TALGWU WAWATAKA WANACHAMA WAKE KUJIANDAA KUNUNUA HISA HAPO BAADAE ZA MICROFINANCE PLS


Baadhi ya viongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU)  wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda loa katika viwanja vya kichangani manispaa ya Iringa na kuwataka wanachama kununua hisa kwa wingiili nao wawe wamiliki wa taasisi na kufanikiwa kuwa na maamuzi ya chama hicho kwa maendeleo ya mwanachama 
Baadhi ya wananchi na viongozi walipokuwa wakibadilishana mawazo kwenye banda la TALGWU
 Baadhi ya viongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU)  wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda loa katika viwanja vya kichangani manispaa ya Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini Tanzania (TALGWU) wametakiwa kujiandaa kununua hisa hapo baadae za TALGWU microfinance PLC ili nao wawe wamiliki wa taasisi na kufanikiwa kuwa na maamuzi ya chama hicho kwa maendeleo ya mwanachama.

Akizungumza hii leo kwenye banda TALGWU katika maonyesho ya kuelekea mei mosi,mkurugenzi mtendaji wa microfinance PLC Jackson Ngalama alisema kuwa mwananchama wa TALGWUakinunua hisa atakuwa atapata gawio la kila mwaka kutoka na faida ambayo itakuwa imetengenezwa kwa kipindi hicho kutoka katika kampuni ya TALGWU microfinance PLC.


Ngalama alisema kuwa wananchama aliye na hisi katika kampuni ya TALGWU microfinance PLC ataruhusiwa kukopa kwa riba nafuu ambayo itamuongezea kufanya maendeleo binafsi tofauti naakienda kukopa sehemu nyingine.

“Sisi tunamlinda na kumheshimu mwanachama wetu hivyo hata akikopa atapewa elimu ya jinsi ya kutumia mkopo wake kwa faida maana tumeona watu wengi wakikopa huwa inakuwa vigumu kujua amekopa kwa ajili ya nini hivyo tumeamua kuta elimu kwanza ili kumfanya awe mwanachama mwenye mafanikio makubwa” alisema Ngalama

Ngalama alisema kwa sasa hisa zinatarajiwa kuuzwa kwa shilingi elfumoja na mwananchama anatakiwa kuanza kununua hisa za shilingi elfu hamsini na kuendelea ili kuongeza thamani ya kampuni hiyo na mteja wake anayetumtumia na kupata huduma hiyo.

“hisa zetu zinatarajiwa kuanza kuuzwa hivyo naomba nitoe rai kwa wanachama wetu wote waanze kujiandaa kununua hisa ambazo zitauzwa kwa gharama nafuu ya shilingi elfu moja tu.

Wakati huo huo afisa habari wa TALGWU Shani Kibwasali alisema kuwa TALGWU imekuwa ikiboresha na kuendeleza hali nzuri za wanachama wakiwa kazini,kuondoa tofauti zinazojitokezakati ya mwajiri na mwajiriwa  wakiwa kazini na kuwarudisha kuwa wamoja na kuendelea kufanya kazi na kuleta maendeleo.

“Sisi kazi yetu kuhakikisha mwanachama wetu anapata haki zakezote za msingi hivyo tunaposikia kunamgogoro mahali inatupaswa kwenda kuutatua na kuhakikisha kila mtu anapata haki yake” alisema Kibwasali

Kibwasali alisema kuwa TALGWU imefanikiwa kuishawishi serikali kuwarudisha wafanyakazi waliokuwa wamefukuzwa kazi mwaka 2017 kwa kuwa walikuwa wanaelimu ya kidato cha nne,mwaka 2016 hadi 2017 walishinda jumla ya kesi 37 zilizokuwa zinawakabili wanachama wakena pia walisimamia kutolewa kwa muundo mpya wa mwaka 2013/2014 wa watendaji wa kata,mitaa na vijiji.

Aidha Kibwasali alisema kuwa TALGWU imeweka mikakati ya mwaka 2016 hadi 2021 kwa kuhakikisha inawaunganisha wanachama wote kuwa kitu kimoja,kujenga na kuhimiza wanachama kuwa wawajibikaji wakiwa makazini,kuimalisha chama kiuchumi ili kutoa huduma inastahili kwa wanachama,kufanya ziara ya mara kwa mara ili kujua kero na changamoto mbalimbali zinawazowakabili wanachama wake

Tuesday, April 24, 2018

MICHEZO YA MEI MOSI MKOANI IRINGA YASHIKA KASI,HUKU TRA IKIPATA USHINDI KWA TAABU SANA

 Wachezaji wawili waliozavalia jezi za rangi ya njano na nyeusi ni wachezaji wa timu ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wakijaribu kumnyang'anya mpira mcheza wa timu ya Ukaguzi katika mchezo uliochezwa hii leo jioni katika dimba la kumbukumbu ya Samaro
 Mchezaji hatari katika mchezo wa leo wa timu ya TRA mwenye jenzi ya njano na nyeusi akielekea kutoa pasi ya goli huku beki wa timu ya Ukaguzi akiishia kumuangalia tu kwa macho
 TRA wakipata goli lao la kwanza na la ushindi leo katika uwanja wa Samora uliopo manispaa ya Iringa
 Golikipa wa timu ya ukaguzi akiwa hana la kufanya zaidi ya kuutolea macho mpira ukiingia nyavuni
 Wachezaji wa timu ya TRA wakishangilia mara baada ya kupa goli ambalo pia limekuwa goli lao la ushindi katika mchezo wa leo
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na Kocha wa timu ya Lipuli wanapaluengo Suleman Matola walikuwepo kwenye michezo huo uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora manispaa ya Iringa

TAKUKURU MKOA WA IRINGA WAMECHUNGUZA MIRADI NANE NA MIWILI IMEKUTWA NA UBADHIRIFU


 Kamanda  wa  taasisi ya  kuzuaia  na kupambana na  rushwa  (TAKUKURU)  mkoa  wa  Iringa  Aidan  Ndomba  akizungumza na  waandishi wa habari ofisini  kwake  kuelezea juu ya kilichotokea katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2017.


 Baadhi ya viongozi wa takukuru na waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda  wa  taasisi ya  kuzuaia  na kupambana na  rushwa  (TAKUKURU)  mkoa  wa  Iringa  Aidan  Ndomba 

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda  wa  taasisi ya  kuzuaia  na kupambana na  rushwa  (TAKUKURU)  mkoa  wa  Iringa  Aidan  Ndomba 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Iringa imepokea jumla ya malalamiko 91 ya rushwa kutoka kwa wananchi katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2017.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa Aidan Ndomba alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU Mkoani hapa katika kipindi cha mwezi Julai hadi disemba 2017 na kuongeza kuwa katika sekta ya TAMISEMI kumekuwa na malalamiko 18.

Ndomba  alisema kuwa taasisi imechunguza  miradi  nane ya  sekta ya elimu ,maji na barabara  yenye  thamani  ya  takribani  bilioni 2.5 katika  wilaya ya Iringa , Mufindi na  Kilolo baada ya  kuwepo kwa dalili  ya matumizi mabaya ya  fedha  za  za  miradi hiyo .


alisema  ndani ya  kipindi  hicho  ofisi yake  ilifuatilia  na  kufanya  ukagzi  wa fedha  za  miradi  nane  ya maendeleo  katika  sekta za elimu ,maji na barabara  yenye  thamani ya  takribani shilingi bilioni  2,588,000,000 na kubaini mapungufu  katika  miradi yenye thamani ya  shilingi milioni 818 ambapo  uchunguzi  wa matumizi ya  fedha  za  miradoi umeanzishwa.

Alisema  kuwa  miradi  miwili  ilifuatiliwa  na kukaguliwa  katika  Halmashauri ya  Iringa na  ina  thamani ya   shilingi  1,164,614,899 iliyopo  katika kijiji  cha Mfyome   kata ya  Kiwere   na  Malizanga  kata ya  Mlowa   huku miradi mitatu  iliyofuatiliwa   na  kukaguliwa ipo  katika  Halmashauri ya  Kilolo ina  thamani ya shilingi 908,138,034 kuwa  miradi hii ipo  kijiji  cha Ng'uruhe , Irindi, na Ipalamwa .


 Ndomba alisema kwa upande wa barabara  miradi miwili ilifuatiliwa  na kukaguliwa  katika  wilaya ya  Mufindi  na ina thamani ya  shilingi 407,343,774 na kuwa miradi hiyo ni pamoja na barabara  za Maduma  -Tambalang'ombe  na Maguhani - Udumka .

wakati kwa  wilaya ya  Kilolo kuna  mradi  mmoja  wa barabara   wenye  thamani ya  shilingi  107,343,774 umefuatiliwa na  kukaguliwa  mradi huu ni ule wa Ilula  ujulikanao kama  KItelewasi - Ilambo .
Ndomba  alisema  kuwa  baadhi ya  sekta  zilizolalamikiwa  ni  pamoja na  TAMISEMI ( Halmashauri  na  serikali  za  mitaa,vijiji  )   kwa  kuwa na malalamiko 18  , jeshi la  polisi  malalamiko  12 na  mabaraza  ya  ardhi malalamiko 8.

Aidha  Ndomba alisema  mashauri  mawili  yalikamilika  kwa  kutolewa  hukumu  katika shauri  namba  CC 03/2017 kati ya  Jamhuri na  Upendo Mponzi  (VEO- Ilula)  na  mwenzake Tulinutwa  Alphonce  Mlangwa  ambae  ni  diwani wa  kata ya  Kipaduka wote  wakiwa ni  watumishi  wa   umma  hakimu wa  mkoa  wa Iringa John Mpitanjia  aliwatia  hatiani wote  na  kuhukumiwa  jela miezi 6 ama  kulipa faini ya  shilingi 300,000 kila  mmoja .

Pia  alisema katika  shauri  la  pili  namba CC.39/2016 mshtakiwa  Selemani Futani  ambae ni mfamasia  msaidizi  wa Halmashauri ya  Mufindi aliachiwa   huru  na mahakama  ya  wilaya ya  Mufindi  hata  hivyo upande  wa Jamhuri  (Takukuru)  wamekata  rufaa mahakama kuu .

Kamanda  Ndomba  alisema kwa  kipindi  hicho  Takukuru  mkoa  wa Iringa imefanikiwa  kuokoa  kiasi cha shilingi 100,000 baada ya  kubaini  kuwa  kiasi hicho  cha fedha  zilikuwa  zilipwe mahakamani  kama  faini zilitumiwa na mtumishi  binafsi  wa mahakama  badala ya  kuziingiza  kwenye  mfuko  wa serikali .

Hivyo  amewataka  wananchi  kuendelea  kufika  ofisini kwake ama  ofisi  za wilaya   kutoa  taarifa  mbali mbali za  rushwa ama  kutumia  simu  0784606519/0754606519 ama  kupiga  simu ya  bure 113 au  *113# kupitia  huduma ya longa  nasi kwa ujumbe  mfupi SMS 113


Monday, April 23, 2018

JE UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUPENDEZESHA NYUMBA YAKO NA JUMIA?

Na Jumia Tanzania


Asilimia kubwa miongoni mwetu tunaishi kwenye nyumba ambazo hatuwezi kupaita ni nyumbani. Najua unaweza ukajiuliza kuna tofauti gani kati ya nyumba na nyumbani.

Nyumba ni jengo ambalo unaishi na kukupatia mahitaji yako ya msingi pamoja na hali ya usalama. Wakati, nyumbani ni mahali ambapo panakupatia amani na utulivu wa kiakili, mahali ambapo unatamani kuwepo pindi unapokuwa mbali na pilikapilika za ulimwengu.


Lakini jambo la kusikitisha miongoni mwa watu wengi wanaishi katika nyumba ambazo hazistahili kuziita ni nyumbani. Mwonekano wao nje na shughuli wanazozifanya ni tofauti kabisa na mahali wanapoishi na kutumia muda mwingi kutafakari mustakabali wa maisha yao ya kila siku.

Je na wewe unadhani kwamba nyumba yako unaweza kuiita ni nyumbani? Unajisikia vibaya kwamba sehemu unayoishi haistahili kuitwa nyumbani? USIJALI


Amini usiamini nyumba yako inaweza kuwa na muonekano mzuri, wa kisasa na wenye kustarehesha bila ya kutumia gharama kubwa! Jambo la msingi ni kufahamu ni kwa namna gani unaweza kufanya manunuzi ya vifaa ambavyo vitaipendezesha nyumba yako au sehemu unayoishi!

Jumia, inaendesha kampeni inayokwenda kwa jina la ‘BIG HOME MAKEOVER.’ Kampeni hii imedhamiria kuwawezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na nyumba zenye hadhi ya kuitwa nyumbani. Kupitia kampeni hii Jumia inalenga kupendezesha nyumba za wateja wake kwa kuwapatia mapunguzo makubwa ya bei ya vifaa mbalimbali vya nyumbani.


Akizungumzia juu ya kampeni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Vifaa vya Nyumbani wa Jumia Tanzania, Priscilla Eliphas ameelezea kuwa, “tumegundua kuwa watu wengi wana kasumba ya kutumia vifaa vya nyumbani kwao kwa muda mrefu. Kwa mfano, unaweza kukuta mtu anatumia jokofu (friji), jiko la umeme, mashine ya kufulia nguo au kupasha chakula moto pamoja na samani za ndani kwa muda wa takribani miaka 10! Na unaweza kustaajabu ni sababu zipi zinazopelekea mtu kuendelea kutumia vifaa kwa muda mrefu kiasi hiko! Na bado wengi miongoni mwao huendelea kuvitumia kadri iwezekanavyo. Tunafahamu kwamba vifaa kama hivyo ni uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye nyumba za kuishi hivyo ni dhahiri kwamba watu huwa makini kwenye ubora na makampuni yanayotengeneza hivo vifaa.” 

“Jumia inafahamu kwamba kufanya mabadiliko kwenye nyumba hususani kuifanya iwe na muonekano mpya na wa kuvutia ni kazi kubwa na tena yenye gharama. Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyotupelekea kuja na kampeni ya kupendezesha nyumba za wateja wetu. Kwa kuliona hilo tumekuja na kampeni ya zaidi ya wiki moja ya manunuzi ya vifaa tofauti vya nyumbani kama vile jikoni, sebuleni na mapambo ya nyumbani. Kampeni hii imeanza tangu Aprili 16 na kudumu mpaka Aprili 26, wateja wataweza kununua bidhaa lukuki za nyumbani kwa bei nafuu zenye ofa na mapunguzo makubwa,” alihitimisha.


Jumia inawasihi wateja wake kuitumia kampeni hii ipasavyo kwani wameshirikiana na kampuni kubwa za nchini Tanzania na kimataifa zinazotengeneza bidhaa zenye ubora wa kuaminika kama vile Samsung, Bruhm, Sony, Geepas, Nippotec, TCL, Star X, Philips, Aborder, Nikai, Ocean na Tronic. Cha kuvutia zaidi kuna mapunguzo ya bei, ofa, vocha za bure na zawadi kemkem kupitia kwenye tovuti yao! 

Wateja wanaweza kufanya manunuzi kwa urahisi kupitia mtandaoni, mahali popote walipo kwa bei za kipekee. Kwa kuongezea, bidhaa hufikishwa kwa mteja alipo kwa uharaka zaidi huku mteja akiwa na fursa ya kufanya malipo baada ya kuridhika na bidhaa alizoziagiza. Wateja wamepewa machaguo mengi zaidi ya bidhaa, takribani bidhaa zaidi ya 20,000 zimewekwa mtandaoni huku punguzo la bei likifika mpaka asilimia 60! 

TIMU ZAPUNGUA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MEI MOSI MKOANI IRINGA

Makamu mwenyekiti wa kamati ya michezo ya mei mosi kitaifa Joyce Benjamini akitoa kero ya kamati ya mashindano ya mei ya mosi taifa inasikitishwa na kupungua kwa timu shiriki katika mashindano hayo yanaendelea mkoa wa Iringa kutoka timu kumi na Tano (15) mwaka jana hadi timu kumi (10) mwaka huu 2018 mbele ya katibu tawala msaidizi mkoa Majuto Njanga  aliyekuja kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza. 

Viongozi mbalimbali wa michezo ya mei mosi wakiwa jukwani  wakipokea maandamano ya timu shiriki zilizokuwa zikiingia uwanjani
Timu ya uchukuzi na timu nyingine zikiingia uwanjani  
 Baadhi ya viongozi na wadau wakiwa jukwaani wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mei mosi katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora  

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

KAMATI ya mashindano ya mei ya mosi taifa inasikitishwa na kupungua kwa timu shiriki katika mashindano hayo yanaendelea mkoa wa Iringa kutoka timu kumi na Tano (15) mwaka jana hadi timu kumi (10) mwaka huu 2018.

Kauli hiyo imetolewa na makamu mwenyekiti wa kamati ya michezo ya mei mosi kitaifa Joyce Benjamini wakati wa uzinduzi wa michezo ya mei mosi kwenye kiwanja cha kumbuku ya Samora Mkoani Iringa.

Benjamini alisema kuwa kupungua kwa idadi ya timu shiriki kunatokana na baadhi ya mashirika ya sekta ya UMMA na serikali kushindwa kupeleka timu kwa visingizio vya ukata ili hali timu ya Rais ikiwa imeshiriki mashindaano hayo.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa tunapenda kutoa malalamiko yetu juu ya kupungua kwa hizi timu na kusingizia ukata wa pesa jambo ambalo sio kweli kwa kuwa waziri mkuu,makamu wa rais na rais wetu ni viongozi wapenda michezo hivyo uoga wao ndio umefanya kushindwa kuzileta timu zao zishiriki mashindano haya” alisema  Benjamini

Benjamini alisema kuwa hakuna mahali ambako rais amekataza wafanyakazi wa serikalini kutoshiriki michezo mbalimbali,viongozi wetu wa serikali wamekuwa waoga kwenye matumizi ya fedha za serikali,anachokitaka Rais ni uhalisia wa matumizi ya fedha katika maeneo husika.

“Mhesmimwa mkuu wa mkoa hata ukiangalia kwenye ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi mwaka 20102 ibara ya 61 ukurasa wa 218 hadi 219 unasema wajuu ya kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini,sasa kwanini viongozi hawafuati ilani hiyo” alisema  Benjamini

Benjamini alizitaja timu zinazoshiriki mashindano hayo mkoani Iringa kuwa ni timu kutoka Ofisi ya Rais –Ikulu,Wizara ya Uchukuzi,Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na sayansi (MUHAS),Hifadhi za Ngorongoro,Geita gold mine (GGM),Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),Shirika la umeme Tanzania (TANESCO),Tumbaku-TTPL ya Morogoro,Ukaguzi na Wenyeji timu ya RAS Iringa.

“Hizo ndio timu zilifika kwenye kituo hiki mkuu lakini nichukue nafasi kuzitaja timu ambazo zimenipa simanzi ya kutoshiki mashindano haya ni kama vile timu ya Ofisi ya Waziri mkuu,Wizara ya Mambo ya Ndani,Maliasilina Utalii,Wizara ya afya maendeleo ya jamii,timu za mashirika ya UMMa kama TTCL,Posta,Bima,NSSE na nyingine nyingi ambazo zilikuwa washirika wazuri wa michezo ya mei mosi” alisema

Akizungumza kwa niamba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza, katibu tawala msaidizi mkoa Majuto Njanga amezionya timu ambazo zinashiriki kwenye michuano ya mei mosi kuacha kuchukua wachezaji ambao sio wafanyakazi kwani kufanya hivyo kunapunguza ladha ya mashindano hayo.                                

Njanga alisema kuwa michezo hujenga undugu na furaha baina ya wanamichezo hivyo kuwaingiza wachezaji ambao sio wafanyakazi kwenye mashindano hayo wataondoa maana halisi ya mashindano hayo jambo ambalo linaweza kuwafanya kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea. 


“Mashindano haya ni ya wanamichezo wafanyakazi,kuna wale wanamichezo ambao sio wafanyakazi ambao wanajulikana kama mamluki au wavamizi kwamba hapa sio mahala pao nawasihi tuchezeshe wafanyakazi halisi ili mshindi apatikane kihalali na sio vyenginevyo kwa sababu ni hatari sana kumleta mwanamichezo ambaye sio mfanyakazi kwenye michezo hii anaweza kuvunjika mguu au akifa kwa mfano hatuombei itokee hiyo itakuwaje “Alisema Njanga 

Aidha Njanga alizitaka timu hizo kuacha kuwatumia wachezaji wa aina hiyo kwani wana madhara makubwa hasa pale yanapokuwa yakijitokeza kwa kuzitaka timu zenye utamaduni huo kuhakikisha wanaondokana nao. 
  
Hata hivyo Njanga alionekana kukerekwa na baadhi ya menejimenti za Taasisi,Mashirika na makampuni mbalimbali kuwa na utashi wa kutokupenda michezo na wengine kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha kuacha kufanya hivyo badala yake wamuunge mkono Rais Jakaya Kikwete katika jitihada zake za kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini. 

Akizungumzia waamuzi wanaochezesha mashindano hayo, Njanga aliwataka kuchezesha kwa haki bila upendeleo kwa kufuata sheria za mchezo husika ili mshindi aweze kupatikana kihalali kwa sababu wakienda kunyume chake wanaweza kusababisha tafrani na manung’uniko kwa baadhi ya timu shiriki. 

Hali kadhalika aliwataka kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano ikiwemo kukubaliana na matokeo pindi watakapojikuta wamefungwa wakati wa mashindano hayo. 

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More