Akikabidhi vifaa hivyo |
Kiswaga akieleza sababu za kufadhili ligi hiyo kwa lengo la kukuza sekta ya mchezo wa soka wilayani Iringa |
Wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa timu hizo |
na fredy mgunda,iringa
“HAKIKUSOEA
hata kidogo; kilicheza karata yake vizuri,” maneno hayo yanaweza kusemwa na
mpenda soka yoyote wa wilaya ya Iringa baada ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya
ya Iringa (IDFA) April 26, 2014 kumteua na kumsimika Mkurugenzi wa Kampuni ya
Tigo Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga kuwa mlezi wake.
Katika
awamu ya pili ya udhamini wake wa ligi soka nngazi ya wilaya hiyo maarufu kama
Kiswaga Cup; Kiswaga amemwaga vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 10 vitakavyotumiwa
na timu shiriki za ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi April 15, mwaka huu.
Hafla
ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilifanyika katika hoteli ya Gentle Hills juzi huku
ikihudhuriwa na Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Cecile Tiano aliyekabidhi
vifaa hivyo kwa timu hizo.
Vifaa
vilivyotolewa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na seti za jezi na
mipira.
Timu
hizo zinaingia katika msimu mwingine wa ligi hiyo huku ikikumbukwa kwamba timu
ya Ugwachanya FC ndiye bingwa wa ligi hiyo msimu uliopita
0 comments:
Post a Comment