mwanahabari frank kibiki, aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.
na mwandishi wetu,iringa
Wananchi wa manispaa
ya iringa wamempongeza , Frank Kibiki kwa kuanzisha mashindano ambayo yalengo
la kuwataka wakazi wa mkoa wa iringa kujua kuwa albino ni binadamu kama
binadamu wengine hivyo tunatakiwa kuacha kuwauwa na kuwa nyanyasa kijinsia.
Wakizungu kwa nyakati
tofauti na blog hii wamesema kuwa wazo la mbunge mtarajiwa la kutoa elimu ya kupinga
mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) kwa
njia ya michezo yatawasaidia wakazi wa manispaa kwa kuwa wananchi wengi
wanapenda michezo hivyo itakuwa rahisi kuwafikia.
Pia walimtaka FRANK
KIBIKI kuendelea na harakati za kupigania na kuwania ubunge wa jimbo la iringa
mjini kwa kuwa anakila sababu ya kufanya hivyo kutokana na malengo pamoja na
msimamo anaouonyesha kwa wakazi wa manispaa.
Kwa upande wao
viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) mkoani iringa wamempongeza na kumuomba katika
mashindano hayo wanaomba timu yao ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)kuwa
moja kati ya timu itakayoshiriki katika mashindano hayo.
“Tunaomba nasi
kushiriki katika mashindano hayo ya Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 kwa kuwa
ujumbe wa mashindano hayo unatulenga sisi, hivyo haitakuwa busara mashindano
yaendelee bila sisi kuleta timu uwanjani”walisema viongozi wa watu wenye
ulemavu wa ngozi (albino).
viongozi wa watu
wenye ulemavu wa ngozi (albino) waliwataka wananchi wa manispaa ya iringa
kumuunga mkono frank kibiki katika harakati zake za kugombea ubunge wa jimbo la
iringa mjini kwa kuwa anaoneka kabisa kuwajari wananchi wenye kipato kidogo
tofauti na wale wagombea wengine ambao wanatumia pesa nyingi kuutaka ubunge wa
jimbo hilo.
Walimalizia kwa
kusema kuwa kesho watapeleka barua maalum kwa frank kibiki ya kumpongeza na
kuwaomba wananchi wengine kumuunga mkono kibiki ili kuyafanya mashindano hayo
kuwa bora zaidi.
Naye Kibiki ametoa
wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia
kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
Alisema tayari
shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo,
ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao
wenyewe watajiongoza.
lakini kibiki hakusita kuwashukuru viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)mkoani iringa kwa kutambua lengo lake japo bado ajaletewa rasmi barua hiyo ya pongezi kwa naye amesikia tu kwa wananchi wakimshukuru kwa elimu na ujumbe aliouweka katika mashindano yake.
Kwa upande wao wadau
wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza
kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji
ikiwemo michuano ya watoto.
0 comments:
Post a Comment