JESHI
la Polis mkoani Kagera limeanza opereisheni ya kuwasaka waganga na
wapiga ramli,ikiwa ni harakati za kutokomeza vitendo vya mauaji
vinavyodaiwa kusababishwa na baadhi ya waganga wa kienyeji kwa kutoa
ushauri kwa waharifu.
Opereisheni hiyo endelevu imeanza Machi 4 kwa kuwahusisha katika
wilaya ya Biharamulo kwa kuwashirikisha askari Polis pamoja na kikosi
cha Mali Asili,nakufanikiwa kuwakamata jumla ya wapiga ramli 18
waliokuwa katika viji vya kata nne za Kabindi,Nyamigogo,Runazi na
Nyabizozi zote zikiwa ndani ya tarafa Nyarubunga wilayani Biharamulo.
Kamanda wa jeshi la Polis mkoani hapa Hennry Mwaibambe,akiongea
katika tukio hilo katika kituo cha Polis Kabindi,Opereisheni hiyo
imeanza ili kuhakikisha vitendo vya mauaji na kishirikina
vinatokomezwa,kwani vitendo vya mauaji vimekuwa vikishamiri katika
maeneo ya wilaya ya Biharamulo.
Kamanda Mwaibambe alisititiza kuwa opereisheni hiyo si nguvu ya
soda,bali itakuwa endelevu kwani wapo baadhi ya wahusika na vitendo vya
uharifu wa mauaji wamekuwa wakihusika katika mauaji ya binadamu kwa
kutafuta viungo vya binadamu hasa kwa kuwaua binadamu wenye ulemavu wa
ngozi(Albino)hivyo jeshi la Polis mkoani Kagera kwa kushirikiana na
maafisa wanyama poli poli la Burigi,watahakikisha wanapambana na hali
hiyo.
"Jeshi letu limejipanga kuhakikisha linalinda watu hawa(wenye
ulemavu wa ngozi)tunaomba jamii iwe tayari kuwafichua wale wote wenye
dhamira na kujihusisha katika vitendo hivyo vya kijama,vitendo hivi
vinalitia doa taifa letu,lazima tuhakikishe tunatokomeza hali hii!natoa
onyo kwa wale wanajihusisha na shughuli ya upigaji ramli na uganga wa
kienyeji.tabia hii haivumiliki tena!"alisisitiza Kamanda Mwaibambe.
Aliongeza mara baada ya kukamilika taratibu za mahojiano,watuhumiwa
wote 18 waliokamatwa watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka
yaliyo mbele yao.
Kwa upande wa Afisa Wanyama Poli Poli la Burigi Jimmy
Mushana,alisema opereisheni hiyo imefanikiwa kuwakamata waganga wa
kienyeji hao waliojihusha kupiga ramli na kumbaini walikuwa wana Nyara
za serikali kinyume cha sheria za nchi.
Alisema nyara mbalimbali zilizotokana na wanyama 39 na ndege
mmoja,ambazo thamani yake ni shilingi milion 60,464,250/=zilipatikana
kutokana opereisheni hiyo.
Wakati huo huo,jeshi la Polisi linaendelea kumhifadhi mtoto Mwenye
ulemavu wa ngozi(Albino)aliyedaiwa kutorokwa na mzazi(baba) wake
aliyejulikana kwa jina la Pius Simon(22)ambaye alitokomea kusikojulikana
kwa kisingizio kuwa alienda kuchoma mkaa.
Mtoto huyo Meshack Pius (3)aliachwa kwa babu yake aliyejukana kwa
jina la Simon Kagobe(70)mkazi wa Nyabizozi,tangu mnamo Fbruari 18 na
kuwepo hali ya hatari kwa kijana huyo,ambaye babu yake ilibidi
amsalimishe katika kituo cha Polis Kabindi kwa kuhofia mtoto huyo
kufanyiwa vitendo vya kinyama.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe,mtoto huyo Meshack bado anahudumiwa
na jeshi la Polis huku akiomba wasamalia wenye nia njema kujitokeza
kumsaidia mtoto huyo hasiye na hatia wakati utaratibu wa serikali
unatafuta jinsi ya kumsaidia kwani bado anahitaji huduma za malezi licha
ya kuwa na akili timamu na afya njema.
Tukio la jeshi hilo kupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi ni pili
ndani ya miezi miwili iliyopita mwaka huu,kwani mnamo Januari mwaka
huu,mtoto mwingine aliterekezwa kituoni hapo na kutafutiwa mazeneo ya
kuishi kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa.
0 comments:
Post a Comment