Friday, March 6, 2015

WALEMAVU IRINGA WALIA NA ALBINO

CHAMA cha watu wenye ulemavu, mkoani Iringa kimelaani vikali mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayoendelea nchini na kuitaka serikali kuandaa sheria kali itakayokomesha vitendo hivyo vya kikatili.
 
Mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa, Haluna Mbilinyi alisema kwa miaka mingi sasa walemavu wa ngozi wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa ndani ya nchi yao kutokana na kuuawa, huku viungo vyao vikikatwa bila huruma.
 
Mbilinyi alisema lazima sheria kali ya kuwabana watu wanaofanya ukatili huo ianishwe ili iwe fundisho kwa wale wenye mawazo finnyu kwamba viungo vya binadamu vinaweza kuwasababishia utajiri.
 
“Wakiwamaliza walemavu wangozi wanaweza kuhamia kwa walemavu wa viungo, hii ni hatari sana kwa jamii kwa sababu walemavu wenzetu wanaishi kwa kukimbia kikmbia ndani ya nchi yao wenyewe,”alisema Mbilinyi.
 
Aidha aliitaka jamii kufichua waovu na waganga wa kienyeji ambao wamekuwa chanzo kikubwa cha mauaji ya ngozo kwenye jamii.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More