SHULE
ya sekondari Nyabula imeingia katika hatua nyingine ya kukamilisha ujenzi wa
maabara zake baada ya kupata msaada unaohusisha mabati 50 na mifuko ya saruji
30.
Msaada
huo kwa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Parokia ya Nyabula
ulitolewa na mdau wa maendeleo ambaye pia ni Kamanda wa Chipukizi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) wa wilaya hiyo, Jackson Kiswaga.
Akikabidhi
msaada huo hivikaribuni, Kiswaga aliwataka wananchi kujitokeza kuchangia
shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao ili kuondokana na dhana ya
kila jambo kufanywa na serikali.
“Ukiwaita
watu kwenye harambee ya kufanikisha kwa mfano, harusi, wengi watajitokeza na
kutoa michango yao lakini ukiwaita kuchangia maendeleo yao hawajitokezi,”
alisema.
Alisema
katika dunia ya ushindani, elimu ndio ufunguo muhimu zaidi wa maisha
kwakuzingatia kwamba ukishakuwa nayo hakuna mtu wa kukupokonya.
“Elimu
ni kila katika katika ulimwengu huu unaolinganishwa hivisasa na kijiji kimoja.
Elimu ni maisha, elimu ni maendeleo kwahiyo nitoe wito kwa wazazi, walezi na
kila mwenye uwezo wa kufanya kazi aone umuhimu wa kuchanngia maendeleo yake,”
alisema.
Alisema
katika soko la ajira duniani kote waajiriwa wanapimwa au kupatikana kutokana
kwa kuzingatia vigezo vya elimu vinavyotakiwa.
“Kwahiyo
tukiulizwa vipaumbele vyetu, tunaweza kusema elimu elimu elimu kwasababu hiyo
pekee ndio inayoweza kutumika kubadili mazingira yetu na kutuletea maendeleo,”
alisema.
Kiswaga
alisema kwa kuzingatia hilo ataendelea kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu
wilayani humo na kwingine kote atakakoombwa kwa kuzingatia nafasi atakayokuwa
nayo.
Akishukuru
kwa msaada huo, Padri wa Parokia ya Nyabula Philipo Kindole alisema utasaidia
harakati zao za kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule hiyo na akaomba
wadau wengine kujitokeza kuichangia sekta hiyo.
0 comments:
Post a Comment