kulia ni Mwenyekiti wa mashindano ya Ritta Kabati challenge cup 2018 na kushoto ni katibu wa kamati ya mshindano hayo walipokuwa wakiongea na vyombo vya habari kwenye ofisi zao zilizopo manispaa ya Iringa mkoani Iringa mapema hii leo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Kamati ya ya mshindano ya Ritta
Kabati challenge cup 2018 imezindua rasmi kwa kuanza kuzialika timu kwa ajiri
ya kuchukua fomu kushiriki na wameweka bayana jinsi mfumo wa mashindano
utakavyokuwa pamoja na zawadi kwa washindi wote.
Akizungumza na waandishi wa
habari mwenyekiti wa mashindano hayo Gerald Malekela alisema kuwa analialika
timu mbalimbali za mkoa wa Iringa kuja kuchukua fomu za mashindano kwa gharama
ya shilingi elfu thelathini (30,000/=) ambazo zinapatikana katika kituo cha
radio cha Nuru Fm.
“Naomba viongozi wa vilabu
vinavyotaka kushiriki mashindano haya vinatakuwa kufika katika ofisi za Nuru fm
au kumpigia mratibu wa mashindano haya Fredy Mgunda kwa kumpigia simu ya
nambari 0714201006 au mnipigie mimi
mwenyewe kwa namba hii 0762687732 hapo utakuwa umerahisisha jinsi ya kuzipata
hizo fomu na maelezo kwa kina” alisema Malekela
Malekela alisema kuwa lengo la mashindano ni kuibua vipaji vya vijana mkoani Iringa,Kuonesha
uwezo wa vijana na kutengeneza ajira kwao,Kujenga
kizazi chenye afya bora na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi,Kutoa burudani
kwa wakazi wa iringa kwa mchezo wa mpira
wa miguu,Kuwakutanisha vijana pamoja ili kuzungumza lugha moja ya kimichezo na
maendeleo,Kuwaepusha vijana na makundi au vijiwe visivyo faa na Kuhamasisha
michezo katika mkoa wa Iringa,kutimiza agizo la makamu wa raisi juu ya kufanya
mazoezi
“Sasa hapo utagundua kuwa jinsi
gani mashindano hayo yalivyo yanaumuhimu katika kukuza vipaji hapa mkoani kwa
ustawi wa soka letu la nchi hiii” alisema Malekela
Aidha Malekela alizitaja zawadi pamoja na vifaaa ambavyo
vitatolewa kwa timu shiriki
VIFAA
msimu wa mwaka huu wa 2018 Kupitia mdhamini
RITTA KABATI tunataraji kutoa vifaa vya
michezo kama ifuatavyo kwa timu shiriki.
Kifaa
|
Muhusika
|
idadi
|
Mipira ya
mazoezi
|
Timu shiriki
|
Mpira mmoja
(1)
|
Jezi za mechi
|
Timu shiriki
|
Jezi set 1
|
Jezi za
waamuzi
|
Waamuzi
|
Set 6
|
D: ZAWADI.
No.
|
Muhusika
|
Zawadi ya
kwanza
|
Zawadi ya
pili
|
1.
|
Mshindi wa
kwanza
|
Kombe 1,000,000.00
|
2,000,000.00
|
2.
|
Mshindi wa
pili
|
1,000,000.00
|
|
3.
|
Mshindi wa
tatu
|
500,000.00
|
|
4.
|
Mchezaji bora
|
100,000.00
|
|
5.
|
Mfungaji bora
|
100,000.00
|
|
6.
|
Golikipa bora
|
100,000.00
|
|
7.
|
Waamuzi bora
|
100,000.00
|
|
8.
|
Kikundi bora
cha ushangiliaji
|
200,000.00
|
|
9.
|
Timu yenye
nidhamu
|
100,000.00
|
|
Jumla
|
1, 000,000.00
|
4,200,000
|
Ligi yetu itakuwa kama msimu
uliopita tutakuwa na hatua ya mtoano
kulingana na timu zitakazo jitokeza kuchukua fomu za kushiriki mashindano haya
na hatimaye kupata timu kumi ambazo zitacheza hatua ya makundi mawili na kupata
timu nne ambazo zitacheza nusu fainali na hatimaye fainal
Matarajio yetu mashindano
yatazinduliwa rasmi tarehe 10 mei 2018 siku ya jumapili wapi na itakuwaje na
nani atakuwa mgeni rasmi hayo yote yatawekwa bayana muda si mrefu.
Kama kamati tunamshuru sana Mh.
Mbunge Ritta Kabati kwa kukubali kudhamini mashindano haya na kuwathamini
vijana wa mkoa wa iringa fedha hii ambayo anaitoa kwaajili ya kufanya yote haya
angeitumia kwa kazi zake nyingine kwa maendeleo ya familia yake lakini kwa
kutambua nafasi aliyonayo na kuwathamini vijana ndio maana anafanya haya yote
hivyo sisi kamati tunamshukuru na kumpongeza aendelee kuwa na moyo huu.
Leo tarehe 21 / 5/ 2018 ndio
rasmi dirisha la uchukuaji fomu za usajili linafunguliwa na
litafungwa tarehe 31 /5/2018 – gharama
ya fomu ya usajili wa timu kwenye mashindano haya ya RITTA KABATI
CHALLENGE CUP IRINGA 2018 ni
shilingi 30,000.00 tu na fomu zinapatikana kwa kamati ya mashindano na
si kuingine, unaweza kupiga namba hii
kwa maelezo 0715779233 AU 0714201006 AU
0762687732, au wanaweza wakafika nuru fm ndiko viongozi tulipo.
0 comments:
Post a Comment