Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru mkoani hapa kwa kufanya shughuli ya kuzindua jumla ya miradi arobaini (40)
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa wakiwa wanamsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ofisini kwa hii leo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Jumla ya miradi 40 ya maendeleo
nyenye thamani ya shilingi 24,427,360,696 inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa
uhuru mkoani iringa kuanzia tarehe 23 / 05 /2018 wilayani mufindi.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa mwenge wa
uhuru utatembelea mira mbalimbali ikiwamo miradi kumi ya sekta ya elimu,afya
miradi saba,maji miradi mine ,maliasili mmoja,kilimo mitano,uvuvi mmoja viwanda
miwili na mapambano zidi ya rushwa mine.
“Gharama za miradi hiyo
zimetokana na michango ya wananchi shilingi 1,251,610,850, serikali kuu kiasi cha
shilingi 8,638,969,449.40, halmashauri
kiasi cha shilingi 253,564,461 na wadau wa maendeleo kiasi cha shilingi
14,283,215,936” alisema Masenza
Aidha Masenza aliitaja ratiba
ya mbio za mwenge wa uhuru mkoani Iringa itakuwa kama ifuatavyo tarehe 23 /05
2018 mwenge wa uhuru utapokelewa halmashauri ya Mufindi,tarehe 24 / 05 / 2018,
halmashauri ya wilaya ya iringa,tarehe tarehe 25 / 05 / 2018 halmashauri ya
Kilolo, tarehe 26 / 05 / 2018 halmashuri ya manispaa ya iringa na tarehe 27 /
05 / 2018 na halmashauri ya mji wa Mafinga na baada ya hapo mwenge wa uhuru
utaelekea mkoani Njombe kuanzia tarehe 28 / 05 / 2018.
Masenza alisema kuwa kauli mbiu
ya mwaka 2018 ya mwenge wa uhuru ni elimu ni ufunguo wa maisha ;wekeza sasa kwa
maendeleo ya taifa letu. Na ujumbe huo unalenga kuweka mkazo kwenye
umuhimu wa uwekezaji wa elimu bora unaofanywa na serikali pamoja na wananchi wa
maeneo husika.
“Serikali imeweka mikakati
madhubuti ya kupinga vita umsikini na kujenga taifa lenye maendeleo ya viwanda
hivyo ndio maana katika maeneo mengi hapa nchini swala la elimu limepewa
kipaumbele na kuhakikisha kuwa tunapata wasomi wengi ambao watasaidia kuendesha
viwanda hapa nchini” alisema Masenza
Masenza alisema kuwa mbio za
mwenge wa uhuru mwaka 2018 zilizinduliwa mkoani Geita na mheshimiwa waziri mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 2 /5 / 2018 na mwenge huu utakimbizwa
kwa mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhitimishwa na rasmi na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani tanga tarehe 14 /10 /2018
0 comments:
Post a Comment