Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea na viongozi wa misikiti yote ya manispaa ya Iringa wakati wa utoaji sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya kiislamu
wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa waislamu
wa wote wa manispaa ya Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka ya tunda la tende kwa waiislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikabidhi tende alizokabidhiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka kwa waiislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Mkuu wa walimu na msimamizi wa misikiti ya Dhinureyn Tanzania Abdul Salam Ahmad Ayub akimshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa sadaka aliyoitoa kwa waislam katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na viongozi wa misiki ya manispaa ya Iringa walipohudhulia zoezi la utoaji wa sadaka ya tende ilitolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya kiislamu
wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa waislamu
wa wote wa manispaa ya Iringa
Akizungumza wakati wa kukabidhi
sadaka hiyo katika msikiti wa Dhinureyn Gangilonga Kabati alisema kuwa kila
mwaka amekuwa akifutulisha katika maeneo mbalimbali hivyo mwaka huu ameamua
kununua tende na kugawa kwenye misikiti yote ya manispaa ya Iringa.
“Unajua mwaka huu tende ni
tunda ambalo linahitajika katika kipindi hiki cha mfungo na kuna watu ambao
hawana uwezo wa kununua tende hizi na ukiangalia mwaka huu tende zimepanda bei
sana hivyo kwa kiasa ambacho nakipata nimeamua kutoa sadaka hii kwa waumini wa
kiislam” alisema Kabati
Kabati aliwataka wananchi
wengine kuendelea kumuabudu mwenyezi mungu pale ambapo tunapata nafasi ili
kupunguza maovu ambayo tumekuwa tukiyatenda kwa kukusudia au bila kukusudia na
kufanya hivyo basi mwenyezi mungu atatuongezea pale ambapo tumepunguza kwa
ajili ya kumtumiaka mungu.
“Katika kipindi hiki nawaomba
wazazi,walezi na viongozi wetu naomba tutoe elimu kwa vijana wetu kwa kuwapa
elimu ya dini pamoja maadili ya nchi yetu kwa lengo la kuwajenga vijana wawe
wanamcha mungu hasa kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa ametoa
sadaka ya tende tani mbili ambayo ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa
kwa ajili ya misikiti yote na vituo vya watoto yatima ambavyo vinawatoto wa
kiislam ambao wanafunga katika kipindi hiki cha mfungo.
“Mimi nimeleta tani mbili ili
kuongezea nguvu wafungaji wa kipindi hiki lakini kutoa sadaka kwa mwenyezi
mungu katika kipindi ambacho waislamu wapo kwenye mfungo wa ramadhan
nakuwasidia wale ambao hawana uwezo wa kununua tunda hili la tende” alisema Kabati
Kwa upande wake mgeni rasmi
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka ya tunda la tende kwa
waiislamu katika kipindi hiki cha mfungo
wa ramadhan.
“Tunashukuru sana kwa sadaka
hii ambayo umetusaidia kwa waislam wa manispaa ya Iringa kwa msaada wako ambao
utasiadia kwa wale ambao wanamahitaji maalumu na mungu atakuongezea aple
ulipopunguza na mungu akubariki” alisema Masenza
Masenza aliwaomba maimamu
kuwagawia tende hizo waislam ambao hawana uwezo wa kununua tende tukani ili nao
wapate hiki chakula cha kwanza pindi unapofungua na wale wenye uwezo wa kununua
tende dukani basi waendelee kununua
Naye mkuu wa walimu na
msimamizi wa misikiti ya Dhinureyn Tanzania Abdul Salam Ahmad Ayub alisema kuwa
msaada aliotoa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi
(CCM) Ritta Kabati utawasaidia waislam waliofunga.
“Sadaka hii aliyoitua huyu
mbunge Kabati umekuja wakati muafaka na umamanufaa makubwa sana kwa waislam kwa
kuwa tumehimizwa kufuturu kwanza tende hivyo kwa muislam kula tende ni fadhila
kubwa sana”alisema Ayub
Ayub alisema kuwa katika
kipindi hiki cha mfungo waislam tunatakiwa kupeana vyakula ili kila mtu ambaye
hana kitu aweze kupata chakula na ndio alivyofanya huyu mbunge Ritta Kabati kwa
waislam wa manispaa ya Iringa.
“Zamani watu walikuwa
wanatandika jamvi nje wakati wa kufutulu ili waweze kufutulu na waislam ambao
hawana uwezo na ndio uzalendo wenyewe huo,hivyo tunamuombea mbunge huyu
aendelee na moyo huo huo” alisema Ayub
0 comments:
Post a Comment