Afisa mradi wa shirika lisilo la kiserikali la
peoples development forum (PDF) ambalo linafadhiwa na UNICEF
upande wa usafi wa mazingira lishe bora watoto
Adventina Lazaro akitoa neno kwa wazazi na wanafunzi juu ya kutambua na kutoa elimu juu ya hedhi na jinsi ya kujihifadhi kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mwesa wakiwa na mabango yakiwa na maandishi yaliyoandikwa kwa maneno tofauti tofauti wakatika maadhimisho ya siku ya hedhi duniani
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Mwesa wakitengeneza pedi za asili kwa kuonyesha kuwa sio lazima kununua dukani bali waweza kutengeneza hata nyumbani kwako na zikakustili vizuri tu
NA FREDY MGUNDA, MUFINDI IRINGA.
SHIRIKA lisilo la kiserikali la
peoples development forum (PDF) ambalo linafadhiwa na UNICEF mkoani Iringa
wilaya ya Mufindi limelenga kuwawezesha wasichana kutimiza ndoto za maisha yao
kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowafanya wabaki nyuma katika
kuhudhuria masomo kipindi wakiwa katika hedhi.
Hayo yamezungumzwa na afisa mradi wa
shirika lisilo la kiserikali la peoples development forum (PDF) upande wa usafi
wa mazingira lishe bora watoto Adventina Lazaro wakati wa maadhimisho ya siku
ya hedhi Duniani ambapo wilaya ya Mufindi yalifanyika katika shule ya msingi
Mwesa kata ya Mtambula,tarafa ya Kasanga lakini kimkoa yalifanyika kwa mara ya
kwanza katika Bustani za Manispaa na kuhudhuriwa na wanafunzi wa kike kutoka
shule mbalimbali za sekondari za mjini hapa
Lazaro alisema kuwa changamoto kubwa
ambayo wanakabiliana nayo watoto wa kike wengi walioko mashuleni ni kipindi cha
hedhi ambapo baadhi yao wamekuwa hawana elimu, kutojiamini na utoro mashuleni
wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi hali inayosababisha utoro.
lazaro alisema kuwa ni jukumu la kila
mmoja kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anahudhuria masomo yake kwa mwaka mzima
pasipo kuwa na vikwazo vinavyosababishwa ama na mazingira duni au ukosefu wa
bajeti katika kupata taulo hizo maalum za hedhi.
Aliwataka wadau na wananchi kwa
ujumla kuvunja ukimya juu ya suala la hedhi salama kwa mtoto wa kike na
kuwezesha mtoto wa kike kupata taulo maalum kila mwezi na mkoa wa Iringa una
mkakati maalum wa kumaliza changamoto hizo.
“Changamoto mbalimbali zinazowakabili
wasichana wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi yanapaswa kujadiliwa na
kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuwa yanachangia kurudisha nyuma jitihada za
kuwainua watoto wa kike nchini na kuwataka mabinti kuondoka na aibu ya katika
suala la hedhi hivyo mkakati upo kumaliza kwa kuwapatia bure mataulo maalum
watoto wa kike” alisema lazaro
Alisema kuwa serikali ya awamu ya
tano inayo dhamira ya dhati kuhakikisha elimu bure inapatikana kwa jinsia zote
hivyo basi suala la hedhi salama kwa wa kike ni jambo la msingi katika ngazi ya
familia, jamii, na hata mashuleni kuwapatia elimu itakayowezesha kuwa na
ufahamu wa masuala ya hedhi.
Awali diwani wa kata ya Mtambula, Isack
Kilamlya alisema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuvunja ukimya juu ya masuala
ya hedhi ikiwemo kuondokana na dhana potofu kwamba hedhi ni ugonjwa pamoja na
namna bora ya kuhakikisha mtoto wa kike anajiweka katika hali ya usafi ili
abaki shuleni badala ya kukosa masoko kila apatapo hedhi.
Kilamlya Alisema ukosefu wa mazingira
bora kama vyoo, maji safi na salama pamoja na vyumba mahsusi vya kubadilishia
nguo, hasa kwa watoto wa kike wanapokua katika hedhi mashuleni kuna changia
utoro.
“Hakuna vikwazo zaidi wezesha
wanawake na wasichana kupata hedhi salama hivyo wananchi wanapaswa kutoa
ushikiano kwa shirika hilo lina mikakati ya kuwezesha watoto wa kike kupata
elimu kwa mtoto kike kama wanafunzi wengine na kuhudhuria masomo yake akiwa
huru” alisema Kilamlya
Akisoma risala kwa mgeni rasmi Adili
Mlema mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Mwesa alisema kuwa
analishukuru shirika lisilo la kiserikali la peoples development forum (PDF) ambalo
linafadhiwa na UNICEF kutoa elimu ya maswala ya hedhi ambayo sasa yamekuwa
msaada kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mlema aliongeza kwa kuwataka wazazi
na viongozi mbalimbali wa serikali na wasio wa serikali kutoa elimu ya hedhi
kwa jamii husika ili kuondoa aibu ambayo wazazi wengi wanayo katika kuwaeleza
watot wao wa kike.
“Bila shirika lisilo la kiserikali la
peoples development forum (PDF) hadi leo hii tungekuwa hatuna elimu ya maswala
ya hedhi ambapo wanafunzi wengi walikuwa wanaona aibu kuja shule siku wakiwa
katika siku za hedhi” alisema Mlema
Naye mmoja wa wazazi aliyehudhulia
siku ya hedhi wilaya ya Mufindi Emeliziena Danda aliwataka wazazi kutoa elimu
juu ya hedhi kwa watoto wa kike wanakaribia kuvunja ungo ili wajue elimu hiyo.
“Nawapongeza sana shirika lisilo la
kiserikali la peoples development forum (PDF) kuwa kututoa aibu wananchi kwa
kutuambia ukweli ambao leo hii tumekuwa huru kuwaambia watoto wenu na watoto
wetu nao wamekuwa huru kutuambia nini kinachiwatokea” alisema Danda.
0 comments:
Post a Comment