NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MBUNGE wa viti
maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa
sadaka ya tende,pesa taslimu kiasi cha shilingi laki saba (700,00) na msaada wa
mataulo maalumu kwa wafungwa wa Gereza manispaa ya Iringa kwa ajili wanawake
kuyatumia wakati wakiwa katika kipindi cha hedhi.
Akizungumza na
waandishi wa habari mbunge Ritta Kabati alipowatembelea wafungwa wa Gereza la
wilaya ya Iringa alisema kuwa lengo la kwenda kuwatembelea wafungwa ni kwenda
kuzijua changamoto ambazo wamekuwa wanakabiliana nazo wakiwa kifungoni.
“Mimi nimekuwa
muumini mkubwa sana kwa kujihusisha na maswala ya kijamii hivyo hii leo sio
mara yangu ya kwanza kuja hapa Gerezani nimekuja mara nyingi na nimesikiliza
kero nyingi na ndio maana zimekuwa zikitatuliwa mara kwa mara kwa kuwa huwa
nawasemea vizuri nikiwa bungeni kwenye kuchangia hoja” alisema Kabati
Kabati alisema
kuwa licha ya kuwa anakwenda kuwatembelea mara kwa mara lakini huwa anabeba
zawadi kwa ajili ya wafungwa,hata hivyo alifanikiwa kutoa zawadi ya sadaka ya
tunda la tende kwa ajili ya wafungwa waislamu ambao wamefungwa katika
gereza hilo.
“Huu ni mwezi
mtukufu hivyo nimeamua kuja na tende hizi angalau na wafungwa waislamu na
wapate tunda hilo ambalo waislamu wengi wamekuwa wakilitumia wakati mfungo wa
ramadhani na huu ndio wakati sahihi ndio maana nimefanya hivyo” alisema Kabati
Aidha Kabati alisema
kuwa ametoa msaada wa mataulo maalum kwa wafungwa wanawake kwa ajili ya
kuwayatumia wakati wakiwa kwenye kipindi hedhi pamoja na kuchangia kiasi cha
shilingi laki saba (700,00) pesa taslimu.
“Mimi ni mwanamke
hivyo najua mahitaji yetu sisi akina mama hivyo msaada wangu huu wa haya
mataulo maalum utaweza kuwasaidia kwa kipindi ambacho wapo Gerezani kwa kuwa
wanaweza kuyatumia na kuyafua na kuendelea kutumia tena na pesa ambazo nimetoa
nyingine zilikuwa ahadi za msimu ulipita nilipokuja kutelea hapa hivyo nimetoa
hizo pesa pamoja na kuwaongeza nyingine” alisema Kabati
Kabati
aliwapongeza viongozi wa gereza hilo kwa kuanzisha kiwanda kidogo ndani ya
gereza hilo na kuwanya wafungwa kuongeza ujuzi na wengine kuendelea kukuza
vipaji vyao wakiwa gerezani.
Naye mwenyekiti wa Jumuiya
ya wanawake wa Chama
Cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Iringa
Nicolina Lulandala alimpongeza
MBUNGE wa viti maalum mkoa
wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kujitoa kuisaidia
jamii ambayo imekuwa ikikumbana na changamoto nyingi.
“Toka jana juzi na siku zilizopita watanzania
na wanairinga tumeshuhudia shughuli anazozifanya huyu mbunge hivyo ni lazima
sisi cha viongozi wa chama kumuunga mkono kwenye juhudi zake maana tusipofanya
hivyo tutamkatisha moyo wa kujitolea kama ambavyo anafanya sasa” alisema
Lulanda
Lulanda aliwapongeza pia viongozi wa gereza
kwa kuanzisha kiwanda kidogo ndani ya gereza kitu ambacho kinaongeza ufanisi wa
kazi kwa wafungwa na kuendelea kukuza vipaji vyao na kuibua pia vipaji vipya
ndania ya gereza.
“Mimi na wezangu ambao tumefika hapa gerezani
tumefurahi sana kitendo cha kuona kuwa kuwa kunakiwanda cha kutengeneza vikapu
fagia na vitu vingine kweli nimefarijika ndio maana tukashawishi hata kuvinunua
bidhaa ambazo wanazingeneza ambazo zinaubora mzuri kweli” alisema Lulanda
0 comments:
Post a Comment