Friday, March 20, 2015

MKURUGENZI WA TIGO JACKSON KISWAGA ATUMIA ZAIDI YA SH MILIONI 10 KUFANIKISHA LIGI SOKA WILAYA YA IRINGA MAARUFU KAMA KISWAGA CUP



Kamu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Cecile Tiano akikabidi jezi kwa moja ya timu zinazoshiriki ligi ya wilaya ya Iringa (Kiswaga Cup) anayeshuhudia kushoto ni mdhamini wa ligi hiyo Jackson Kiswaga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini

Akikabidhi vifaa hivyo

Kiswaga akieleza sababu za kufadhili ligi hiyo kwa lengo la kukuza sekta ya mchezo wa soka wilayani Iringa

Wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa timu hizo

 na fredy mgunda,iringa
“HAKIKUSOEA hata kidogo; kilicheza karata yake vizuri,” maneno hayo yanaweza kusemwa na mpenda soka yoyote wa wilaya ya Iringa baada ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Iringa (IDFA) April 26, 2014 kumteua na kumsimika Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga kuwa mlezi wake.



Katika awamu ya pili ya udhamini wake wa ligi soka nngazi ya wilaya hiyo maarufu kama Kiswaga Cup; Kiswaga amemwaga vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 10 vitakavyotumiwa na timu shiriki za ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi April 15, mwaka huu.



Hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilifanyika katika hoteli ya Gentle Hills juzi huku ikihudhuriwa na Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Cecile Tiano aliyekabidhi vifaa hivyo kwa timu hizo.



Vifaa vilivyotolewa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na seti za jezi na mipira.


Taarifa kamili ya kilichofanywa na Kiswaga ambaye pia ni Kamanda wa Chipukizi wa Chama cha Mapiduzi Wilaya ya Iringa katika kufanikisha ligi hiyo kitakujia leo.
 
Timu hizo zinaingia katika msimu mwingine wa ligi hiyo huku ikikumbukwa kwamba timu ya Ugwachanya FC ndiye bingwa wa ligi hiyo msimu uliopita

MSHINDI KISWAGA CUP IRINGA VIJIJINI KUONDOKA NA KOMBE NA MILIONI MOJA, ZAWADI LUKUKI KUTOLEWA KWA WASHINDI WENGINE


Monday, March 16, 2015

VIONGOZI WA ALBINO MANISPAA YA IRNGA WAMBARIKI FRANKI KIBIKI KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI

 mwanahabari frank kibiki, aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.

 na mwandishi wetu,iringa



Wananchi wa manispaa ya iringa wamempongeza , Frank Kibiki kwa kuanzisha mashindano ambayo yalengo la kuwataka wakazi wa mkoa wa iringa kujua kuwa albino ni binadamu kama binadamu wengine hivyo tunatakiwa kuacha kuwauwa na kuwa nyanyasa kijinsia.



Wakizungu kwa nyakati tofauti na blog hii wamesema kuwa wazo la mbunge mtarajiwa la kutoa elimu ya kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino)  kwa njia ya michezo yatawasaidia wakazi wa manispaa kwa kuwa wananchi wengi wanapenda michezo hivyo itakuwa rahisi kuwafikia.



Pia walimtaka FRANK KIBIKI kuendelea na harakati za kupigania na kuwania ubunge wa jimbo la iringa mjini kwa kuwa anakila sababu ya kufanya hivyo kutokana na malengo pamoja na msimamo anaouonyesha kwa wakazi wa manispaa.



 Kwa upande wao viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)  mkoani iringa wamempongeza na kumuomba katika mashindano hayo wanaomba timu yao ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)kuwa moja kati ya timu itakayoshiriki katika mashindano hayo.



“Tunaomba nasi kushiriki katika mashindano hayo ya Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 kwa kuwa ujumbe wa mashindano hayo unatulenga sisi, hivyo haitakuwa busara mashindano yaendelee bila sisi kuleta timu uwanjani”walisema viongozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).





viongozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) waliwataka wananchi wa manispaa ya iringa kumuunga mkono frank kibiki katika harakati zake za kugombea ubunge wa jimbo la iringa mjini kwa kuwa anaoneka kabisa kuwajari wananchi wenye kipato kidogo tofauti na wale wagombea wengine ambao wanatumia pesa nyingi kuutaka ubunge wa jimbo hilo.



Walimalizia kwa kusema kuwa kesho watapeleka barua maalum kwa frank kibiki ya kumpongeza na kuwaomba wananchi wengine kumuunga mkono kibiki ili kuyafanya mashindano hayo kuwa bora zaidi.





Naye Kibiki ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.





Alisema tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe watajiongoza.

lakini kibiki hakusita kuwashukuru viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)mkoani iringa kwa kutambua lengo lake japo bado ajaletewa rasmi barua hiyo ya pongezi kwa naye amesikia tu kwa wananchi wakimshukuru kwa elimu na ujumbe aliouweka katika mashindano yake.



Kwa upande wao wadau wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.








Thursday, March 12, 2015

ZAIDI ya watu 40 wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea katika mji mdogo wa mafinga



Wednesday, March 11, 2015

IRINGA KIBIKI CHILDREN CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI IRINGA




 MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI

MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI na wanahabari
 
NA MWANDISHI WETU, IRINGA
LIGI inayoshirikisha  watoto walio chini ya umri wa miaka 16, inaloitwa  Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) inatarajia kuanza kutimua vumbi jumamosi ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa.
Mratibu wa ligi hiyo, Haruna Salehe alisema lengo la mpira huo ni kukuza vipaji vya watoto na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu wa ngozi nchini.
Alisema ligi hiyo iliyobuniwa na kuendeshwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, inatarajia kushirikisha timu nane za watoto katika manispaa ya Iringa.
“Lengo kubwa ni kukuza vipaji na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wenzetu walemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku bila huruma jambo ambalo, hatutaki liendelee kwenye jamii yetu,”alisema
Alisema michuano hiyo itakuwa ikifanyika katika uwanja wa mwembetogwa ambao ni wa wazi ili watu wengi wapate nafasi ya kushiriki.
Kwa upande wake, mdau wa soka na mwanahabari wa gazeti hilo, Frank Kibiki alisema ameamua kubuni ligi hoyo ili kupanda mbegu ya kupenda michezo na kutambua vipaji vya soka tangu utotoni, ili iwe rahisi kuwapata wachezaji bora siku zijzo.
“Mpira ni ajira na huu hauna dini, kabira wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza kushiriki kwenye mpira hivyo tumebuni jambo hili ili kuendelea kukuza vipaji huku tukibeba ujumbe wa kupinga ukatili kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,”alisema
Kibiki ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
Alisema tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe watajiongoza.
Kwa upande wao wadau wa soka, manispaa yaa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.

Friday, March 6, 2015

WAKAZI 10000 KUNUFAIKA NA UKARABATI BWAWA LA KALEMAWE

DSC_0001
Mshehereshaji wa kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Mtaalamu wa masuala ya fedha wa UNCDF, Bw. Imanuel Muro akisherehesha kongamano hilo. Katikati ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akifuatiwa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika.
Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya watu 10,000 wanaozunguka bwawa la Kalemawe wilayani Same mkoani Kilimanjaro watanufaika na ukarabati wa bwawa hilo na kuwekewa muundo mpya wa kiutawala na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji wa Mitaji (UNCDF).
Bwawa hilo ambalo lipo katika kata za Kalemawe na Ndungu lilijengwa na watawala wa Kiingereza mwaka 1952-1959 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo na ufugaji baada ya kuanzishwa kwa hifadhi ya Mkomazi na hivyo wakazi kuzuiwa kwenda katika hifadhi hiyo kwa shughuli mbalimbali.
Taarifa ya kuwepo kwa mradi huo mkubwa, imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini, Bw. Peter Malika wakati akiwakaribisha madiwani wa kata hizo ambao wameitwa katika kongamano la siku moja Dar es salaam kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa hilo.
DSC_0038
Pichani juu na chini ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi kufungua rasmi kongamano hilo.
Malika amesema Mfuko huo wa ukuzaji wa mitaji unasaidia ukarabati wa bwawa hilo kupitia mpango wake wa uendelezaji rasilimali kwa kutumia fedha za ndani (LFI) .
Amesema baada ya ukarabati huo, mradi utaendeshwa kwa pamoja kati ya serikali na watu binafsi.
Malika alisema ukarabati huo unakidhi lengo la mfuko ambalo ni kuwezesha miundombini inayoleta maendeleo.
“Ukarabati na hatimaye uendeshaji wa bwawa hilo kutasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya mitaji kwa watu binafsi na umma.” alisema
DSC_0026  
Kongamano hilo lililofunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi lilizungumzia masuala ya umiliki, masuala ya kisheria ya taasisi, utawala bora, masuala ya kiufundi ya ukarabati,uvuvi wa samaki wa kibiashara, matumizi ya maji kwa ajili ya umwagiliaji, ufugaji, mabadiliko ya tabia nchi na mazingira, uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake, mfumo wa utoaji wa huduma za fedha na masuala mengi mengine ya mipango ya maendeleo endelevu.
Kapufi alisema kwamba pamoja na kushukuru Mfuko wa Mitaji kukubali kuwasaidia, amesema bwawa hilo ni muhimu sana katika kuondoa migogoro na migongano ndani ya jamii pia na mamlaka ya hifadhi ya Mkomazi.
Alisema kurejeshwa kwa hali yake ya zamani kutasaidia wafugaji, wakulima na watumiaji wengine wa bawawa hilo kama wavuvi wa samaki kila mmoja kuwa na nafasi katika matumizi ya bwawa.
DSC_0067
Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akizungumza kwenye kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro lililoandaliwa na UNCDF.
Aidha alisema ukarabati utakaofanywa na muundo wa uendeshaji wa bwawa hilo utasaidia wilaya pia kufikiria namna ya kutengeneza bwawa jingine katika Mto Ruvu kwa sababu kama hizo za kuwapa uwezo zaidi wananchi katika maendeleo yao kwa kutumia rasilimali maji.
Toka kujengwa kwake katika miaka ya 1950, bwawa hilo lenye urefu wa takaribani kilomita tatu na upana wa mita 200 limepungua ukubwa wake kwa karibu nusu ya uwezo wa awali kwa sababu za kujaa tope, matumizi mabaya, kukosa ukarabati na usimamizi.
Aidha limeota magugu maji ambayo inaua kizazi cha samaki na kuvuruga uvuvi.
DSC_0072
Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akisisitiza jambo kwenye kongamano hilo lililowakutanisha madiwani wa kata za halmshauri ya wilaya ya Same na wataalam kutoka UNCDF kujadili pamoja kabla ya utekelezaji.
DSC_0082
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano hilo la siku moja ambao ni madiwani wa kata za Same, mainjinia na wakandarasi kutoka halmashauri ya wilaya ya Same pamoja na wataalam kutoka UNDCF.
DSC_0028
DSC_0096
Washiriki wakitamaza video ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro kujionea hali halisi ya bwawa hilo linalohitaji ukarabati.
20140626_124641
Pichani juu na chini ni muonekano wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati UNCDF walipotembelea eneo hilo.
20140626_124736

JESHI LA POLISI KAGERA LAANZA KUWANUSURU ALBINO NA KIFO...LAANZA KUWASAKA WAGANGA NYUMBA HADI NYUMBA

JESHI la Polis mkoani Kagera limeanza opereisheni ya kuwasaka waganga na wapiga ramli,ikiwa ni harakati za kutokomeza vitendo vya mauaji vinavyodaiwa kusababishwa na baadhi ya waganga wa kienyeji kwa kutoa ushauri kwa waharifu.
Opereisheni hiyo endelevu imeanza  Machi 4 kwa kuwahusisha katika wilaya ya Biharamulo kwa kuwashirikisha askari Polis pamoja na kikosi cha Mali Asili,nakufanikiwa kuwakamata jumla ya wapiga ramli 18 waliokuwa katika viji vya kata nne za Kabindi,Nyamigogo,Runazi na Nyabizozi zote zikiwa ndani ya tarafa Nyarubunga wilayani Biharamulo.
 
Kamanda wa jeshi la Polis mkoani hapa Hennry Mwaibambe,akiongea katika tukio hilo katika kituo cha Polis Kabindi,Opereisheni hiyo imeanza ili kuhakikisha vitendo vya mauaji na kishirikina vinatokomezwa,kwani vitendo vya mauaji vimekuwa vikishamiri katika maeneo ya wilaya ya Biharamulo.
 
Kamanda Mwaibambe alisititiza kuwa opereisheni hiyo si nguvu ya soda,bali itakuwa endelevu kwani wapo baadhi ya wahusika na vitendo vya uharifu wa mauaji wamekuwa wakihusika katika mauaji ya binadamu kwa kutafuta viungo vya binadamu hasa kwa kuwaua binadamu wenye ulemavu wa ngozi(Albino)hivyo jeshi la Polis mkoani Kagera kwa kushirikiana na maafisa wanyama poli poli la  Burigi,watahakikisha wanapambana na hali hiyo.
 
"Jeshi letu limejipanga kuhakikisha linalinda watu hawa(wenye ulemavu wa ngozi)tunaomba jamii iwe tayari kuwafichua wale wote wenye dhamira na kujihusisha katika vitendo hivyo vya kijama,vitendo hivi vinalitia doa taifa letu,lazima tuhakikishe tunatokomeza hali hii!natoa onyo kwa wale wanajihusisha na shughuli ya upigaji ramli na uganga wa kienyeji.tabia hii haivumiliki tena!"alisisitiza Kamanda Mwaibambe.
 
Aliongeza mara baada ya kukamilika taratibu za mahojiano,watuhumiwa wote 18 waliokamatwa watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yaliyo mbele yao.
 
Kwa upande wa Afisa Wanyama Poli Poli la Burigi Jimmy Mushana,alisema opereisheni hiyo imefanikiwa kuwakamata waganga wa kienyeji hao waliojihusha kupiga ramli na kumbaini walikuwa wana Nyara za serikali kinyume cha sheria za nchi.
 
Alisema nyara mbalimbali zilizotokana na wanyama 39 na ndege mmoja,ambazo thamani yake ni shilingi milion 60,464,250/=zilipatikana kutokana opereisheni hiyo.
 
Wakati huo huo,jeshi la Polisi linaendelea kumhifadhi mtoto Mwenye ulemavu wa ngozi(Albino)aliyedaiwa kutorokwa na mzazi(baba) wake aliyejulikana kwa jina la Pius Simon(22)ambaye alitokomea kusikojulikana kwa kisingizio kuwa alienda kuchoma mkaa.
 
Mtoto huyo Meshack Pius (3)aliachwa kwa babu yake aliyejukana kwa jina la Simon Kagobe(70)mkazi wa Nyabizozi,tangu mnamo Fbruari 18 na kuwepo hali ya hatari kwa kijana huyo,ambaye babu yake ilibidi amsalimishe katika kituo cha Polis Kabindi kwa kuhofia mtoto huyo kufanyiwa vitendo vya kinyama.
 
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe,mtoto huyo Meshack bado anahudumiwa na jeshi la Polis huku akiomba wasamalia wenye nia njema kujitokeza kumsaidia mtoto huyo hasiye na hatia wakati utaratibu wa serikali unatafuta jinsi ya kumsaidia kwani bado anahitaji huduma za malezi licha ya kuwa na akili timamu na afya njema.
 
Tukio la jeshi hilo kupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi ni pili ndani ya miezi miwili iliyopita mwaka huu,kwani mnamo Januari mwaka huu,mtoto mwingine aliterekezwa kituoni hapo na kutafutiwa mazeneo ya kuishi kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More