Friday, July 28, 2017

DIWANI KISOMA AKATAA AGIZO LA KUSHUSHA BENDERA ZA CHADEMA SOKO KUU MJINI MAFINGA

 Diwani wa  kata ya Boma katika Jimbo la Mafinga Mjini Jurist Paulo Kisoma  akizungumza na waandishi wa Habari juu ya kukataa agizo la Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini mh Charles Makoga
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mafinga Charles Makoga akiliongoza baraza la madiwa wa halmashauri ya Mafinga Mjini na kutoa agizo la kushushwa kwa bendera zote zilizopo soko kuu la mjini Mafinga.

Na fredy Mgunda, Iringa.

Diwani wa  kata ya Boma katika Jimbo la Mafinga Mjini Jurist Paulo Kisoma amelikataa angilo za Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mafinga Charles Makoga la kushusha bendera zote zilizopo soko kuu la mjini hapo.
Agizo hilo lilitolewa wakati wa baraza la madiwani lilofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiii,Makoga alisema kuwa wanasiasa wamekuwa wakifanya siasa ndani solo badala ya kufanya biashara hiyo ili kuondoa hilo ameamuru kuwa bendera zote zishushwe.
"Hapa siangalii bendera ya chama gani zote zinatakiwa kushushwa haraka iwezekavyo ili kuwafanya wanunuzi kufika sokoni na kununua mahitaji yao muhimu bila kuwepo kwa bendera za vyama maana ukiingia pale sokoni ni mabendera tu hadi yamekuwa kero sasa lazima zitoke zote"alisema Makoga
Aidha Makoga aliwataka wananchi wa halmashauri ya mji wa Mafinga kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuendelea kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli kwa anavyoiongozi nchi hii.
Makoga alisema kuwa ukiwafuata sana vitu vya wanasiasa maendeleo ya halmashauri ya mji wa Mafinga yatachelewa na hayataendana na kasi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo agizo langu linatakiwa kufuatwa Mara moja na hakuna mtu wa kulipinga agizo hili.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Boma ambaye pia ndio Mwenyekiti wa soko hilo Jurist Paulo   kuwa hawezi kushusha bendera za chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa kuwa anahaki ya kuendelea kuipeperusha bendera hizo kwani yeye ndio kiongozi wa Kata hiyo.
"Huyo Mwenyekiti Makoga anaongea vitu ambavyo haviwezi kutekelezeka mimi na wanachama wa chama cha CHADEMA Jimbo la Mafinga Mjini hatuwezi kushusha bendera zetu,halafu bahati mbaya tunaongozwa na kiongozi ambaye hafikirii maamuzi yake Mimi ndio Rais wa Kata hii ya boma pamoja na hili soko lipo chini yangu narudia kusema sishushi bendera"alisema Kisoma
Kisoma aliongeza kwa kusema kuwa Mwenyekiti wa halmashauri anatakiwa kujitathimini juu ya uwezo wake wa kuongoza halmashauri hii maana anaongoza kama halmashauri hii ni ya chama kimoja wakati wapinzani tupo.
"Mimi siwezi kuburuzwa hovyo kwa vitu navyovijua,maana hata ukiangalia kila siku mapato yanashuka kutokana na uongozi usiokuwa wa kuridhisha bila jitihada za mbunge Cosato Chumi halmashauri hii ingekuwa chini kimaendeleo kwa kweli niwe muwazi huyu Mbunge anafanya kazi kweli na kazi inaonekana lakini kuna baadhi vitu anaangushwa na huyu Mwenyekiti Makoga" alisema Kisoma

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More