Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akikagua gwalide la vijana wa JKT kama mgeni wa Heshima.
Vijana wa JKT wanaohitimu mafunzo ya awali, wakipita mbele ya Mgeni wa heshima kutoa heshima ya kijeshi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa. Riziki Shemdoe,
akipokea heshima ya kijeshi Mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za kambi
ya 841 Mafinga kushiriki maafali hayo.
Na Ofisa Habari Mufindi
Serikali Wilayani Mufindi, amewataka
vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kujitolea ya Jeshi la kujenga Taifa JKT
kikosi cha 841 Mafinga, kuwa walinzi namba moja wa amani katika jamii zao, kwa
kuwafichua waharifu watakao jaribu kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini
kwa sasa
Rai hiyo imetolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, wakati akifunga mafunzo ya awali ya
kijeshi kwa vijana waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa
kutoka kikosi cha 841 kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.
“ kwa
siku za hivi karibuni kumekuwa na maadui wa nje na ndani ya nchi wanaojaribu
kuvunja Amani na utulivu uliostawi kwa muda mrefu hapa nchini, hivyo, nawaagiza
Mkalinde
kiapo chenu cha utii na uadilifu
kwa Taifa na Mkuu wa nchi kwa kutekeleza sera ya Taifa inayotanabaisha
kuwa kila raia wa Tanzania ni Mlinzi wa
nchi yake”
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya
amewaasa vijana watakao pata fursa ya kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama
mara baada ya kuhitimu mafunzo, wakafanye kazi kwa nidhamu, uadilifu na
uaminifu na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuajiri vijana wa JKT pekee
kwenye sekta zote zinazohusika na ulinzi na usalama wa nchi.
Jumla ya vijana (846)
wavulana wakiwa (612 ) na wasichana (234) wenye elimu za Msingi mpaka chuo kikuu,
wamehitumu mafunzo ya awali ya kijeshi ya miezi (06) na kufuzu kuingia hatua ya
pili ya mafunzo ya Malezi na stadi za kazi katika Jeshi la kujenga Taifa JKT.
0 comments:
Post a Comment