Mbunge
wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu jana alishikiliwa kwa muda polisi baada
ya kutokea vurugu katika kikao cha kamati ya siasa ya chama hicho.
Dk
Nagu aliyewahi kuwa waziri katika wizara kadhaa wakati wa utawala wa
Serikali za awamu mbili zilizopita, alishikiliwa kwa muda na kuachiwa
baada ya kuhojiwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Masawe alisema Dk Nagu alifikishwa
kituoni kutokana na vurugu zilizoibuka kwenye kikao cha kamati ya siasa
ya CCM Wilaya ya Hanang baada ya makundi mawili kujitokeza.
Masawe
alisema baada ya mahojiano kufanyika na kuandika maelezo, kwa kuwa
mgogoro huo ulikuwa ni mambo ya ndani ya CCM walimwachia.
"Taarifa ambazo nimepata ameachiwa baada ya kuandika maelezo na tayari walifikia makubaliano wenyewe," alisema.
Awali, mkuu wa wilaya hiyo, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya, Sara Msafiri alisema: "Ni kweli amekamatwa lakini nipo kwenye kikao siwezi kuzungumza.”
Habari
kutoka ndani ya kikao hicho, zimeeleza Dk Nagu alikamatwa kutokana na
malumbano ya kupitisha wagombea wa uchaguzi ndani ya CCM.
0 comments:
Post a Comment