Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William akipeana makono na mmoja katia ya wachungaji walioambatana na Mkuu wa jimbo.
Mkuu wa jimbo la Mufindi mchungaji Antoni Kipangula akiwa amemkabidhi fedha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William.
Kanisa
la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) jimbo la Mufindi limekabidhi zaidi ya shilingi milioni 02 kwa Mkuu wa wilaya ya
Mufindi ikiwa ni sadaka maalum iliyotolewa na waumini wa kanisa hilo kwa
wahanga wa janga la tetemeko la ardhi lililotokea
Mkoani Kagera mnamo septemba 13 mwaka huu.
Taarifa
ya kitengo cha habari na mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa
vyombo vya habari, emeeleza kuwa, msaada huo wenye jumla ya shilingi milioni 02 laki 02 na 52 elfu, umewasilishwa
na mkuu wa jimbo la Mufindi mchungaji ANTONI KIPANGULA wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya mkuu wa Wilaya Bomani mjini Mafinga.
Mchungaji
KIPANGULA amesema wakati wa mkutano wao wa jimbo ulioketi mapema mwezi oktoba, kwa kauli moja
walikubaliana kutoa sadaka maalum kwa lengo la kusaidia wahanga wa
janga hilo kubwa na lakihistoria hapa nchini.
Akitoa
shukrani mara baada ya kupokea misaada hiyo kwa niaba ya serikali, Mkuu wa
wilaya ya Mufindi Jamhuri William, amewashukuru waumini wote waliojitoa kwa
sadaka hiyo maalum kwa ajili ya waathirika wa Kagera na kuahidi kuikabidhi kwa
Mkuu wa Mkoa, kisha akaziomba taasisi za dini ziendelee kuisadia serikali na
jamii kwa ujumla katika masuala mbalimbali ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment