Mchambuzi wa maswala ya
jamii na siasa nchini Tanzania Mathias Canal (Picha na David Mtengile)
Na Mathias Canal
Katika
sehemu ya maelezo yake Raisi wa 16 wa Marekani Bw Abraham Lincoln namnukuu
aliwahi kusema kuwa Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni
sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya
masuala ya umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina
maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile katika
chaguzi.
Kabla sijaanza kuzungumzia
uchaguzi wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Tutazame Mwongozo wa kumteua muaniaji Urais
nchini Marekani Kabla ya Wamarekani kuamua nani
wanayemtaka awe rais ajaye, wao kwanza huteua nani atakayewania kiti hicho.
Mchakato huo hungo'oa nanga kwa
mchujo wa kamati za wajumbe ambapo wananchi hupata fursa ya kumchagua muaniaji
kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic au kile cha Republican.Mshindi wa mchujo huo huwakusanya
wajumbe - hawa ni wanachama wenye nguvu ya kupiga kura kumchagua mgombea katika
mikutano ya chama.
Nchini Marekani inakumbukwa kuwa kulikuwa na
upinzania mkali katika uchaguzi wa nafasi ya Rais kati ya vyama viwili ambapo
ni Republican na Demokratic, Kwa upande wa Democrats upinzani mkali ulikuwa
kati ya Hillary Clinton na Seneta Bernie Sanders ambaye alionekana nae kupata
uungwaji mkono zaidi dhidi ya Clinton. Kwa upande wa Republican kulikuwa na
wagombea kama Marco Rubio na Ted Cruz sambamba na Donard Trump aliyeibuka kuwa
mshindi wa chama hicho na mshindi wa nafasi ya Urais wa Marekani.
Tutakubaliana wote kwa pamoja kwamba Vyama
vyote nchini Marekani vilisimamisha wagombea katika kura za awali kabisa ambao
wote kwa pamoja walipigiwa kura na wajumbe wao hapakuwa na kura za Ndio na
Hapana kwa maana ya Kivuli/Jiwe na Mtu sasa tutazame mchakato ulivyo kuwa
kwenye vyama vinavyounda umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA vikiongozwa na Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jinsi vilivyompata mgombea wake wa Urais.
Julai
30, 2015 nikiwa natazama Luninga majira ya saa tatu na dakika moja usiku niliona
katika kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na chombo cha habari cha BBC kupitia
Televisheni ya Star Tv kikiarifu kuwa WANACHAMA wapya wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa pamoja na na Juma Duni Haji wamepitishwa
katika Mkutano Mkuu wa chama hicho kugombea ngazi ya urais na umakamu wa rais
kwa asilimia 99.3 ambapo jumla ya wajumbe 2021 kati ya 2035 waliotakiwa kuhudhuria
kwenye mkutano huo, walipiga kura za NDIO kwa kuwa hapakuwa na wagombea
wemngine na kuibua kishindo katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa
Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Awali kabla
ya kufanyika uchaguzi huu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Freeman Alikael Mbowe
Akizungumzia utaratibu wa kuteua mgombea huyo alisema kuwa, kwa mujibu wa
katiba hiyo kifungu namba 7.16, mgombea urais pamoja na makamu wake wanateuliwa
na sio kupigiwa kura.
Yaani
kama kuna mtu hakuelewa vyema hapo katika maelezo hayo naomba nimsaidie kwa
hili naamini ataelewa vyema zaidi Mbowe alisema kuwa kwa mujibu wa katika huku
akitaja kifungu Mgombea Urais hapigiwi kura na wajumbe bali anateuliwa. Hii ni
kauli ya kishujaa nay a ubakaji wa Demokrasia kwa uwazi kabisa.
Tujikumbushe
Demokrasia ni nini kabla ya kuendelea na mjadala ili tuende sawa: Utawala
wowote wa Demokrasia ni ule unaotokana na ridhaa ya wananchi, ambao kutokana na
utaratibu waliojiwekea hufanya maamuzi ya kuwapata viongozi wao. Wananchi
hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja
kwenye chaguzi. Tukubaliane sasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA hakuna Demokrasi kama ambavyo inahubiriwa katika vijiwe na majukwaa ya kisiasa.
Na kama demokrasia ni pamoja na kushirikisha wananchi kufanya maamuzi kwa nini
Mbowe aliamua yeye kwamba Lowassa na Duni wateuliwe sio kupigiwa kura na wajumbe
zaidi ya 2000, kwa akili ya kawaida tu na karne hii unaweza kuwaambia watu
fanyeni maamuzi kati ya Jiwe/kivuli na mtu...? Lakini katika hili sikuwaona
vijana wa CHADEMA wakihoji wala wale wa Umoja wa Kizazi cha Kuhoji (UTG)
wakihoji. Huenda walipitiwa hawakuliona hili sasa tuendelee.
UCHAGUZI KANDA YA NYASA
Kwa
kunukuu gazeti la Rai linalochapishwa na KAMPUNI ya New Habari (2006) Ltd ambayo
pia inachapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba na The African, la
Disemba 8, 2016 liliandika habari ilikuwa na kichwa cha habari kilichosema
UCHAGUZI CHADEMA NI ‘VITA’ KALI
‘NI vita’, hivyo ndivyo tafsiri inapatikana
kufuatia mvutano mkali ulioibuka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kati ya Mchungaji Peter Msigwa na Patrick Ole Sosopi ambao walikuwa
wanapambana kuwania nafasi ya uenyekiti kanda ya Nyasa.
Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini alipamba
na kijana Machachari katika Siasa za Tanzania Patrick Ole Sosopi ambaye ni
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), kuwania Kanda hiyo
ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa,
Njombe na Songwe.
Tangu maandalizi ya uchaguzi kanda nane za
Chadema yalipoanza mwezi uliopita kulikuwapo na majibizano kati ya wafuasi wa
wagombea hao wawili ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakitumia
mitandao ya kijamii kuanika madhaifu ya kila mgombea.
Hata hivyo, Msigwa alionekana kushambuliwa
zaidi na wafuasi wa Chadema Kanda ya Nyasa kutokana na madai mbalimbali ikiwamo
tabia ya kutoshirikiana na wabunge wenzake katika kukijenga chama, pia kujiweka
mbali na wabunge wa chama hicho kipindi walipokuwa wakipambana kutetea madai
yao kwa Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti la
RAI zinaeleza kuwa baadhi ya wabunge na viongozi wa chama hicho walionekana
kusita kumuunga mkono Mbunge huyo kutokana na madai ya ubinafsi aliouonyesha
katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kwa kushindwa kushirikiana na
makada wa chama hicho kuzunguka sehemu mbalimbali.
Hata hivyo baadhi ya wafuasi wa Ole Sosopi
walionekana kulalamika kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mmoja wao
alisema: “Nimeshangaa sana watu kunifuata inbox na kunitukana hata wengine
kutumia lugha ambayo si njema. Kumuunga mkono Sosopi ‘it’s just my perception.’
Kwa kuwa nina akili timamu siwezi kujibu matusi kama mlivyofanya “Imeniuma
sana, nimeumia sana. Naomba niliweke wazi hili, Peter Msigwa ni Mbunge wangu,
ni mlezi wangu na sina ugomvi naye. Sosopi na Msigwa wote ni Chadema na wote ni
familia moja ndani ya chama chetu Chadema,”
SIKU
YA UCHAGUZI WA KANDA YA NYASA
Tarehe Disemba 22, 2016 ndio siku ambayo
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilifanya uchaguzi huo lakini mapema
asubuhi kabla ya kuanza kwa uchaguzi jina la Patrick Ole Sosopi liliondolewa katika
kinyang’anyiro cha kugombeanafasi ya uenyekiti Kanda ya Nyasa na Uongozi wa Kamati
kuu ya Chama hicho iliyokuwa inaongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman
Alkael Mbowe.
Sosopi alipewa taarifa kwa njia yam domo kwamba
jina lake limetolewa pasina kupewa hata maelezo kwa njia ya maandishi lakini
pia taarifa hiyo alipewa asubuhi siku ya uchaguzi sio siku moja ama mbili kabla
ya uchaguzi
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambaye kwa
sasa ni katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Hamphrey Polepole aliwahi kusema
kuwa Huu si wakati wa siasa za kutafuta uongozi; Ni wakati wa siasa za
maendeleo na kujenga nchi hapo alikubaliana na dhana ya mfumo wa kupunguza
madaraka kwa viongozi inayohubiriwa naserikali ya wamu ya tano chini ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kuwataka viongozi
kuwa na cheo kimoja serikalini ikibidi kuwa na cheo kimoja pia kwenye chama cha
siasa isiwe zaidi ya hapo.
Kabla ya kuendelea naomba nikurejeshe katika
kauli ya Mchungaji Peter Msigwa ya Mwaka 2015 aliyoisema kwamba “Raisi
apunguziwe madaraka, na wakuu wa mikoa pia wana vyeo vingi sana
wapunguziwe" by peter msigwa 2015.
Lakini tutazame sasa vyeo alivyonavyo
mchungaji Msigwa kwenye chama na seriakli kabla ya kutazama uchaguzi wa
Mwenyekiti Kanda ya Nyasa ulivyoendeshwa
Mchungaji Msigwa ni Mbunge wa Jimbo la Iringa
Mjini
Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema
Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Baraza kuu Chadema
Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema
Mchungaji Msigwa ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa
Mchungaji Msigwa ni Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa
Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema
Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Baraza kuu Chadema
Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema
Mchungaji Msigwa ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa
Mchungaji Msigwa ni Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa
Mchungaji Peter Simion Msigwa amekipata cheo cha sita ndani
ya Chadema na kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa baada ya wagombea wengine
kuenguliwa, hivyo kuwa mgombea Pekee ambaye ni yeye Msigwa na Mgombea mwingine
ambaye ni Jiwe/kivuli. Binafsi najiuliza sana lakini najiuliza kimya kimya hivi
vikao vya vyeo hivyo vyote vya watu sita anahudhuriaje!
Maana ya upatikanaji wa Mchungaji Msigwa kama
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa ni kwa njia ya kuteuliwa na sio
kuchaguliwa lakini Demokrasia ambayo CHADEMA huihubiri ni wazi wamekuwa
wakiivunja wao maana wanawanyima nafasi wagombea pendwa na kukata majina yao na
hatimaye wanakubali mgombea mmoja ashindane na kivuli pamoja na kwamba
hakubaliki.
UCHAGUZI
WA CHADEMA KANDA YA NYASA ULIKUWAJE BAADA YA MSIGWA KUBAKI MGOMBEA PEKEE
AKISHINDANA NA KIVULI CHAKE MWENYEWE
Kwa mujibu wa andiko la lililosomeka kama “NIMEAMINI MAISHA BILA UNAFIKI HAYAENDI”
lililoandikwa na Mwalimu Pasaka Rucho mara
baada ya mchakato mzima wa kumalizika na mshindi kutangazwa. Umeeleza tangu mchakato
kuanza wajumbe walitaharuki sana kusikia taarifa ya kutolewa kwa jina la sosopi,
tazama mchakato ulivyokuwa:
Wajumbe halali ni 98
Waliosusia 28
Waliopiga kura ni 106
Kura za ndio kwa msigwa 62
Kura za hapana ambazo zilipigia kivuli cha mgombea ni 44
Waliosusia 28
Waliopiga kura ni 106
Kura za ndio kwa msigwa 62
Kura za hapana ambazo zilipigia kivuli cha mgombea ni 44
Hii ikiwa na maana Ukichukua Kura 44 za
Hapana dhidi ya Msigwa + na kura 28 za wajumbe waliosusia uchaguzi jumla yake
ni =72 hivyo Sosospi tayari kama alikuwa mshindani alikuwa amejihakikishia
ushindi kwa kura 78.
Kura zilizoongezeka kwa zile zilizopigwa ni 8
maana wapiga kura waliongezeka kutoka wapiga kura halali 98 na kuwa na wapiga
kura wasio halali 8 waliofanya idadi kuongezeka na kuwa na wapiga kura 106.
Wajumbe waliopaswa kubaki ndani ukiondo
waliokuwa wamekataa kuingia ndani ni 70
98-28=70.
98-28=70.
Kwa maana halisi ni kwamba kulikuwa na wapiga
kura 36 walioletwa na kuwa wajumbe wasio halali maana baada ya kura 44 za
Hapana na wajumbe 28 kutoka ukumbini hivyo kulipaswa kupatikana kura za halali
28 ambazo ndizo kura za Ndio kwa Msigwa.
Hii inamaanisha kwamba katika hali ya kawaida
hata kama wajumbe wale 28 wasingeingia kama walivyofanya Msigwa angeshinda kwa
kura 26 tu kwa maana ya wajumbe waliopaswa kubaki ndani 70- wajumbe 44
waliomkutaa=26 ambayo ndio idadi ya kura za Msigwa katika uchaguzi huo.
kwa ufupi kwa kutumia wajumbe halali katika
uchaguzi kama Sosospi asingetolewa uchaguzi ungemalizika hivi:
Sosopi 72 (73.5%)
Msigwa 26 (26.5%)
Sosopi 72 (73.5%)
Msigwa 26 (26.5%)
HITIMISHO
Nianze kwa
kumnukuu Dkt Benson Bana wa Chuo Kikuu
cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa alipokuwa akizungumza
katika mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi. Alisema
pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na
utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na
aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya
siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.
Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa
na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya
siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa
kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa
na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Hata hivyo
mara kadha amesema kuwa ili nchi yetu iweze kupiga hatua ni dhahiri lazima kuwe
na Upinzani imara unaochukia Rushwa, na Uminyaji wa Demokrasia.
Binafsi sasa nakitoa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika Ukuzaji wa Demokrasi kwa kauli ya Mbowe
kwa kusema kuwa Mgombea Urais hachaguliwi bali anateuliwa jambo ambalo
ameliongoza pia kwa kumteua Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Mchungaji Msigwa
badala ya kuruhusu wajumbe kugombea na kuchagua kiongozi wanaomtaka.
TANZANIA ina vyama vya siasa 21 vyenye
usajili wa kudumu huku kikiwepo kimoja ambacho kina usajili wa muda. Vyama hivi
vimepatikana baada ya mabadiliko madogo ya Katiba yaliyotoa fursa ya kurejesha
mfumo wa vyama vingi katika nchi yetu mwaka 1992.
Kufuatia mabadiliko haya, Chama cha Mapinduzi
(CCM) ndicho kilichokuwa cha kwanza kupata usajili wa kudumu mwaka 1992, huku
kikifuatiwa na vyama vipya vya CUF, CHADEMA,UMD, NCCR, NLD, UPDP, NRA, TADEA NA
TLP vilivyopata usajili wa kudumu mwaka 1993.
Vyama vingine na usajili wao kwenye mabano
ni: UDP (1994), Demokrasia Makini (2001), CHAUSTA (2001), DP (2002),
APPT(2003), Jahazi Asilia (2004), SAU (2005), AFP (2009), CCK (2012), ADC
(2012), CHAUMMA (2013) na ACT (2014). RNP ni chama pekee kilichopo katika
orodha ya vyama visivyo na usajili wa kudumu.
Katika vyama vyote hivi 21 mpaka sasa ni
CHADEMA pekee ndicho kisichokuwa na Demokrasi kama ambavyo nimebainisha katika
maeneo kadha wa kadha katika andiko langu.
Mwandishi Henry Mwangonde Aprili 23, 2014
katika gazeti la The Citizen, alimnukuu Dk. Benson Banna Katika makala yake ya
“Vyama vingi vimeisaidia Tanzania” na kuandika; “vyama vya siasa nchini
Tanzania havina nguvu katika kutanua mianya ya demokrasia kutokana na kukosa
sera nzuri, mikakati pamoja na tabia ya viongozi wa vyama hivi kutokutumia
mtaji wa wanachama wao kuviendeleza badala yake kuwatumia kwa masilahi
binafsi.” Kwa mujibu wa Dkt Bana katika makala hiyo; vyama hivi vimeshindwa
kutanua miaya ya demokrasia kwa kuwa havina demokrasia ndani yake.
Ni aibu kubwa sana kwa CHADEMA chama
kinachojificha katika Mwamvuli wa Demokrasia katika Karne hii ya 21 kusimamisha
mgombea Kivuli/Jiwe na Mtu…! Na bado kivuli kinapata kura 44? Watu 28 wanaishia
mitini? Mtu anapata kura 66 naye anarudi kumsimulia Mkewe na Watoto kwamba
ameshinda uchaguzi.
Sasa hapa wachambuzi na wajuzi wa Siasa
watahoji Tofauti ya CHADEMA na Yule mtu waliompa umaarufu kwa kumuita Bwana Yule
upo wapi…? Lakini nimkumbushe Msigwa na CHADEMA kuwa raha na uzuri wa kura za
Ndio na Hapana ni pale amabapo mshindi anaibuka kidedea kwa kura nyingi sio
unapata kura 62 wakati zinakukataa ni kura 44 huku kura zingine 28 zikisusia
namna ya Demokrasia ndani ya Chama.
Wakati vyama Vingine nchini vikiwa vinasonga
mbele katika kuimarisha chaguzi zao za ndani ya Chama lakini CHADEMA wao
wanarudi nyuma na kutoa mwanya kwa vyama vyenzake kusonga mbele.Naitazama CHADEMA
kuanguka Kama umaarufu wa NCCR Mageuzi mwaka 1995.
Nitafurahi sana kuona na kusikia kauli za vijana mbalimbali wa CHADEMA wakiwemo UTG wakihoji kuhusiana na Uminyaji wa Demokrasia ndani ya chao chao CHADEMA ili tuzijue rangi zao katika kuhoji na kujenga hoja.
Mwandishi wa Makala haya ni Mathias Canal, Mchambuzi wa maswala ya
jamii na siasa nchini Tanzania, Anapatikana kwa Barua Pepe ya canalmathias@gmail.com na kwa simu
namba 0756413465
0 comments:
Post a Comment