WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuita Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho,
Bw. Hassan Jarufo ili aje amueleze ni kwa nini wakulima wa zao hilo
wanacheleweshewa malipo yao kinyume na maagizo ya Serikali.
Ametoa
kauli hiyo jana mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa
mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu
ndogo wilayani Nachingwea. Waziri Mkuu amewasili wilayani Nachingwea
akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
“Niliagiza
wanunuzi waje na bond (dhamana ya mauzo), waziweke benki ndipo
waingizwe kwenye mnada. Kwa maana hiyo mnada ukimalizika, benki inakata
fedha husika na kuingiza kwenye chama cha wakulima.”
“Hapa
tatizo ni kwamba hatukusimamia vizuri zuala hili. Tulipaswa
tujiridhishishe kwanza kama mnunuzi amelipa fedha benki. Tatizo la
biashara hii watu wengi ni madalali, wanaangalia hali ikoje na wakibaini
kuna cha juu, ndiyo anaagiza na kuamua kuja kulipa. Kama angekuwa
amelipa benki, ile hela ya awali ingekatwa katika fedha ya dhamana
aliyokwishaitoa,” alisisitiza.
Oktoba
16, 2016 wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani Nachingwea, mkoani Lindi,
Waziri Mkuu alisema alishatoa maelekezo tangu Aprili, mwaka huu kwamba
wanunuzi wa korosho ni lazima watoe asilimia 25 ya malipo wanayotaka ili
kuepuka tatizo la madalali kuingilia kati biashara hiyo.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey
Zambi na Wakuu wote wa wilaya za mkoa huo wawahimize wakulima wapande
miche mipya ya korosho kwa sababu mikorosho iliyopo imezeeka na haitoi
mazao ya kutosha.
“Mnatakiwa
muwahimize wananchi wapande miche mipya mara tu mvua zitakapoanza ili
ianze kukua wakati wakusubiria kung’oa ile ya zamani. Nimeambiwa korosho
bora hazipaswi kuzidi punje 190 ili zijae kwenye kilo moja. Ubora wa
miti ya korosho ukishuka na idadi ya punje pia inapungua,” alisema.
Alisema
kigezo kikuu cha ununuzi wa korosho hivi sasa ni idadi ya punje na kwa
Ruangwa na Nachingwea, idadi inakuwa kubwa kwa sababu punje zake ni
ndogo. “Wenzetu wa Tandahimba walipanda miche mipya tangu miaka minne
iliyopita kwa hiyo sasa hivi wanavuna korosho zenye ubora,” ameongeza.
Alimpongeza
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba kwa uamuzi wake
wa kuvunja mfuko wa wakfu wa korosho (CIDTF) na akamtaka afute mifuko
kama hiyo kwenye mazao mengine kama katani, chai na kahawa kwani
inafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na bodi za mazao hayo.
“Waziri
Tizeba alishaanza na zao la pamba, sasa aende kwenye mazao mengine ili
fedha ambazo watu wa mfuko huu walikuwa wakizitumia kulipana posho tu,
sasa ziende kwenye bodi kuhamasisha wakulima walime zaidi na ikibidi
wapewe hata mashine za kupulizia dawa,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment