Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akicheza pamoja na wakuu wake wa wilaya za mkoa wa Iringa kabla ya kupokea mwenge |
MWENGE wa uhuru waanza mbio zake mkoani Iringa leo kwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya kimaendeleo 43 yenye thamani ya zaidi ya Tsh bilioni 25 .4
Huku kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa George Mbijima akiwashukia baadhi ya watu wanaopinga mbio hizo za mwenge wa Uhuru kuwa hawapo sawa na wanapaswa kupelekwa milembe kuchunguzwa utashi wao. Akipokea mwenge wa uhuru kutoka mkoa wa Njombe jana mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza alisema kuwa ujumbe wa mbio za mwenge wa Uhuru ni Vijana nguvu kazi yua taifa washirikishwe na wawezeshwe .
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa uwezeshaji wa vijana kushiriki katika maendeleo ya mkoa huo umekuwa ukipewa kipaumbele zaidi ikiwa ni pamoja na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbali mbali zinazokwamisha vijana kujiajiri na kuajiriwa ndani ya mkoa na taifa .
“ mkoa umekuwa ukitekeleza mikakati mbali mbali ikiwemo ya kutenga maeneo kwa ajili ya vijana na mfano Mufindi imetenga maeneo kwa ajili ya vijana ardhi yenye ukumbwa wa hekta 870, Iringa Hekta 79 ,Kilolo Hekta 192 na Iringa Manispaa imetenga maeneo 12 huku mji Mafinga eneo moja “
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwaunganisha vijana na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mikopo yenye riba ndogo na masharti nafuu pia kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana katika kutoa elimu ya ujasiliamali ,stadi za kazi na stadi za maisha
Pia kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Tsh 942,952 ,622 kwa vijana asilimia tano waliopo mkoani hapa kupitia fedha za makusanyo ya ndani kwenye halmashauri ambazo ni fedha zilizotengwa kwa mwaka wa fedha 2016 na 2017.
Hata hivyo alisema mkoa umejipanga na tayari umeanzisha skim za umwagiliaji ili kufanya kilimo chenye tija na kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia kilimo kisichotegemea mvua .
Akizungumzia juu ya mapambano dhidi ya rushwa alisema kuwa kwa mwaka 2015 /2016 mkoa umetoa elimu ya mapambano ya Rushwa kwa wananchi 22,402 wakiwemo wanafunzi 11,838 na kuendesha semina 101 na mikutano 53 na kuwa jumla ya taarifa 132 zimepokelewa kati ya mwaka 2015 na 2016 huku taarifa 41 zilifunguliwa majalada kwa ajili ya uchunguzi wa taarifa za rushwa na kesi 21 ziliweza kufunguliwa Mahakamani ambapo kesi 6 zilitolewa hukumu .
Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mkoa wa Iringa umeendelea na jitihada za kupunguza makosa yatokanayo na madawa ya kulevya kwa asilimia 32.72 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwa kutoka asilimia 89 kwa mwezi janjuari hadi Mei 2015 kwa kufikia 49 kwa kipindi cha januari hadi Mei 2016 huku kiwango cha dawa za kulevya kimepungua kutoka kilo 506.5 kwa Januari hadi Mei 2015 hadi kufikia kilo 13.9 kwa januari hadi mei 2016.
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw Mbijima aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Iringa kwa kuchangia mkiradi ya Mwenge kwani alisema kuwa miradi hiyo ni fahari kwa mkoa na Taifa katika kuwakomboa wananchi wa mkoa huo.
Bw Mbijima alisema kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihamasisha jamii kuchukia mwenge wa Uhuru jambo ambalo ni ukosefu wa uzalendo kwa Taifa na kuwa baadhi ya nchi ulimwenguni zimekuwa zikitamani kuiga kukimbiza mwenge lakini zinashindwa .
Alisema Tanzania imekuwa ni mfano kwa mataifa mengine katika ukimbizaji wa mwenge wa uhuru na baadhi ya nchi zimeishika njiani katika kukimbiza mwenge wa uhuru hivyo kuwataka wananchi kuendelea kupenda mwenge wa Uhuru na kuwapuuza wanaobeza mwenge wa uhuru na kuwataka wapelekwe milembe ambako ni Hospitali ya vichaa kuchunguzwa akili zao.
0 comments:
Post a Comment