Ni Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe
Asumpta Mshama akihutubia wananchi wakati wa sherehe za siku ya mazingira
duniani, katika kijiji cha Lugodalutali, wilaya ya Mufindi
LEAT yagawa vitabu na vipeperushi vinavyotoa elimu ya mazingira na maliasili
na fredy mgunda,iringa
Timu ya
Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) imewaasa wananchi kushiriki
kikamilifu katika usimamizi wa mazingira na maliasili na kuzitaka mamlaka za
usimamizi wa mazingira na maliasili kutimiza wajibu wao kwakuwa serikali
imewaamini na kuwapa jukumu hilo.
Akizungumza na
wananchi wa wilaya ya Mufindi katika maadhimisho ya siku ya mazingira
iliyofanyika katika kijiji cha Lugoda Lutali wilayani Mufindi mkoani Iringa Afisa
Mawasiliano wa LEAT Miriam Mshana ,alisema kuwa uharibifu wa mazingira
umechangiwa kwa sehemu kubwa na shughuli za binadamu ikiwa ni pamoja na ukataji
miti ovyo bila kupata vibali na uvunaji haramu wa wanyamapori, usio rafiki
kiuchumi na kimazingira.
Mshana alisema, uvunaji wa kasi hasa wa misitu
umeathiri na kuchangia mabadiliko ya tabia nchi, kuiweka nchi katika hatari ya
kuwa jangwa. Uvunaji haramu wa wanyamapori hususan tembo umeipa hasara taifa.
‘’’’Kwa mujibu wa ripoti ya Mtaalam Mashuhuri
wa tafiti za tembo duniani, Ian Douglas Hamilton, kwa mara ya kwanza mwaka 1976
alifanya utafiti wa angani, Tanzania kwa ujumla ilikuwa na tembo 316,000,
ambayo ilikuwa idadi kubwa sana ikilinganishwa na maeneo mengine
duniani’’’’’alisema mshana
Kwakufanya hivyo
tutakuwa tunaitikia wito wa kaulimbiu ya mwaka 2016 ya siku ya mazingira
duniani-‘Shiriki kufanya dunia mahali pazuri’.
Jowika Ksunga ni
mkuu wa wilaya ya Mufindi nae alisema, Mwaka 1976, mbuga ya Selou pamoja na
maeneo jirani ilikuwa na idadi ya tembo109,000,Utafiti uliofanywa mwaka 2013,
ulibaini kuwa mbuga ya Selou ilikuwa na
tembo 13,084 pekee.
Kasunga alisema takwimu hizo zinaashiria
hatari ya kutoweka kabisa kwa tembo katika nchi yetu na itaathiri biashara ya
utalii ambayo ilikuwa ikitoa mchango mkubwa katika pato la taifa.
‘’’’’’’Maeneo
mengi ya mijini yamechafuliwa kwa utupaji taka ovyo, hivyo kuharibu mandhari ya
miji yetu na kuchangia katika magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na
kipindupindu, alisema Kasuga.
Alisema, utupaji
taka ngumu na zenye sumu karibu na makazi ya watu au vyanzo vya maji, umeleta
athari kubwa kiafya kwakuwa kemikali hizo hupenya ardhini na kudhuru ardhi na
vyanzo vya maji, hasa kwa wananchi wanoishi karibu na viwanda na sehemu za
uchimbaji madini.
“Inasikitisha kuwa wamiliki wa viwanda vingi
na machimbo ya madini wanakiuka sheria ya mazingira lakini pia wameshindwa
kuwajibika kwa jamii zinazo wazunguka ambazo ndio wadau wakubwa wa biashara
zao, kwa kaidi kuchukua hatua za kuzuia uharibifu wa mazingira hata baada ya athari
kutokea”, alisema Jowika’’’’’’’’’
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Asumpta Mshama alisema kuwa
shirika la LEAT limekuwa mstari wa mbele kwa zaidi ya miaka 20, katika
kusimamia mazingira nchini katika sekta ya madini, viwanda, machinjio na
mazingira kwa ujumla.
Asumpta alisema taarifa
ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa mwezi Aprili, 2016 inaonesha
takribani watu milioni 2 hufa kila mwaka duniani na zaidi ya watu bilioni moja
hupatwa na magonjwa yanayo sababishwa na uchafuzi wa mazingira
‘’’’’Iwapo
serikali, wananchi na wamiliki wa viwanda na machimbo ya madini, kila mmoja akitimiza
wajibu wa kutunza mazingira tutakuwa natekeleza haki ya kuishi, haki ya afya
bora na ustawi, kama ambavyo serikali ilivyo ridhia katika mikataba mbalimbali
ya kimataifa ikiwemo mkataba wa Stockholm nchini Sweden na Rio De janeiro nchini Brazil’’’’’’’’alisema
Asumpta
0 comments:
Post a Comment