skip to main |
skip to sidebar
Thursday, June 30, 2016
mwangaza wa hbari
No comments
SERIKALI ya mkoa wa Iringa imetekeleza agizo la Rais Dr John Magufuli kwa kukabidhi jumla ya madawati 21,304
kwa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri zote tano za mkoa huo .
Mkuu wa mkoa wa Iringa
Bi Amina Masenza akikabidhi mgao wa madawati hayo kwa wakurugenzi wa Halmashauri hizo leo zoezi lililofanyika
kwenye karakana na chuo cha ufundi stadi VETA , alisema kuwa utekelezaji wa agizo hilo umefanikiwa kutokana na mwitikio mzuri wa wananchi wa mkoa huo na wadau mbali mbali wa maendeleo ambao kwa umoja wao
wamesaidia zoezi hilo kukamilika
.
Alisema kuwa Rais Dr Magufuli alitoa agizo kwa wakuu wote
wa mikoa nchini
kuhakikisha wanafunzi wote wanakaa katika
madawati ifikapo leo Juni 30 mwaka huu
na kutokana na agizo
hilo alilazimika kuwashirikisha wakuu wake wa wilaya na wadau
mbali mbali wakiwemo wananchi mmoja mmoja na kila mmoja
kwa uwezo wake aliweza kuchangia madawati hadi kufanikisha zoezi hilo.
Mkuu huyo alisema
kwa Halmashauri za mkoa
wa Iringa zimetengeneza
madawati kupitia bajeti zake na wadau waliopo
kwenye Halmashauri husika na hadi
sasa mkoa umeweza kutengeneza madawati hayo 21,304 wakati madawati 8,163 kwa ajili ya shule za msingi huku
madawati 1,264 ya shule za sekondari yanaendelea kutengenezwa katika karakana mbali mbali na fedha kwa ajili ya matengenezo hayo tayari zimelipwa .
Hivyo alisema madawati yanayoendelea
kutengenezwa yanatarajiwa kukamilika
July 15 mwaka huu kwani yamechelewa kukamilika kutokana na wakandarasi
wanaotumika kutengeneza madawati hayo kuwa na kazi nyingi .
Bi
Masenza alisema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbali
mbali imeweza kutengeneza madawati
700 kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Halmashauri za kumaliza tatizo la madawati
mapema ,ambayo yamegawiwa katika
Halmashauri tano za mkoa
wa Iringa ambazo ni Iringa Manispaa
madawati 200, Mji Mafinga madawati
100 ,Halmashauri ya Iringa madawati 100 ,halmashaur i ya Mufindi madawati 100 na Kilolo madawati 100
“Nitumie
fursa hii kuwashukuru wadau mbalimbali,wafanyakazi wa Halmashauri na
wananchi wote walioona umuhimu wa kuchangia upatikanaji wa madawati
haya”alisema Masenza na kuongeza.
“Mchango wao umekuwa na umuhimu katika
kuwaandaa vijana wetu tunapoelekea Taifa lauchumi wa kati ifikapo mwaka
2030,michango yao ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa ziada hiyo,kwani mkoa umetoa
madawati 200 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na madawati 100 kwa
Halmashauri za Kilolo,Iringa,Mji Mafinga na Mufindi”alisema Masenza.
Wakati madawati 308 yanaendelea kutengenezwa katika karakana ya VETA pindi yatakapokamilika yatafikisha idadi ya madawati 1,008 jumla ya fedha ambazo zimetumika kutengeneza madawati hayo 1,008 ni milioni 50,400,000 na baada ya madawati yote kukamilika kutengenezwa mkoa wa Iringa hautakuwa na upungufu wa madawati kwa wanafunzi zaidi ya kuwa na ziada ya madawati .
“Kazi
ya kutengeneza madawati itakapokamilika Shule za Mkoa wa Iringa hazitakuwa na
upungufutena wa madawqati bali zitakuwa na ziadiyamadawati 850 na hiini
kutokana na baadhi ya Halkmashauri kuwa kutengeneza madawati ya zaidi na
mengine niyaleyaliyotolewakutoka Ofisi ya Mkoawa Iringa”alisema Masenza.
Mkoa wa Iringa una jumla ya shule za
msingi 478 na shule za sekondari 107zinazomilikiwa na serikali na mkoa huo ulikuwa
na upungufu wa madawati 29,347 ikiwa ni madawati 26,046 ya shule za
Msingi na madawati 3301 kwa shule
za sekondari.
0 comments:
Post a Comment