Saturday, November 26, 2016

KIKOSI KAZI CHAMALIZA KAZI YA KUANDAA MPANGO KAZI WA MATUMIZI YA ARDHI NA KINATARAJIA KUWASILISHA TAARIFA KWA WAZIRI WA ARDHI MH.LUKUVI


 Kikosi kazi katika mkutano wa siku mbili uliofanyika Morogoro

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania Dr. Stephen Nindi akichangia jambo wakati wa mkutano huo
 Bw.Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano huo
 Bw. Marcely Madubi kutoka Asasi ya kiraia ya Care International  (wa pili kulia) akichangia jambo katika kipengele cha Changamoto na mapendekezo kuhusu upangaji , utekelezaji na usimamizi wa mipango na matumizi ya Ardhi
 Bw. Jamboi Baramayegu kutoka Ujamaa-CORT akichangia jambo juu ya hangamoto na mapendekezo katika uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya Ardhi.
 Bw. Gerald Mwakipesile Afisa  Mipango wa Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi akizungumza juu ya Mpango wa Elimu kwa Umma kuhusu maswala mbalimbali yanayokabili upangaji,utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya Ardhi nchini.
Mratibu wa Mradi wa Ardhi yetu kutoka Asasi ya Kiarai ya Care International Bi. Mary Ndaro akizungumzia jambo juu ya Taasisi zinazojihusisha na Mipango ya matumizi za Ardhi nchini na kusisitiza ushirikiano.
 Bw. Paulo Tarimo ambaye ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo akitolea msisitizo Jambo
Profesa Aldo Lupala ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi na Mkuu wa Kitivo cha Usanifu Majengo Akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa mkutano huo
Mmoja wa washiriki katika Mpango kazi akifafanua jambo
Mwakilishi kutoka Asasi ya Kiraia ya kimataifa Oxfam Naomi Shadrack akichangia jambo wakati wa Mkutano huo.
Profesa Aldo Lupala ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi na Mkuu wa Kitivo cha Usanifu Majengo akipitia kuona kazi zinavyofanyika katika makundi mbali mbali.
Majadiliano katika Makundi Mbalimbali yakiendelea

Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa



Wadau mbalimbali wa Mashirika ya Kiraia na Sekta binafsi kwa kushirikiana na TUME  ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wanatarajia kukabidhi  ripoti  maalum kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi ifikapo Desemba mwaka huu ripoti  hiyo ikiwa ni ya uandaaji wa mpango kazi wa utekelezaji wa Makubaliano ya Mkutano mkuu wa Wadau wa Mipango ya Matumizi ya ardhi nchini .

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Kikosi kazi uliofanyika mkoani Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi  ya Ardhi, Dk Stephen Nindi alisema vitu muhimu katika nchi ambavyo vinasaidia kupunguza kwa  kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ni upangaji wa matumizi bora ya ardhi.

Alitaja vitu ambayo ni miongoni vinavyokwamisha kwenda kwa kasi kwa zoezi la upangaji wa matumizi bora ya ardhi ni pamoja na ufinyu wa bajeti na ukosefu wa teknolojia mpya zinazoweza kupima na kupanga ardhi kwa mwendo wa haraka zaidi.

Aidha Dkt.Nindi alisema Kikosi kazi hicho kilikutana katika mkutano huo kwa lengo la kuandaa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kumfikia Waziri Mh. Lukuvi na kuona ni namna gani nchi nzima  inafanikiwa kuwa na mpango mzuri wa matumizi bora ya ardhi na kuondoa migogoro iliyopo sehemu mbalimbali nchini.

Alisema viongozi wa kitaifa wanapaswa kutambua kwamba ardhi ni suala nyeti  na mtambuka hivyo wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mipango ya matumizi bora ya ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa itaweza kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi inayojitokeza.

"Tunatarajia kufikisha ripoti hii kwa Muheshimiwa Waziri Lukuvi na yeye ataona ni namna gani atakavyowashirikisha Mawaziri tofauti tofauti ambao kwa namna moja au nyingine wanaingia katika suala hili la mpango wa matumizi bora ya ardhi ikiwemo katika sekta ya Madini, Kilimo, Misitu na Mifugo na kuona ni namna gani wataweza kutenga bajeti ambayo itaweza kuingia katika suala hili la matumizi bora ya ardhi,"alisema Nditi

Dkt. Nindi aliongeza kuwa ripoti hiyo itawezesha suala la upangaji  wa matumizi bora ya ardhi linakuwa suala la kitaifa na kuiwezesha  serikali kupanga bajeti itakayofanya mchakato huo wa upimaji na upangaji wa matumizi bora kwenda kwa haraka na kufikia vijiji vingi zaidi.

Naye Mratibu wa Programu ya Mradi ya Ardhi yetu kutoka asasi ya kiraia ya  CARE INTERNATIONAL nchini Tanzania, Bi.Mary Ndaro alisema serikali inapaswa kuweka dhamira kisiasa ya kuweka utayari wa kufanya suala la ardhi kuwa ni kipaumbele na kuongeza bajeti ya fedha katika suala la matumizi ya ardhi.

Alisema  asasi za kiraia zipo tayari kufanya kazi na serikali pamoja na Wizara zinazohusika na  suala la matumizi bora ya ardhi na kuhakikisha mabadiliko yanapatika katika suala hilo

"Tupo tayari kuungana na serikali katika kuhakikisha suala hili linapewa kipaumbe na kupunguza migogoro inayoendelea kujitokeza kwa sasa ya ardhi hivyo sisi tupo tayari kuona  serikali inatoa  mwongozo wake kupitia Wizara zinazohusiana na masuala ya ardhi kwa pamoja tuungane na kushikamana katika kusaidia suala hili linafanikiwa na vijiji vinapangwa na kupimwa kwa matumizi bora ya ardhi," alisema Ndaro.

Pia Bi. Ndaro alisisitiza wananchi kuwa watulivu na kukwepa muingiliano kwani asasi hizi zimejizatiti kusaidia wananchi hivyo rai yangu kwa baadhi ya asasi za kiraia zinazo penda kusaidia mchakato huu ziapaswa kujitokeza kwa wingi ilikuweza kumaliza shughuli hii kwa haraka zaid kwani tukiiachia serikali peke yake haitoweza kumaliza sehemu zote kwa wakati kwani inabajeti ambayo ni ndogo ambayo inaweza kumudu vijiji vitano tu kwa mwaka.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More