Mchakato wa
ndege za Saudi Arabia na Tanzania waanza kusukwa
*Ni matokeo
ya kikao kati ya balozi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu Saudi Arabian Airline
*Vivutio vingi
vya utalii nchini Tanzania vyatajwa kwenye kikao hicho cha aina yake
Balozi wa
Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin
Nasser Al Jasser, katika kikao chao maalum cha kujadili namna ya ndege za shirika hilo kuanza safari za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania. Picha zote kwa Hisani ya Ofisi ya Balozi wa Tanzania Saudi Arabia.
Na Mwandishi
Wetu, Saudi Arabia
WATALII,
wafanyabiashara, mahujaji wa Watanzania pamoja na watu kutoka nchi za Kiarabu
hususan Saudi Arabia, huenda wakapata fursa ya kuwasili Tanzania kwa urahisi
endapo mchakato Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines wa kutoa ndege za
kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania utakapofanikiwa kama ulivyoanza
kushughulikiwa.
Mapema wiki
hii Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza alifanya
mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh
Saleh Bin Nasser Al Jasser, ambapo shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vya
Tanzania vilijadiliwa, kama njia ya kuangalia namna bora ya ndege hizo kufanya
safari zake vizuri kwa kuzingatia mkataba wa ushirikiano wa mambo ya anga baina
ya Tanzania na Saudi Arabia Bilateral Air Service Agreement (BASA).
Balozi wa
Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin
Nasser Al Jasser kushoto.
Kikao kinaendelea kati ya balozi wa
Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin
Nasser Al Jasser kushoto.
Akizungumza
katika kikao hicho, Balozi Mgaza alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio
vingi vya Utalii kama mbuga nzuri za wanyama pamoja na Mlima wa Kilimanjaro
ambao ni alama bora za utalii nchini humo inayochochea wageni wengi kuingia na
kutoka katika nchi hiyo yenye amani na upendo.
Alisema
endapo kutakuwa na ndege za moja kwa moja kutoka Saudi Arabia hadi nchini
Tanzania, Shirika linaweza kutoa huduma bora bora kwa kupitia sekta ya utalii
pamoja na ile ya mahujaji.
“Unapozungumzia
sekta ya utalii, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna vivutio vingi vinavyosisimua,
hivyo naamini kuna kila sababu ya Shirika hili la Ndege kuangalia jinsi ya kuanzisha
safari za moja kwa moja.
“Nchi yetu
imepiga hatua katika sekta mbalimbali na viwanja bora vya ndege vipo katika
hali nzuri, huku tukiamini kuwa endapo wazo hili litafanikiwa nchi yetu
Tanzania itapiga hatua kubwa kwa sababu watu wengi watahamasika kufika kutalii
bila kusahau watakaotaka kuwekeza kwenye mbio za serikali za kuifanya nchi yetu
kuwa nchi ya viwanda,” Alisema Balozi Mgaza.
Kwa sasa
mashirika makubwa yanafanya safari zake kama vile Emirates, Oman Air, Etihad
Airways, Fly Dubai, Qatar Airways, Egypt Air na Turkish Airlines jambo
linalochochea kiu kubwa kwa abiria wa Saudi Arabia na Tanzania wanaopenda
kuingia na kutoka kwenye nchi hizi mbili.
0 comments:
Post a Comment