Viongozi
wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umeitaka
serikali kusitisha zoezi la upigaji wa kura ya maoni ya katiba kutokana
na zoezi hilo kutokidhi vigezo vya kisheria na badala yake ielekeze
nguvu na rasilimali fedha katika zoezi la uandikishaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura ili kuliepusha taifa kuingia katika machafuko.
Viongozi wakuu wa vyama vinavyounda umoja huo wa katiba ya wananchi
ukawa wakiongozwa na Profesa Ibrahimu Lipumba wa chama cha wananchi CUF
na Freeman Mbowe wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, chama
cha NLD Dr Emmanuel Makaidi, chama cha NCCR mageuzi Mosena Nyambabe
wameitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba amemtaka rais Prof Jakaya
Mrisho Kikwete kutoa kauli ya kuusitisha mchakato wa kura za maoni ya
katiba pendekezwa kwa kuwa zoezi hilo kwa sasa haliwezi kutekelezeka
April 30 ya mwaka huu kama rais alivyotangaza licha ya kutokuwa na
mamlaka ya kutangaza tarehe ya kufanyika kwa kura hizo za maoni.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
Chadema Freeman Mbowe ameitaka serikali kuelekeza fedha kidogo zilizopo
katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa
kuwa zoezi hilo linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya
kutosha na kusitisha kabisa zoezi la kura za maoni ya katiba ili
kuiepusha nchi na kile alichodai kuwa ni machafuko yanayowea kuzuilika.
Hivi sasa taifa liko katika maandalizi ya kushiriki katika zoezi la
kura za maoni ya katiba pendekezwa linalotarajiwa kufanyika alhamis ya
April 30, 2015 kama ilivyotangazwa na mh rais wa jamhuri ya mungano wa
Tanzania licha ya uwepo wa kauli za kulipinga zoezi hilo kutoka hasa
katika vyama vya siasa vya upinzania na baadhi ya vyama vya kiraia kwa
sababu kadha wa kadha
0 comments:
Post a Comment