skip to main
|
skip to sidebar
Home
Home
About us
News
National News
International News
Business and Economics News
Sports and Entertainments News
Contact us
Wednesday, February 25, 2015
FFU watumia mabomu kutuliZa vurugu Ilula ,magari yachomwa moto ,mahabusu waachiwa silaha zaporwa
Wednesday, February 25, 2015
mwangaza wa hbari
No comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Askari wa FFU wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu kubwa zilizoibuka leo Kati ya Polisi na wananchi wa mjini wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kufuatia kifo chenye utata cha mwanamke mmoja
Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi Leo na kudumu hadi Majira ya saa 10 jioni huku kituo cha Polisi kikivunjwa ,bunduki kuporwa na nyingine kuchomwa moto pamoja na magari matatu na Pikipiki Moja ya polisi.
Wakielezea tukio hilo wakazi wa mji wa Ilula wameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz kuwa chanzo ni askari watatu watatu akiwemo mkuu wa kituo cha Ilula kwenda kufanya msako wa wananchi wanaokunywa pombe muda wa kazi.
Hivyo kutokana na tukio hilo mwanamke huyo aliyepoteza Maisha aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi aliamua kukimbia kukwepa kukamatwa na Polisi hao Kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la klabu hicho cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Ilala Mjini Ilula akiwa amekufa.
" Polisi hawa kila siku wamekuwa wakifika hapa klabuni na kukamata watu na siku kwanza walimkamata marehemu na kumtoza faini ya Tsh 20,000 na siku ya pili walimkamata yeye na mumewe na kuwatoza faini Tsh 40,000 na leo walikuwa wakija kumkamata tena na hapo ndipo mwanamke huyo aliamua kutimua mbio Kabla ya kukutwa amekufa" alisema shuhuda wa tukio hilo Shida Ngwata.
Huku Mkazi mwingine ambae hakutaka jina lake kutajwa hapa alisema kuwa Polisi hao walilazimika kutumia mabomu na risasi za moto kutokana na umati mkubwa wa watu waliojitokeza huku Moja Kati ya bomu likiokotwa ambalo lilikuwa halijalipuliwa.
Alisema kuwa askari watatu watatu ndio ambao walikuwa wakisakamwa na Raia hao ambao pia wamevunja vioo vya basi la Upendo kufuatia mkuu wa kituo Ilula kukimbilia ndani ya basi hilo wakati akifukuzwa na Raia hao .
Diwani wa kata ya Nyalumbu Ally kikunga alisema kuwa alipigiwa simu na wananchi wake kujulishwa juu na vurugu hizo na Baada ya kufika Eneo la tukio alikuta mwanamke huyo akiwa mahututi ila hakuweza kupata msaada toka kwa wananchi wengine ila kumkimbiza hospitali .
Diwani huyo alilishauri jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu zaidi Kwani alisema Eneo hilo la klabu ni Eneo ambalo pia wananchi wanapata mahitaji mbali mbali na kuwa mwanamke huyo alikuwa akifanya usafi katika chumba chake cha biashara ya pombe.
Hata hivyo alisema Raia hao wameharibu Mali mbali mbali pamoja na nyaraka zote na kuwafungulia mahabusu wote waliokuwemo mahabusu huku Lori Moja lililokamatwa kituoni hapo likilindwa kuharibiwa kuwa halina kosa.
Vurugu hizo zilisababisha wasafiri wanaotumia barabara ya Kuu ya Mikoa ya Nyanda za juu kusini kukwama kwa zaidi ya masaa 6 .
Kaimu mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya kilolo ilifika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kutoa taarifa kamili ya Mali zilizoharibiwa na chanzo halisi cha tukio hilo Baada ya kukaa kikao na viongozi wa jeshi na Polisi na wale wa mji wa Ilula
Japo mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari mawili ya Polisi na Pikipiki yakiwa yamechomwa moto ,gari Moja la askari pia lilichomwa moto na magari mawili Moja la askari na daladala moja na basi la upendo kuharibiwa vibaya
Newer Post
Older Post
Home
0 comments:
Post a Comment
Popular Posts
KENANI KIHONGOSI MWENYEKITI MPYA WA UVCCM MKOANI IRINGA
M wenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi akitangazwa na msimamizi mkuu wa u...
WANAFUNZI WALIOHITIMU DARASA LA SABA 1993 SHULE YA MSINGI NYAKATO JIJINI MWANZA WAIKUMBUKA SHULE YAO.
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi Afisa...
KONGAMANO LA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA UN LAFANA TANGA
Tanga , WANAFUNZI wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa kutoka vyuo Vikuu na Shule za Sekondari na Msingi kutoka Mikoa mbalimbal...
ZIJUE AINA TANO ZA MITUNGI YA KUZIMIA MOTO
1.MTUNGI WA MAJI(WATER) Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingi...
DC IGUNGA HAITIMISHA ZOEZI LA KUPOKEA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH-OFAB
Wakulima wa Kijiji cha Igogo wanaunda Kikundi cha Imala Makoye katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakiwa wameshika mb...
BONANZA LA KWAYA ZA VIJANA KUTOKA SHARIKA MBALIMBALI ZA KANISA LA MORAVIAN JIJINI DAR LAFANA KATIKA VIWANJA VYA NIT
Kikosi cha kwaya ya Usharika wa Mabibo (waliovaa jezi za Dark Blue) na kwaya ya Usharika wa Kinondoni (waliovaa jezi nyekundu) wakiwa kat...
BREAKING NEWS!!!!!! ALBERT CHALAMILA NDIO MWENYEKITI CCM MKOA WA IRINGA
Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila akitoa hotuba yake ya kwanza kuwashukuru wapiga kura ...
PICHA ZA MATUKIO YA KUUNGUA KWA NYUMBA ANAYOKAA KATIBU WA UVCCM ALPHONCE PATRICK MUYINGA
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akizunguza na waandishi wa habari katika eneo latukio ...
WAKURUGENZI MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KUNUA CHAKI ZINAZOZALISHWA MKOANI HUMO
1 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Dkt Rehema Nchimbi akishiriki kazi ya uzalishaji chaki wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Kiwanda...
LIPULI BADO PANAFUKA MOSHI
Abu Changawe Majeki akiongea na waandishi wa habari wa Mkoani iringa juu ya sakata lake la kusimamishwa uenyekiti wa timu ya lipuli B...
Categories
Habari za jamii
Habari zote
Siasa
Videos
Blog Archive
►
2024
(1)
►
March
(1)
►
2023
(1)
►
October
(1)
►
2021
(2)
►
July
(1)
►
June
(1)
►
2018
(249)
►
June
(9)
►
May
(16)
►
April
(36)
►
March
(67)
►
February
(60)
►
January
(61)
►
2017
(1008)
►
December
(81)
►
November
(125)
►
October
(166)
►
September
(80)
►
August
(109)
►
July
(51)
►
June
(37)
►
May
(57)
►
April
(78)
►
March
(89)
►
February
(61)
►
January
(74)
►
2016
(1104)
►
December
(54)
►
November
(47)
►
October
(74)
►
September
(125)
►
August
(88)
►
July
(67)
►
June
(60)
►
May
(72)
►
April
(102)
►
March
(108)
►
February
(152)
►
January
(155)
▼
2015
(410)
►
December
(113)
►
November
(160)
►
October
(89)
►
September
(1)
►
August
(2)
►
July
(6)
►
June
(7)
►
May
(5)
►
April
(4)
►
March
(12)
▼
February
(11)
MTOTO MCHANGA AUAWA NA KUTUPWA KICHAKANI MKOANI MO...
UKAWA WAITAKA SERIKALI KUSITISHA ZOEZI LA UPIGAJI ...
JESHI LA POLISI LAPATA AIBU KUBWA, POLISI WAKE AKU...
SERIKALI ISIMAMIE VYEMA HAKI ZA BINADAMU KWA KUSHI...
FFU watumia mabomu kutuliZa vurugu Ilula ,magari y...
KIJANA WA KITANZANIA AUNDA REDIO STESHENI
WATANZANIA WAASWA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA ...
CHAMA CHA ALBINO KUMSHITAKI RAIS KIKWETE UMOJA WA ...
MTANDAO WA HAKI ZA BINADAMU WATOA TAMKO JUU YA KUT...
TAMWA YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI WA MIKOA YA NYA...
JAY Z NA MTOTO NJE YA NDOA
adv1
0 comments:
Post a Comment