Msemaji wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Josephat Torner
CHAMA
cha Albino Tanzania (TAS), kimetoa miezi mitatu kwa Rais Jakaya Kikwete
kuingilia kati vitendo vya mauaji ya albino yanayoendelea nchini.
Akishindwa kuchukua hatua, watamshitaki Umoja wa Mataifa (UN).
Akizungumza
Afisa Habari wa TAS, Josephat Torner amesema, wamechoshwa na vitendo
vya mauaji ya albino vinavyoendelea huku Rais Kikwete akiwa kimya.
Torner
amesema Rais Kikwete ni rais wa Watanzania wote hivyo analazimika
kukomesha mauaji ya albino na akishindwa kuchukua hatua katika kipindi
hicho walichompa watapeleka malalamiko yao UN.
Alisema
watalazimika kufika huko kwani chama chao kimesajiliwa chini ya UN
hivyo wakishindwa kusaidia wa Rais Kikwete watalazimika kukimbilia huko
ambako wana imani watasaidiwa.
Msemaji
huyo alisema kabla ya kupeleka malalamiko yao UN watafanya maandamano
makubwa Machi 2, 2015 nchini nzima, na kwa upande wa Dar es Salaam
wataanzia Ocean Road na kumalizikia Ikulu ambapo wamepanga kumuona Rais
Kikwete na kumpa malalamiko yao.
“Maandamano
hayo ya amani yatakuwa na kauli mbiu ‘MAUAJI YA ALBINO SASA BASI’.
Mikoani Albino wataandamana kwenda ofisi za wakuu wa mikoa kupeleka
vilio vyao,” alisema Torner.
Tangu
mwaka 2006 zaidi ya Albino 76 wameuawa, na majeruhi waliopo ni zaidi ya
56 na makaburi 18 yamefukuliwa na kuchukuliwa miili ya waliozikwa huku
walioachwa na ulemavu wa kudumu ni 11, hakuna muuaji hata mmoja
aliyekamatwa.
0 comments:
Post a Comment