Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mhe Festo Mgina akizungumza na Mwandishi wa habari juu ya maafisa watendaji wa vijiji vyote vya halmashauri ambao si waadilifu katika kufanya kazi walizopewa.
Na Fredy Mgunda,Mufindi
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa inakabiliwa kuwa na watendaji wa vijiji na kata ambao sio
waanilifu kutokana na matumizi mabaya ya fedha za wananchi katika vijiji kitu
kinachosababisha migogoro mingi huko vijijini.
Akizungumza na blog hii mwenyekitii
wa halmashauri ya wilaya ya mufindi Festo Mgina alisema kuwa halmashuri
inakabiliwa na watendaji wa vijiji ambao wanatumia vibaya pesa za wananchi na
ndio sababu inayosababisha kutoitisha mikutano ya hadhara.
“Mimi kama mwenyekiti
wahalmashauri hii ni muumini mkubwa wa utawa bora hasa kwa kuzingatia dhana ya
uwazi na uwajibikaji kwasasababu nikizangatia dhana hii basi kila kitu kitaenda
vizuri tatizo watendaji wangu hawataki kabisa dhana ya uwazi na uwajibikaji
yaani watendaji wangu wa vijiji wengi wao ni mizigo tu kwangu” alisema Mgina
Mgina alisema kuwa wamekuwa
wakiwawajibisha pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji hao wa vijiji ili
kuepuka migogoro kwa wananchi.
“Wananchi wanachanga pesa za
maendeleo lakini unakuta mtendaji ametoka alikotoka na kuanza kuzitafuna pesa
za wananchi hiyo sio haki jamani niseme ukweli maafisa watendaji wangu wa
vijiji si waadilifu na nitatizo kubwa linalosababisha migogoro mingi huko
vijijini”alisema Mgina
Aidha Mgina amekiri kuwa na
ubungufu wa maafisa watendaji wa kata na vijiji na ndio sababu inayosababisha
kukaimisha viongozi wengine wa serikali kushika nafasi za kuwa maafisa za
watendaji.
“Saizi tunawatumia waajiliwa
wa serikali hasa maafisa kilimo kuwa watendaji wa vijiji kutokana na kuwa
uhabari wa wanayakazi wa kada hiyo na labda niseme ukweli nimepiga marufuku
waalimu kukaimishwa nafasi hiyo kwa kuwa hata walimu wengi wamekuwa
wakisababisha migogoro kutokana n wao kutokujua nini cha kufanya” alisema Mgina
Mgina alisema endapo Rais wa
Jamhuri wa muungano Dr John Pombe Magufuli akitoa ruhusa za kuanza kuajili
tutajili watendaji wengi na kuwafukuza watendaji wote ambao sio waandilifu kwa
kuwa wanaitia doa halmashauri ya Mufindi.
“Waandishi wa habari mkoani
Iringa mmekuwa mashaidi kwa kutoa habari mbaya za utendaji mbovu wa baadhi ya
watendaji wa vijiji na kata sasa njia sahihi ni kufukuza kazi tu maana tumekuwa
tukiwaonya mara kwa mara lakini hawabadiliki bora kuwafukuza tu angalia radio
Ebony fm,Nuru fm, magazeti,tv na blogs mbalimbali zinatoa habari mbaya za halmashauri
ya Mufindi zinazosababishwa na maafisa watendaji” alisema Mgina
Lakini Mgina aliwashukuru
shirika la LEAT kwa jitihada zao za kutoa elimu ya utawala bora kitu
kilichowasaidia wananchi kuwa na uelewa mkubwa wa kuhoji kwa viongozi wao ambao
si waadilifu ndio maana mara kwa mara tumeona viongozi wakifukuzwa katika
nafsi zao za kiungozi.
Kwa upande wake afisa habari wa shirika la LEAT Edina Tibaijuka alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasimamia vilivyo watendaji wa vijiji ili kuzitunza Maliasili walizonazo kwa kuwa wao ndio wanajukumu hilo.
Kwa upande wake afisa habari wa shirika la LEAT Edina Tibaijuka alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasimamia vilivyo watendaji wa vijiji ili kuzitunza Maliasili walizonazo kwa kuwa wao ndio wanajukumu hilo.
1 comments:
Sio watendaji tuu na madiwani wake......
Post a Comment