Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia), akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni Hamisi Ramadhani wakati wa uzinduzi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Miradi Endelevu wa SBL, Hawa Ladha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) na Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo.
Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako , akisoma hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo. Kulia ni Diwani wa Viti Maalumu, Mwanakombo Mwinyimvua na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa katika eneo hilo.
Hii ni Crew nzima ya Kampuni ya Concept waratibu wa masuala yote ya mawasiliano ya SBL.
Mwonekano wa mradi huo.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyanja akizungumza kwenye hafla hiyo kuhusu mradi huo.
Uzinduzi ukiendelea. |
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Bia Serengeti leo
imezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo
katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam ikiwa
ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.
Ukiwa na uwezo kwa kuhudumia
watu 4,000 mradi huo unajumuisha kisima pamoja na mifumo
yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la
maji ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila masaa ishirini
na nne.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie alisema kuwa
mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni miongoni
mwa mikakati kama hiyo ambayo kampuni ya
bia imeiendesha katika mikoa ya Iringa,
Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha zaidi
ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.
Weesie alisema kwamba mradi wa
Chang’ombe sio tu kwamba utaboresha afya za wakazi wa
eneo hilo bali pia utaongeza tija kiuchumi, “hususani kwa watoto wa
kike na wanawake ambao hawatahitaji kutumia saa
nyingi kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya
kuhudhuria shule wakiwa huru.”
“SBL ina sera iliyojikita
katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne
ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo
lake kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Weesie akielezea
vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na
Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.
Mkurugenzi huyo Mtedaji aliendelea
kusema SBL ina programu ya kilimo ambayo katika kipindi cha miaka
mitatu iliyopita imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa
kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na
maisha ya jumuia zao.
Weesie alisema kutokana na
juhudi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa
wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 10,000 na hili
limechangia katika kukua kwa kampuni na
kukuza kipato cha wakulima.”
Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia
katika kukua kwa uchumi wa taifa kupitia malipo ya kodi
ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa
hususani katika kutoa huduma ya
maji safi na salama ndani ya nchi.”
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
0 comments:
Post a Comment