Thursday, June 22, 2017

ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILLE WA KKKT DAYOSISI YA IRINGA KUANZA KAZI RASMI TAREHE 25 / 6 / 2017

Katibu mkuu KKKT dayosisi ya Iringa Nayman chavala akizungumza na wanahabari

Na Fredy Mgunda, Iringa

KANISA la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa limesema maandalizi ya kumwingiza kazini askofu mteule litafanyika jumapili huku likimpongeza Rais Dkt John pombe Magufuli kwa utendaji kazi.

Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala ameyasema hayo leo

wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari kuhusu maandalizi yaliyofikiwa ya sherehe kubwa ya kuwekwa wasifu kwa askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi Saga.

Alisema kuwa sherehe za kumpa madaraka ya kuanza kufanya kazi kama askofu wa kanisa la KKT Jimbo la Iringa mchungaji Gavile na msaidizi wake Saga itafanyika jumapili ya june 25 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Gangilonga .

Kuwa ibada hiyo itaongozwa na askofu mkuu wa KKKT Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella na kuwa kabla ya idaba kutakuwa na maandamano ya wachungaji na washarika yatakayoanzia usharika wa kanisa kuu hadi Gangilonga.
" Tunaomba wananchi wote na washarika kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria pia tunategemea kuwa na viongozi mbali mbali wa serikali na wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya Tanzania"

Chavala alisema maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya tukio hilo kubwa ambalo lilikuwa likisubiliwa kwa shauku kubwa .

Askofu Gavile amechukua nafasi ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Dkt Mdegella ambaye alistaafu kwa heshima kubwa na kuacha heshima ya aina yake ndani ya KKKT .

Wakati huo huo Katibu huyo amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya kuwatumikia watanzania kwa uadilifu mkubwa na kuwa kazi kubwa kwa watanzania ni kuendelea kumpa ushirikiano .

Kwani alisema kuwa hatua ya kuwabana wasio waadilifu pamoja na kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu (MAKINIKIA) ni hatua ya kupongezwa kwani suala hilo lilikuwa likiwanufaisha wachache huku Taifa likibaki patupu .

" Sisi kama kanisa tumekuwa tukimuombea kila wakati tena kwa kumtaja kwa jina na hatutachoka kuendelea kumuombea maana kazi anayoifanya ni ngumu ambayo silaha kubwa ni maombi "

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More