Na Mwandishi wetu, Arusha
Mtandao wa Wasanii wa Injili na Maadili ya Utaifa Tanzania (Tagoane) umeandaa tamasha kubwa la ‘Tanzania Mama Niwathamani’ linaloitwa Tamani Festival "Asante Mama" lenye lengo la kumshukuru Mungu kwa ajili ya Mwanamke(Mama), kuonyesha thamani ya mama (Mwanamke) na kurejesha shukrani kwa mama kutokana na umuhimu wake kwenye jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Tagoane Dkt. Godwin Maimu alisema tamasha hilo litakalofanyika June 29-Julai mosi jijini Arusha litawashirikisha watu wengi wakiwamo wanamuziki wa Injili.
Alisema lengo hasa ni kurejesha shukrani kwa ‘mama’ Asante Mama ambapo pamoja na mambo mengine, watu watachangia damu salama kwa ajili ya kuokoa uhai wa mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Dkt. Maimu alisema sio hivyo tu, tamasha hilo litatoa fursa kwa wanawake kupima afya bure yakiwemo magonjwa mbalimbali kama saratani, figo,shinikizo la damu na mengine yasiyo ya kuambukiza.Hivyo watakuwepo madaktari wabobezi kwa ajili ya kuangalia afya za mama zetu, ni sisi tunaopaswa kuangalia uhai wao na sio mwingine,” alisema.
“Ni tamasha kubwa la siku tatu, japo kutakuwa na uimbaji na mambo mbalimbali tutakuwa na Maonyesho ya kazi za ubunifu na ujasiriamali za kina mama kwa kuinua uchumi wao, mafunzo mbalimbali ya ujasiria mbali, maombezi na fursa za kunyanyuka kiuchumi.
Alitaja mengine yatakayofanyika kwenye tamasha hilo ni onyesha upendo la uzalendo kwa mama kutoa zawadi maalumu kwa mama (Asante Mama)ikiambatana na ziara maalumu ya kutembelea hifadhi za Taifa Manyara na Tarangire ikiwa ni kuenzi utalii wa ndani kwa vitendo aliongeza Dkt.Godwin Maimu Rais wa Tagoane.
Saturday, June 2, 2018
NAIBU WAZIRI JULIANA SHONZA MGENI RASMI TAMASHA LA TAGOANE ARUSHA
Saturday, June 02, 2018
mwangaza wa hbari
No comments
0 comments:
Post a Comment