Wednesday, June 28, 2017

KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu Tanzania jijini Dar es Salaam le...

WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO.

Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru. Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro. Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika. Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA IDD EL FITRI KATIKA MSIKITI WA RIADHA MJINI MOSHI.

Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa akiwasili katika msikiti wa Riadha mjini Moshi kwa ajili ya Swala ya Eid el Fitri iliyofanyika kitaifa mjini Moshi. Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa aikishiriki Swala ya Idd el Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi. Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakishitiki Swala Idd. Swala ya Idd ikifanyika katika msikiti wa Riadha mjini Moshi. Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa,akiwa na Sheakh Mkuu wa Tanzania ,Mufti Abubakary Zubery ,Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu ,Said Mwema. Mshindi wa kuhifadhi Quran tukufu...

WAISLAMU WATAKIWA KUENDELEZA UCHA MUNGU

Na Swahilivilla Washington Waislamu wametakiwa kuendeleza Ucha Mungu na mema waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh Yussuf Mecca, kutoka Columbus, Ohio Wito huo ulitolewa jana na Sheikh Yussuf Mecca alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Iddi zilizoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania wa Jiji la Washington na Vitongoji vyake ijulikanayo kwa jina la TAMCO. "Kwa vile mwezi wa Ramadhani umekwisha isiwe yale yote mazuri tuliyokuwa tunayafanya ikawa ndiyo basi, na tusubiri Ramadhani nyengine" alisema Sheikh Yussuf. Aliendelea kusisitiza umuhimu wa kujitahidi kumcha Mungu wakati wowote na kujitahidi katika kutenda mambo mema na ibada ili kujiandaa na safari ya Akhera ambayo inanaweza kumfikia mtu wakati...

Saturday, June 24, 2017

ZAIDI YA VIJANA 400 WAPATA ELIMU YA UJASILISIAMALI KUTOKA KWA MBUNGE RITTA KABATI

 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akitoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana zaidi ya 400 wa kanisa la kikatoriki parokia ya Ismani Mkoani Iringa  Baadhi ya vijana walishiriki katika mafunzo ya kupewa elimu ya ujasiliamali katika kanisa la parokia ya Ismani Na Fredy Mgunda, Iringa Zaidi ya vijana mia nne (400) wa kikatoriki kutoka katika parokia kumi zinaizunguka Manispaa ya Iringa wamepata elimu ya ujasiliamali kutoka kwa mbunge wa viti maalum Mkoani kupitia chama cha mapinduzi (CCM). Mafunzo hayo yametolewa katika Kanisa la kikatoriki parokia ya Ismani linaloongozwa paroko Leonard Maliva. Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo mbunge wa viti maalumu Ritta Kabati alisema kuwa ujasiliamalia ni kitendo...

Friday, June 23, 2017

AKINAMAMA WALIMA NYANYA KINYEREZI DAR WAJIFUNZA KILIMO CHA UYOGA

Mafunzo kwa vitendo. Akinamama wa Kinyerezi Green Voices wakiweka udongo kwenye mifuko kama maandalizi ya kilimo cha uyog...

FANYA YAFUATAYO KUNOGESHA SIKUKUU YA EID-AL-FITR

Na Jumia Travel Tanzania Ni siku chache zimebakia kabla ya waumini wa dini ya kiislamu nchini na duniani kote kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Zipo namna tofauti za kusherehekea sikukuu hii kulingana na sehemu watu walipo. Jumia Travel ingependa kukushirikisha mambo yafuatayo ambayo yanaweza kuifanya sikukuu hii kuwa ya tofauti na kipekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka.      Fanya maandalizi pamoja na familia. Katika kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia sikukuu basi ni vema ukawashirikisha kwenye maandalizi yake. Kama baba au mama wa familia na una watoto au ndugu unaishi nao litakuwa ni jambo zuri kama mtafanya hata kikao kidogo na kujadili. Kwa mfano,...

SBL YAZINDUA MRADI WA MAJI KWA WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia), akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni Hamisi Ramadhani wakati wa uzinduzi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68  uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Miradi Endelevu wa SBL, Hawa Ladha.&nbs...

Thursday, June 22, 2017

ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILLE WA KKKT DAYOSISI YA IRINGA KUANZA KAZI RASMI TAREHE 25 / 6 / 2017

Katibu mkuu KKKT dayosisi ya Iringa Nayman chavala akizungumza na wanahabari Na Fredy Mgunda, Iringa KANISA la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa limesema maandalizi ya kumwingiza kazini askofu mteule litafanyika jumapili huku likimpongeza Rais Dkt John pombe Magufuli kwa utendaji kazi. Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari kuhusu maandalizi yaliyofikiwa ya sherehe kubwa ya kuwekwa wasifu kwa askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi Saga. Alisema kuwa sherehe za kumpa madaraka ya kuanza kufanya kazi kama askofu wa kanisa la KKT Jimbo la Iringa mchungaji Gavile na msaidizi wake Saga itafanyika jumapili...

Tuesday, June 20, 2017

UNESCO YATOA TAHADHARI ONGEZEKO LA JANGWA

Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu. Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo - hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa. Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya 'wakimbizi wa mazingira' sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. Na hili hii inategemewa kundelea kuongezeka. Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka 2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na Ulaya. Utabiri huu unaonyesha...

"NEXT EINSTEIN" YAZINDUA WIKI YA SAYANSI AFRIKA TANZANIA

Mtaalamu wa masomo ya Sayansi, Fadhil Leonard akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza gari linalojiendesha bila ya kuwa na dereva wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sayansi Afrika Tanzania iliyofanyika  katika viwanja vya Shule ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam leo.&nbs...

VIDEO: BUNGE LA WATOTO LAVUTIA WENGI MKOANI MWANZA

Jana juni 16,2017 mataifa mbalimbali barani Afrika yaliungana pamoja kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkoani Mwanza, maadhimisho hayo yalifanyika uwanja wa Furahisha kwa kujumuisha matukio mbalimbali ya watoto. Wengi walivutiwa na kipengere cha bunge la Watoto mkoani Mwanza kwenye maadhimisho hayo yaliyokuwa na kaulimbiu ya "Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto. Tazama video ...

ZIFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM

Na Jumia Travel Tanzania Umaarufu wa Dar es Salaam kwenye shughuli za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu kuvizingatia vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa kuviona tu lakini bila ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana na wageni huja wakitokea nchi mbalimbali kujifunza.   Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi eneo la Oyster Bay, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba unaweza kujifunza na kufurahia mambo mengi pindi utakapotembelea maeneo yafuatayo. Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni. Makumbusho haya awali yalifunguliwa mwaka 1940 kama kumbukumbu ya Mfalme George wa tano ambapo kihistoria huwarudisha watanzania nyuma walipotokea. Makumbusho...

Friday, June 16, 2017

Save the Children yaadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika Dar

Shirika la Save the Children nchini limeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kukutana na Watoto mbalimbali wa shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo Walimu na Maafisa wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii walishiriki na kuchangia mijadala iliyoibuliwa na watoto wenyewe kuhusu malengo ya usawa na haki ya jinsia ifukapo mwaka 2030.  Katika tukio hilo baadhi ya shughuli walizofanya watoto ni pamoja na kuibua mijadala ya Haki na Wajibu wa Mtoto, Unyanyasaji na changamoto za kurepoti kesi za unyanyasaji. Watoto walipata majibu jinsi ya kuripoti kesi za ukatili na unyanyasaji katika kituo cha dawati la jinsia kwenye kituo cha Polisi karibu nao. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi...

Page 1 of 69412345Next
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More