frank Kibiki ambaye pia ni Mwanahabari wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa mkoani |
frank Kibiki akionyesha walivyo kosea jina lake. |
WAKATI
kura za maoni za kutafuta wagombea ubunge katika majimbo yote nchini kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM) zikipigwa leo, mmoja kati ya wagombea 13 wanaotafuta
nafasi hiyo Jimbo la Iringa Mjini, Frank Kibiki anataka zoezi hilo jimboni humo
libatilishwe.
Wagombea
wengine ni pamoja na Dk Augustino Maiga, Dk Yahaya Msigwa, Frederick
Mwakalebela, Nuru Hepautwa, Michael Mlowe, Aidan Kiponda, Addo Mwasongwe, Jesca
Msambatavangu, Mahamudu Mgimwa, Peter Mwanilwa na Fales Kibasa.
Akizungumza
na wanahabari hii leo, Kibiki ambaye pia ni Mwanahabari wa Magazeti ya Uhuru na
Mzalendo wa mkoani hapa alisema kura hizo zinapoteza uhalali kwasababu jina
lake limekosewa.
“Mimi
naitwa Frank John Kibiki, lakini kwenye karatasi ya kupigia kura ameandikwa
mgombea mpya aliyetajwa kwa jina la Frank John Kibiri,” alisema.
Alisema
kwa kuwa Frank Kibiki na Frank Kibiri ni watu wawili tofauti, hawezi kukubali
kutumia jina la Kibiri ili kuhalalisha mchakato huo na endapo atafanya hivyo
wagombea wenzake wanaweza kukata rufani kupinga matokeo hayo.
Kibiki
alisema ameandika barua ya malalamiko yake kwa uongozi wa CCM wa Manispaa ya
Iringa huku kopi ya malalamiko hayo yanayotaka uchaguzi huo ufanyike upya baada
ya karatasi ya kupigia kura kusahihishwa akiipeleka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa
Iringa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
Akikiri
kupokea barua ya mlalamikaji huyo na dosari iliyojitokeza kwenye karatasi hizo
za kupigia kura, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi alisema; “suala
hili tulikubaliana na mgomea huyo tulimalize kwa kusahihisha kwa peni jina hilo.
Baada ya kuifanya kazi hiyo kabla ya zoezi lenyewe la upigaji kura kuanza,
zoezi limeendelea kama kawaida.”
Taarifa
ya Mwampashi imepingwa na Kibiki mwenyewe aliyesema katika vituo 81 kati ya 90
vya upigaji kura alivyotembelea ni kituo kimoja tu cha Umati alichokuta jina
lake limerekebishwa katika karatasi hizo.
Huku
akiahidi kuishtaki kampuni iliyopewa kazi ya kuchapisha karatasi hizo kwa
kukosea jina lake, Kibiki alisema; “katika hili sitanyamaza, nitakuwa sauti ya
yoyote aliyewahi kuonewa ndani ya chama
vinginevyo nitalazimika kusubiri miaka mitano ijayo ili nishriki kwenye
mchakato mwingine wa haki.” Alisema.
Wakati
huo huo Katibu wa CCM wa Manispaa hiyo amezungumzia idadi ya wana CCM
waliojitokeza katika mchakato huo wa kura za maoni kuwa ni ndogo ikilinganishwa
na matarajio yao ya kushirikisha wanachama zaidi ya 18,000.
0 comments:
Post a Comment