Na Mathias Canal, Iringa
vijijini Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia Umoja wa
katiba ya Wananchi {UKAWA} kimezindua kampeni zake katika Jimbo la Kalenga
lililopo mkoani Iringa kwa muktadha wa kuanza vyema mikikimikiki ya kumnadi
mgombea wake ambaye mara kadhaa amesikika akisema jimbo hilo limekosa
muwakilishi wa wananchi bungeni.
Chadema/ukawa inataraji kuanza kampeni zake za kumnadi mgombea wa Urais,
wagombea ubunge, na udiwani mara baada ya uzinduzi wa kampeni zinazotaraji
kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
zilizofanyika katika eneo la Ifunda, mgombea ubunge kwa tiketi ya
Chadema/Ukawa, Mdede Mussa Leonard amesema kuwa ameamua kugombea jimbo hilo kwa
kuwa ni mkazi wa Kalenga hivyo hakusoma kwenye kitabu changamoto za jimbo na
wala hana haja ya kusimuliwa.
Amesema kuwa lengo mahususi la kugombea jimbo hilo ni kuhakikisha
anaibana serikali na kushirikiana na wanakalenga wa ndani na nje ya jimbo na
wadau mbalimbali wamaendeleo kuhakikisha Jimbo hilo linakwamuliwa kutoka kwenye
mkwamo wa maendeleo na huduma duni za kijamii.
Ameeleza kusikitishwa sana na ukosekanaji wa maji jimboni hapo, ukosefu
wa barabara nzuri ambazo zitawasaidia wananchi kusafirisha mazao yao, gharama
kubwa za elimu ambapo ameeleza kuwa serikali imefuta ada kwa shule za serikali
lakini imesahau kufuta michango ambayo ndiyo imekuwa mikubwa zaidi.
Mdede ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Kipera, Kata ya Nzihi, ana umri wa
miaka 27, shahada ya udaktari ya chuo kikuu cha Afya ya tiba Bugando amewahi
kuwa Rais wa chuo hicho kwa kipindi cha mwaka mmoja sawia na kuwa Rais wa vyuo
vikuu vyote Tanzania bara na visiwani TAHLISO.
Mdede amekuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na
mwaka 2012-2013 alikuwa muasisi na mwenyekiti wa Chadema chuo kikuu cha
Bugando, 2013 alipokuwa mwenyekiti wa chadema kwa vyuo vyote vya mkoa wa
Mwanza.
Aidha Mdede ameshiriki mafunzo ya uongozi kwa marais wa vyuo vikuu vya
Afrika Mashariki yaliyofanyika Arusha mwaka 2013 sambamba na kuhudhuria ziara
ya mafunzo kiuongozi nchini China.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni
jimboni humo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chadema ngazi ya Jimbo,
Wilaya na mkoa, Mdede alisema kuwa jimbo hilo lina jumla ya Kilomita 4038.1,
Wakazi 15079,Tarafa 3,Kata 15,Vitongoji 434, na Vijiji 75, hivyo anaamini
endapo watampa ridhaa atafika kila mahali na kuhakikisha changamoto za wakazi
wa jimbo hilo zinatatuliwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Iringa, Leonce marto
amesema kuwa serikali ya chama cha mapinduzi ambayo inamaliza muda wake
imeshindwa kuwawezesha wananchi kupata hata pembejeo za kilimo, pamoja na nchi
ya Tanzania kuwa na rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na madini, gesi, maziwa,
bahari na vivutio mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbuga za wananyama.
Alisema Tanzania imekosa mafanikio na kuendelea kubaki nyuma kimaendeleo
kwa sababu ya udhalimu na ubovu wa uongozi wa CCM ambao asilimia kubwa
wanatuhumiwa katika kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufisadi.
0 comments:
Post a Comment