akiwa na katibu wa ccm iringa vijijini
NA MWANDISHI WETU,IRINGA.
Baada ya zoezi la
uchaguzi wa wagombea urais kukamilika katika vyama sasa zoezi limeanza kwa
wabunge na madiwani ambapo hii leo Festo Kiswaga ambaye ameweka nia ya kugombea
katika jimbo la isiman.
Katika mkutano huo na
waandishi wa habari KIswaga amekanusha uvumi uliokuwa umezagaa juu ya kuhongwa
pesa mwaka 2010 ili kutogombea huku akidai kuwa alishindwa kwa haiki na si
hongo ya mbunge aliyepo madalakani kwasasa huku akimzawadia ukuu wa wilaya.
Ambapo pia ametumia
mkutano huo ili kuujulisha uma juu ya maelengo yake ya kuchukua form katika
wasifu wake amesema anadigree ya sayansi ya wanyama poli na kutumikia katika
shirika la mbomipa na kuwatumikia wananchi wa misenyi mkoa wa kagera akiwa ni
mkuu wa wilaya na sasa ni mkuu wa wilaya ya Nanyumbu huku akitumikia mashirika
kama tanapa na chuo kikuu cha dar es-laam na kuteuliwa kuwa rais wa wa
shirikisho vyuo vikuu vya umoja wa Afrika mashariki uliojumuisha vyou vikuu
zaidi ya 400 katika nchi
za Tanzania,Uganda,Kenya na Burundi.
Akizungumzia kuhusu
janga la njaa lililopo katika jimbo hilo amekiri kuwa anauzoefu juu ya utatuzi
wa matatizo kama hayo kutokana na nyanja mbalimbali ambazo amepitia na pia
amewataka wananchi wa ismani kumpa lidhaa yya kuwaongoza kutokana tatizo kama
hilo amelikuta katika wilaya ya Namnyumbu na akafanikiwa kulitatua kwa asilimia
100%.
Aidha amesema kutokana
na jimbo hilo kukosa kiongozi mwenye uchungu kama yeye imepelekea kukosekana
kwa huduma kama maji katika vijiji mbalimbali ikiwa jimbo hilo limefikisha
miaka 20 ikiwa mashirika mbalimbali na serikali licha ya kuchangia lakini
ukosefu wa maji umekuwa tatizo si kwa binadamu tuu bali hata kwa mifugo ambapo
hupelekea wananchi kununua maji hadi kwa shiringi mia 500.
Kwaupande wa wananchi
waliohudhulia mkutano huo wamekiri kuwapo kwa tatizo hilo ambalo imekuwapo kwa
miaka mingi sasa hali inyopelekea wananchi upeleka mifugo yao kunywesha usiku
wa manane hali ambayo ineza kuhatarisha usalama wa mifugo hiyo.
Nao kinamama wamekiri kuwa tatizo hilo
limekuwa likiwaathiri kiuchumi kwakuwa hutumia muda mwingi katika kutafuta maji
bila kufanya shughuli nyingine kwaajiri ya kujenga uchumi wao na wanchi.
0 comments:
Post a Comment