katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA
MWAMPASHI
katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA
MWAMPASHI
KEKI ILIYOKUWA IMEANDALIWA SIKU YA SHEREHE HIYO.
Baadhi ya wanachama
wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
Baadhi ya wanachama
wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini wamefanya
maafari yao katika ukumbi wa chama hicho sabasaba.
Wakizungumza wakati wa sherehe hiyo wanafunzi hao wamesema
kuwa sas ccm italajia kurudisha jimbo la iringa mjini kwasababu tayari makatibu
wa chama hicho wameweza kuwarudisha vijana kukipenda chama hicho.
Aidha wamesema kuwa
chama hicho kilipoteza mvuto kwa vijana na vijana walipoteza mvuto na
chama hicho,hivyo chama hicho kwa sasa kimerudisha imani kwa vijana na wanachama wengine.
“Sisi hapa chuoni kwetu tulikuwa wanachama wachache ila kwa sasa tupo wengi na kila siku
wanachama wanazidi kuongezeka kutokana na kukipenda cha hicho kwa wakati huu
tukielekea katika uchaguzi mkuu”walisema wanafunzi hao.
Mbunge wa jimbo hili kwa sasa mchungaji PETTER MSIGWA
ajiandae kuondoka kutoka na chama hicho kujipanga kila kona na tayari
wamejihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuongeza kuwa
wananchi wa manispaa ya iringa wanapenda amani na sio vurugu.
Lakini walimpongeza katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA
MWAMPASHI kwa kufanya kazi nzuri
iliyosababisha wananchi wa jimbo hili kurudisha imani na chama hichi na
kuongeza kuwa MWAMPASHI ni kiongozi mzuri na anajua majukumu yake hivyo ni
vizuri wananchi wa manispaa tukashikiana na jembe hili kulikomboa jimbo hili.
Kwa upande wake KATIBU WA JIMBO HILI ELISHA MWAMPASHE ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo aliwapongeza wanachama wa chama hicho
tawi la tumaini kwa kukikuza chama hicho na kuongeza wanachama.
MWAMPASHI akawataka wanachama hao kukipigania chama hicho
katika uchaguzi mkuu ujao ili waweze kushinda kwa kishindo kikubwa na
kuwaachawapinzani hoi.
“Tunanguvu na nia ya kufanya vizuri katika uchaguzi wa mwaka
huu kwa kuwa tumejipanga kili kona na tumerudisha inmani kwa wananchi wote
hivyo kazi kwa sasa imekuwa rahisi hasa kulikomboa jimbo la iringa mjini ambalo
walilikopesha kwa mpinzani”alisema MWAMPASHI.
Aidha MWAMPASHI aliwataka wananfunzi kuacha kufanya mambo ya
kizinaa pindi wapatapo kazi kwa kudai kuwa anakura ujana ,akaongeza kuwa sasa
ni wakati wa vijana kuwekeza katika biashara mbalimbali ili kujitengenezea
maisha mazuri hapo baadae.
“Nawaomba jamani tusiwe na tamaa katika kutafuta maendeleo
kwa kuiba au kutoa na kupokea rushwa kwa
kuwa hiyo njia sia sahihi kwani hapo mtakuwa mkirudisha maendeleo nyuma na sio
kuendelea kuleta maendeleo”.alisema MWAMPASHI.
Alimalizia kwa kumtaka mbuge wa jimbo hili kufungasha vitu
vyake kwa kuwa muda wake umeisha na wananchi wa manispaa ya iringa wamemchoka
kwa kuwa toka ameingia madarakani hakuna alichokifanya katka kuleta maendeleo
ya jimbo hili zaidi kuanzisha migomo na vurugu katika sehemu mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment